Komeo Lachuma
JF-Expert Member
- Oct 31, 2014
- 7,926
- 17,030
Ndo ya tozo inakoenda.Yaani wewe ndiyo unaiona leo hii? Mbona ya siku nyingi wakati Mbarawa akiwa waziri wa Maji? Wacha huo uchochezi mkuu, siyo hela ya tozo hiyo!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ndo ya tozo inakoenda.Yaani wewe ndiyo unaiona leo hii? Mbona ya siku nyingi wakati Mbarawa akiwa waziri wa Maji? Wacha huo uchochezi mkuu, siyo hela ya tozo hiyo!
Nakulilia Tanzania, unajengwa na wenye moyo na kuliwa na wenye choyo.
View attachment 1948186
Hii nchi inamutaka mtu Kama JPM na ndio maàna sisi tulimuona shuja
Katika shughuli zangu za kikazi mkoani Mbeya kuangalia matatizo ya huduma za jamii katika wilaya za Mbeya, nilikutana na issue ambayo niliombwa nisiiripoti kwa Waziri wa Maji. Leo naomba kuungama dhambi zangu hapa kwa kukaa kimya dhidi ya ufisadi uliofanywa na huyu Mhandisi.Waziri wa Maji, Prof. Makame Mbarawa ameamuru Jeshi la Polisi kumkamata na kumuweka mahabusu Mhandisi Alistides Kanyomo wa kampuni ya Mbesso Construction kutoka Jijini Dar es Salaam
Kwa tuhuma za ubadhirifu wa zaidi ya shilingi bilioni tatu za Ujenzi wa mradi wa Maji Katika Bonde la Mwakaleli wilayani Rungwe na kusababisha wananchi katika vijiji 18 vya Halmashauri za Busokelo na Rungwe kukosa Maji kwa kipindi cha miaka 11.
11years back! Polisi, takukuru, tiss walikuwa wapi? Bussy with Chadema?
Hapo siamini kama hata koleo watalikuta!Wataifishe mitambo yake kufidia huo uhujumu uchumi/ubadhirifu alioufanya
Hii ni mbaya sana. Inabidi waliohusika wawajibishwe.Katika shughuli zangu za kikazi mkoani Mbeya kuangalia matatizo ya huduma za jamii katika wilaya za Mbeya, nilikutana na issue ambayo niliombwa nisiiripoti kwa Waziri wa Maji. Leo naomba kuungama dhambi zangu hapa kwa kukaa kimya dhidi ya ufisadi uliofanywa na huyu Mhandis....
Siyo hivyo mkuu, bali wale wanaopata hizo nafasi huwa ni watu wenye tabia za wizi kwani hata hizo nafasi huzipata kwa mtindo huo, na sababu ni kuwa hao watoa nafasi huwa ni watu wenye tabia zinazofanana.Nchi hii kila mtu mwizi
Uwizi uko damuni mwetu
Ova
Lakini hakuwa Chalamila, naamini.Katika shughuli zangu za kikazi mkoani Mbeya kuangalia matatizo ya huduma za jamii katika wilaya za Mbeya, nilikutana na issue ambayo niliombwa nisiiripoti kwa Waziri wa Maji. Leo naomba kuungama dhambi zangu hapa kwa kukaa kimya dhidi ya ufisadi uliofanywa na huyu Mhandisi.
Serikali ilitoa fedha kwa ajili ya kufikisha maji katika wilaya yo Rungwe. Hili lilihusu kununua mabomba ya maji ili na kuyatandaza kutoka Mlima Rungwe ili maji yaweze kufika maeneo ya mji wa Tukuyu kwa njia ya gravity.
Sasa huyu Mhandisi wa Maji aliamua kuingilia mchakato wa ununuaji wa mabomba ya maji na kusababisha ununuaji wa mabomba yasiyo na kiwango ili kuweza kukwapua fedha za juu. Mabomba ya bei ya chini yalinunuliwa na yakawa hayana kiwango kabisa, na huyu Mhandisi hakukubali kuingiliwa.
Haya mabomba yalitandazwa toka mlima Rungwe hadi mji wa Tukuyu. Siku maji yalipofunguliwa, mabomba yalianza kupasuka moja baada ya jingine kutokana na pressure ya maji, kwa kuwa mabomba hayakununuliwa kwa kuangalia yatahimili pressure kiasi gani.
Huyu jamaa alionekana kuwa karibu na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, na sasa jambo hili waliamua kulizima yeye na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kwa kuahidi kwamba wangetafuta fungu jingine la fedha ili kuziba hii kashfa.
Nilipokuwa Mbeya wadau wao wakanisihi sana nisiliseme hili kwa kuwa tayari walikuwa wana suluhisho. Nilihofia maisha yangu kwa sababu namna waliyokuwa wananisihi ni kama walikuwa wanatishia uhai wangu. Niliwauliza baadhi ya wakazi wa Tukuyu ikiwa kweli walikuja kutatuliwa tatizo la maji nikaambiwa hakuna kilichofanyika.
Nilipoona Mkuu wa Mkoa ni mtu wa karibu wa Raisi Magufuli niliamua kuliacha bila kulisema, sikutaka complications na kupoteza uhai wangu kwa ajili ya ufisadi wao
Mkuu, labda tu nikwambie Mbarawa alijua juu ya huu ufisadi. Alishaanza kuufuatilia halafu akatemwa na Magufuli. Hawa jamaa waliposikia katemwa wakashangilia sana. Ndio maana aliporudi karudi na usongo nao. Alikuwa na habari zote, na utaona alivyokuwa amekasirika kwenye hiyo clip, kwa kuwa kuna kebehi zilifanyika alipoondolewa na Magufuli hawa jamaa wakiona wame-win!
Magufuli mambo yake tangu akiwa waziri wa ujenzi yalikuwa mazito. Si vyema kufukua makaburi.Mkuu, labda tu nikwambie Mbarawa alijua juu ya huu ufisadi. Alishaanza kuufuatilia halafu akatemwa na Magufuli. Hawa jamaa waliposikia katemwa wakashangilia sana. Ndio maana aliporudi karudi na usongo nao. Alikuwa na habari zote, na utaona alivyokuwa amekasirika kwenye hiyo clip, kwa kuwa kuna kebehi zilifanyika alipoondolewa na Magufuli hawa jamaa wakiona wame-win!
Kilichonishangaza, ni kwa nini Dr. Tulia hakuingilia na aliamua kukaa kimya na yeye ni mkazi wa Tukuyu ufisadi huu uliathiri ndugu na jamaa zake kule? Ina maana Magufuli alihusika ndio maana akamuondoa Mbarawa alipoanza kufuatilia?
Waache wafaidi hizo hela watoto na mama sasa, walivumilia makubwa kwa muda mrefu.Magufuli mambo yake tangu akiwa waziri wa ujenzi yalikuwa mazito. Si vyema kufukua makaburi.
Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app