Mbeya: Mhandisi aswekwa ndani kwa kutafuna Bilioni tatu za mradi wa maji. Adai kujenga Kibanda cha mabati cha 'site' kwa Milioni 100

hii ilitokea enzi za mwendazake, inaonyesha uko outdated na yanayotokea TZ....au labda ulikuwa unasaidiana na vikosi vya Talebani kule khost na Kunduz....
 
Waziri wa Maji, Prof. Makame Mbarawa ameamuru Jeshi la Polisi kumkamata na kumuweka mahabusu Mhandisi Alistides Kanyomo wa kampuni ya Mbesso Construction kutoka Jijini Dar es Salaam

Kwa tuhuma za ubadhirifu wa zaidi ya shilingi bilioni tatu za Ujenzi wa mradi wa Maji Katika Bonde la Mwakaleli wilayani Rungwe na kusababisha wananchi katika vijiji 18 vya Halmashauri za Busokelo na Rungwe kukosa Maji kwa kipindi cha miaka 11.
Katika shughuli zangu za kikazi mkoani Mbeya kuangalia matatizo ya huduma za jamii katika wilaya za Mbeya, nilikutana na issue ambayo niliombwa nisiiripoti kwa Waziri wa Maji. Leo naomba kuungama dhambi zangu hapa kwa kukaa kimya dhidi ya ufisadi uliofanywa na huyu Mhandisi.

Serikali ilitoa fedha kwa ajili ya kufikisha maji katika wilaya yo Rungwe. Hili lilihusu kununua mabomba ya maji ili na kuyatandaza kutoka Mlima Rungwe ili maji yaweze kufika maeneo ya mji wa Tukuyu kwa njia ya gravity.

Sasa huyu Mhandisi wa Maji aliamua kuingilia mchakato wa ununuaji wa mabomba ya maji na kusababisha ununuaji wa mabomba yasiyo na kiwango ili kuweza kukwapua fedha za juu. Mabomba ya bei ya chini yalinunuliwa na yakawa hayana kiwango kabisa, na huyu Mhandisi hakukubali kuingiliwa.

Haya mabomba yalitandazwa toka mlima Rungwe hadi mji wa Tukuyu. Siku maji yalipofunguliwa, mabomba yalianza kupasuka moja baada ya jingine kutokana na pressure ya maji, kwa kuwa mabomba hayakununuliwa kwa kuangalia yatahimili pressure kiasi gani.

Huyu jamaa alionekana kuwa karibu na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, na sasa jambo hili waliamua kulizima yeye na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kwa kuahidi kwamba wangetafuta fungu jingine la fedha ili kuziba hii kashfa.

Nilipokuwa Mbeya wadau wao wakanisihi sana nisiliseme hili kwa kuwa tayari walikuwa wana suluhisho. Nilihofia maisha yangu kwa sababu namna waliyokuwa wananisihi ni kama walikuwa wanatishia uhai wangu. Niliwauliza baadhi ya wakazi wa Tukuyu ikiwa kweli walikuja kutatuliwa tatizo la maji nikaambiwa hakuna kilichofanyika.

Nilipoona Mkuu wa Mkoa ni mtu wa karibu wa Raisi Magufuli niliamua kuliacha bila kulisema, sikutaka complications na kupoteza uhai wangu kwa ajili ya ufisadi wao
 
Matatizo ya ulaji hela za umma ni janga la siku nyingi. Investigative journalism ilikuwa inaumbua madudu haya kwa wingi. Serikali kama kinara wa madudu ikaona inadhalilika, ikatunga sheria kuzuia. Kuumbua uharifu ikawa ni uharifu. Nikaamini ukiona kuumbua uharifu unaonekana ni mharifu elewa unatawaliwa na waharifu.
 
Haya tumesikia tusubirie aje kulipa faini ya shilingi milioni mbili au jela miezi 6.....hii nchi bhana tunawachangia watu tu waishi maisha ya ndoto zao.
 
Nchi hii kila mtu mwizi
Uwizi uko damuni mwetu

Ova
 
Katika shughuli zangu za kikazi mkoani Mbeya kuangalia matatizo ya huduma za jamii katika wilaya za Mbeya, nilikutana na issue ambayo niliombwa nisiiripoti kwa Waziri wa Maji. Leo naomba kuungama dhambi zangu hapa kwa kukaa kimya dhidi ya ufisadi uliofanywa na huyu Mhandis....
Hii ni mbaya sana. Inabidi waliohusika wawajibishwe.
 
Nchi hii kila mtu mwizi
Uwizi uko damuni mwetu

Ova
Siyo hivyo mkuu, bali wale wanaopata hizo nafasi huwa ni watu wenye tabia za wizi kwani hata hizo nafasi huzipata kwa mtindo huo, na sababu ni kuwa hao watoa nafasi huwa ni watu wenye tabia zinazofanana.

Siyo rahisi kuwakuta watendaji waaminifu kwenye nafasu nzuri. Waaminifu hupigwa vita ili wasijekwamisha mambo ya wakubwa ambao tayari wametota matope.

System iliyopo ndiyo hiyo, kuisafisha si jambo rahisi.
 
Katika shughuli zangu za kikazi mkoani Mbeya kuangalia matatizo ya huduma za jamii katika wilaya za Mbeya, nilikutana na issue ambayo niliombwa nisiiripoti kwa Waziri wa Maji. Leo naomba kuungama dhambi zangu hapa kwa kukaa kimya dhidi ya ufisadi uliofanywa na huyu Mhandisi.

Serikali ilitoa fedha kwa ajili ya kufikisha maji katika wilaya yo Rungwe. Hili lilihusu kununua mabomba ya maji ili na kuyatandaza kutoka Mlima Rungwe ili maji yaweze kufika maeneo ya mji wa Tukuyu kwa njia ya gravity.

Sasa huyu Mhandisi wa Maji aliamua kuingilia mchakato wa ununuaji wa mabomba ya maji na kusababisha ununuaji wa mabomba yasiyo na kiwango ili kuweza kukwapua fedha za juu. Mabomba ya bei ya chini yalinunuliwa na yakawa hayana kiwango kabisa, na huyu Mhandisi hakukubali kuingiliwa.

Haya mabomba yalitandazwa toka mlima Rungwe hadi mji wa Tukuyu. Siku maji yalipofunguliwa, mabomba yalianza kupasuka moja baada ya jingine kutokana na pressure ya maji, kwa kuwa mabomba hayakununuliwa kwa kuangalia yatahimili pressure kiasi gani.

Huyu jamaa alionekana kuwa karibu na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, na sasa jambo hili waliamua kulizima yeye na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kwa kuahidi kwamba wangetafuta fungu jingine la fedha ili kuziba hii kashfa.

Nilipokuwa Mbeya wadau wao wakanisihi sana nisiliseme hili kwa kuwa tayari walikuwa wana suluhisho. Nilihofia maisha yangu kwa sababu namna waliyokuwa wananisihi ni kama walikuwa wanatishia uhai wangu. Niliwauliza baadhi ya wakazi wa Tukuyu ikiwa kweli walikuja kutatuliwa tatizo la maji nikaambiwa hakuna kilichofanyika.

Nilipoona Mkuu wa Mkoa ni mtu wa karibu wa Raisi Magufuli niliamua kuliacha bila kulisema, sikutaka complications na kupoteza uhai wangu kwa ajili ya ufisadi wao
Lakini hakuwa Chalamila, naamini.

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
Mkuu, labda tu nikwambie Mbarawa alijua juu ya huu ufisadi. Alishaanza kuufuatilia halafu akatemwa na Magufuli. Hawa jamaa waliposikia katemwa wakashangilia sana. Ndio maana aliporudi karudi na usongo nao. Alikuwa na habari zote, na utaona alivyokuwa amekasirika kwenye hiyo clip, kwa kuwa kuna kebehi zilifanyika alipoondolewa na Magufuli hawa jamaa wakiona wame-win!

Kilichonishangaza, ni kwa nini Dr. Tulia hakuingilia na aliamua kukaa kimya na yeye ni mkazi wa Tukuyu ufisadi huu uliathiri ndugu na jamaa zake kule? Ina maana Magufuli alihusika ndio maana akamuondoa Mbarawa alipoanza kufuatilia?
 
Magufuli mambo yake tangu akiwa waziri wa ujenzi yalikuwa mazito. Si vyema kufukua makaburi.

Back
Top Bottom