Mbeya: Mpaluka Nyagali Mdude akamatwa na Heroine, apandishwa kizimbani akikabiliwa na mashtaka ya Uhujumu Uchumi

Mbeya: Mpaluka Nyagali Mdude akamatwa na Heroine, apandishwa kizimbani akikabiliwa na mashtaka ya Uhujumu Uchumi

Hii kesi inaonekana kabisa ya kutengeneza kabisa ila ni hatari sana kwa Nchi inapata laaana za ajabu kwa ajili ya matukio ya watu wachache ingawaje dogo ilitakiwa aachane na mambo hayo kipindi hiki...baadae mnataka watu waiombee Nchi bila kubadilika hizi tabia zenu mnaangaamiza Taifa kwa vizazi vijavyo
Kabisa ukimsikiliza kamanda wa police wa mkoa wa mbeya anamaanisha mdude ni teja na kwamba matumizi ya heroin yanaweza haribu akili za mtu!!kuwa mdude hana akili timamu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sema kashika remote, huku tunatazama vikatumi anavyotuwekea tuvicheki
[emoji16]
tapatalk_1589379651791.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
23gm mahakamani anawashinda hicho ni kiwango cha matumizi mpelekeni rehab [emoji111] [emoji111] [emoji111]
Kumbe uyo mtoto anakula unga pia,yani anakula unga na kuza bidhaha iyo haramu?

CCM DAMUDAMU!!!,CHAMA CHA MAMA &BABA
 
Hapo ndo utaona ndugu wa kweli, sio hawa 'chakubanga' wa 'komaa kamanda usiogope'!!! Leo hii watakoumia ni wazazi wake. Mashabiki hoya hoya hawataonekana... Si mbowe, si lema .. mdude atanyea debe peke yake.

Vijana tuangalie familia zetu, mara nyingi maskini ndo tunatolewa sadaka, si kwamba hatuoni ubaya uliopo duniani la hasha! Tunaona ila tunapambania maisha yetu... Yuko wap saa nane? Yupo wap mawazo? Lakini mtoto wa Mbowe yupo Amerika hana hata habari. Tujitafakari

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kua mpinzani wa uongozi sio dhambi , kutokubaliana na hoja ya mwenzako si dhambi as long huvunji sheria ya nchi, lakini Polisi tunapifikia hatua ya kua chombo cha kisiasa na kukandamiza wote wanaoenda kinyume na chama tawala huo ni udikteta, Polisi na Mahakama vya Tanzania inapoteza Imani sasa kwa wananchi, kukamata mtu na kumwekea kidhibiti cha mtu mwingine ili tu ashtakiwe na kufungwa hiyo ni digrii ya juu zaidi ya roho mbaya duniani na mbinguni wewe hufai kuishi. Polisi tendeni haki , Mahakama toeni hukumu za haki. Binadamu na mengine haya yatapita tu na msisahau kua nyie wote tunaishi mitaani wengine ndugu zetu kabisa !!
 
Ni ufala kabisa. Unajiingiza kichwa kichwa wakati wenzako wana jeshi. Faida gani sasa na hii kesi imekaa vibaya. Hapa kutoka ni baada ya miaka.
Kila mtu angekuwa na mawazo kama yako dunia isingekuwa na mabadiliko yoyote. Kwenye kupigania haki ni lazima kuwe na sacrifice na wale wa mwanzoni wengi huuawa au kuumizwa na kufungwa kwa kesi za kubambikiwa. Hakuna sehemu mabadiliko yamekuja bila baadhi ya watu kuumia. Njia nzuri ni kwa waliobaki wenye kukerwa na ukandamizaji huu kupaza sauti na kusaidia kwa hali na mali. Leo umemuita fala lakini kumbuka utawala wa aina hii huwa na kawaida ya kunogewa na ukatili inaofanya. Pamoja na woga wako si ajabu kesho wewe au ndugu yako akajikuta ameathirika na huu ukatili bila hata kutegemea. Hata marehemu Akwilina alikuwa ''fala''?
First they came for the Communists And I did not speak out Because I was not a Communist
Then they came for the Socialists And I did not speak out
Because I was not a Socialist Then they came for the trade unionists
And I did not speak out Because I was not a trade unionist
Then they came for the Jews And I did not speak out
Because I was not a Jew Then they came for me
And there was no one left To speak out for me
 
Back
Top Bottom