Mbeya: Msanii wa Nyimbo za Injili, Sifa Bujune ashikiliwa kwa tuhuma za kuimba wimbo wenye maudhui ya uchochezi

Mbarikiwa Mwakipesile ana kipaji kizuri sana cha kuimba. Tenzi zile alivyoziimba ni wazi zinadhihirisha kipaji chake lakini nadhani kichwani hayuko sawa. Dishi limeyumba kidogo na anahitaji ushauri wa kidaktari japo nasikia pia huwa hashauriki. Yaani angejikita kwenye Neno tu na kumtukuza Mungu aisee angefika mbali sana.
 
......ni mgonjwa...alikuwa anatumia vidonge siku za nyuma....Dr.D.......Z.....anasema alimbadilishia na kumweka katika sindano moja kila mwezi....alikataa kuchomea hospitali na kutaka awe anachomwa nyumbani kwake......Dr.D.......anasema hajui kama ushauri wake ulitekelezwa.....

Ahurumiwe mchungaji wetu Mwakipesile [emoji120]
 
Bora Mwendazake alishajisemea hadharani kuwa "You are not free to that extent"

Huyu hasemi hivyo ila watu wanabinywa korodani kimya kimya

Siku akija kusema hayo basi tutegemee maiti za kwenye viroba
 
Pole yake. Kuna video moja anamshambulia mchungaji mwenzake kwa matusi mazito tena akiwa madhabahuni huku anajigaragaza chini povu jeupe likimtoka mdomoni. Ukiiangalia utajua kuwa hayuko sawa. Si ajabu alishaacha kutumia dawa na kujikita katika maombi zaidi. Watu wake wa karibu na wamsaidie kungalipo na muda bado 🙏🏿
 
Bora Mwendazake alishajisemea hadharani kuwa "You are not free to that extent"

Huyu hasemi hivyo ila watu wanabinywa korodani kimya kimya

Siku akija kusema hayo basi tutegemee maiti za kwenye viroba
Nadhani hata yeye hapa anasema "You are not free to that extent". Alikuwa makamu kule na sijui kwa nini huwa wanamtenga na mabaya yaliyofanyika kule.

 
Hakika.....

Inasikitisha....

Mch.ana matatizo makubwa na wengi wamzungukao ni kama vile nao "wagonjwa" ilihali ni wazima ila BWANA alinena "watu wangu huangamia kwa kukosa maarifa....".

Maarifa maarifa maarifa [emoji120]

BWANA amsaidie aaamin[emoji120]
 
Kumbe wote wanafanana

Mtoto wa Mjusi wote Mijusi 🙌
Demokrasia sisi bado. Ni dhana tu tuliyopandikiziwa na hawa mabosi wetu kwa sababu wanazozijua wao wenyewe. Na mimi naamini ni mtego mwingine wa kutufanya tusiendelee.

Wenyewe huko wengi wao waliendelea wakati wana tawala za kifalme na kidikteta; na baadhi yao walishapigana wenyewe kwa wenyewe mpaka kuheshimiana. Siamini kama wangeanza na hii demokrasia yao wangefika hapo walipo.

Isitoshe kwa sasa demokrasia kule kwao ni sehemu ya mila na utamaduni wao. Na inaanzia majumbani huko. Ndiyo maana kitoto kidogo cha kizungu kinaweza kumkoromea mshua wake home eti kisa kina demokrasia na kinajua haki zake na mshua hawezi kukifanya cho chote. Sisi bado hatujafika huko. Nyumba nyingi bado kuna udikteta wa mshua na wakati mwingine hata mama. Na mila zetu nyingi zinatuasa kuheshimu na kutotukana watu waliotuzidi umri. Ndiyo maana kuna mpishano na mkanganyiko kuhusu dhana nzima ya demokrasia. Kuna wanaoiga uzungu ndani ya demokrasia huku wakiamini kuwa demokrasia haipaswi kuwekewa mipaka. Hawa ndiyo hawaoni shida hata kuporomosha matusi kwa jina la demokrasia. Huku nako utasikia kutukana watu wakubwa si mila na utamaduni wetu na demokrasia yetu inabidi iendane na mila na utamaduni wetu. Mkanganyiko!

Afrika inahitaji "madikteta" dizaini ya akina Kagame na Magufuli. Tuwape miaka 10 - 20 tu. Afrika ingebadilika kabisa. Na baada ya hapo turudi sasa kwenye hizi ngonjera za demokrasia na kuchekeana chekeana na kutukanana huku hakuna la maana linaloendelea.
 
Trash
Hii ndio hoja yangu japo vijana wanatoa povu hapa eti shujaa wa kizazi chao ni yule anayepinga serikali hadharani tena akiitukana. Mbarikiwa hashauri wala hakemei, ila anatukana na ni kweli ana shida ya akili.

Maneno na matendo yake ya sasa ni ya mtu mwenye matatizo ya akili. Mungu amsaidie.
 
Hashauriki wala haambiliki. Nimeona video nyingi akifanya hivyo. Utumishi wa Mungu umejengwa katika unyenyekevu. Sasa hata anavoongea na kutenda unaona kuna shida kichwani mwake.
 
Haya std7 hongera kwa kumaliza shule juzi. Sekondari unaenda soma wapi?
Fake pastor Kinengunengu baada kumaliza la saba nilienda chuo cha biblia kusoma theolojia
Kwa sasa nipo mtaani nafanya kazi na kuhubiri injili siuzi mafuta, maji wala vitambaa vya upako.
 
Brother watu wamechoka sana.. Kuna lugha ya kuongea na serikali kwasasa maana lugha laini hazina matunda wameshupaza shingo hawaambiliki, hawashauriki..
Hawa wanaopaza sauti zao kwa ukali ni kiwakilishi cha wengi sana waliochoshwa mno na mambo ya hii serikali
Wanaweza kuwajeruhi kuwaumiza na hata kuwafunga lakini wataibuka wengine wengi watakaoongea kwa sauti kali zaidi.. Watu wamechoka sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Toka enzi na enzi hayo yapo na si mapya.....hayajazibadilisha SERIKALI.....

#Never give wisdom to unworthy as it unjust to the knowledgeable [emoji120]
 
kwahiyo siku hizi hamkemei dhambi hadharani mnaenda kuwaeleza na kuwakemea chumbani??? huu kama si us£nge ni nini?? toka mmempa yule kambale wa chato tuzo niliwadharau mpaka leo, hamna kanisa hapo kuna wala sadaka tuu humo. TAG ni useless church
Mkuu naona umegusa nilikopita.
TAG lilikuwa ni kanisa lenye misingi bora kabisa, lskini taratibu Barnabas Mtokambali analipeleka mbali na Mungu.

Rais anapewa TUZO ya corona?
Badala ya kumshukuru Mungu!!!

Hili jambo liliniumiza sana.

Isitoshe akaongea maneno ya hovyo mnoo.
 
huyo binti akae ndani miezi ya kutosha hadi akili zimrudi. kale kakikundi kao kote kanatakiwa kukaa ndani kama njia ya kuwakomboa kutoka kwenye kikundi haramu kinachojiita cha dini.
 
Kwanini pilato alinawa mikono kabla ya Kutoa HUKUMU?

Unajua maana ya Wayahudi kusema Damu yake iwe juu yetu na juu ya watoto wetu?

Usijitie ujuaji Kwa usoyajua.
 
Kwanini pilato alinawa mikono kabla ya Kutoa HUKUMU?

Unajua maana ya Wayahudi kusema Damu yake iwe juu yetu na juu ya watoto wetu?

Usijitie ujuaji Kwa usoyajua.
Wewe maamuma tu, wapi wayahudi walipata mamlaka ya kumuua wakati walikuwa chini ya dola la Rumi? Je wangekuwa na uweza na mamlaka ya kumuua kwanini wasingemuua vichochoroni hadi kwenda kumshatki kwa pilato? nani aliidhinisha kuuawa kwake? Je ni nani waliotekeleza mauaji yake? Kuna sehemu wayahudi walimsulubisha zaidi ya kushtaki wakisubiri pilato atoe hukumu? Je kusema hatia ya damu iwe juu yetu ndio utekelezaji wa mauaji? Nakataa wayahudi hawajamuua ila aliuliwa na dola ya Kirumi ila wayahudi walichochea uuaji wake hizo zingije ni blah blah zako tu mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…