Mbeya: Msanii wa Nyimbo za Injili, Sifa Bujune ashikiliwa kwa tuhuma za kuimba wimbo wenye maudhui ya uchochezi

Wacha blah blah, hakuna unabii wa namna hiyo. Hizo mbwembwe tu. Kuna nabii gani kwenye Biblia alitabiri kama unayosema wewe. Acha uongo na upotoshaji dogo. Sijui kwanini kila kitu sasa mnakiweka kwenye mlengo wa kisiasa. Yaani mtu akikataa kuamini unachoamini na kutaka unalazimisha siasa.
 
Rabbon Ione hii
 
Sio wote kaka🤭nI baadhi tu
Wengine wako vzr
 
Uchochezi haukubaliki
 
Napenda akiimba tenzi!
Hivi ni kweli Hana kipawa Cha kuhubiri?
Au anacho ila Kuna Mahali adui kamuwahi tu katoka kwenye reli?

Niliona mikutano yake kadhaa Iko poa!
Lkn pia mbarikiwa sio masikini bwana Hana njaa ya kusema ategemee sadaka 😅
 
Wanataka Dogo apate viewers wengi, weka link faster
 
Mimi ni kiongozi wa Kanisa na ni miongoni mwa wajumbe CPCT Taifa, kama wapentecoste tulishauri na kutoa maoni yetu kwa Mamlaka kuhusu Bandari kwani nasi tunaaminiwa na watu hatuwezi mshutumu mfalme mbele za watu.
Wewe na wenzako ni ama machawa au mmepewa bahasha. Mfalme kama umempa ushauri wako halafu akaupuuza inapaswa kumpinga hadharani.

Maaskofu wa katoliki kule Zaire (DRC) walimpinga rais Joseph Kabila waziwazi na hadharani tena kwa maandamano alipotaka kuwania muhula wa tatu kinyume na matakwa ya katiba ya nchi hiyo.

Ninyi viongozi wa dini za matumbo yenu ambao miujiza yenu ya uponyaji inaamshwa na fedha na mkipewa fedha na watawala mnasema ni chaguo la Mungu hamfai hata kidogo.

Kiuhalisia wewe na wenzako siyo viongozi wa dini bali matapeli manaotumia dini kufanya utapeli wenu.
 
Napenda akiimba tenzi!
Hivi ni kweli Hana kipawa Cha kuhubiri?
Au anacho ila Kuna Mahali adui kamuwahi tu katoka kwenye relief?
Kiburi na kutokushaurika ndio chanzo cha anguko. Binafsi ni mpenzi wake na nina nyimbo zake nyingi sana za tenzi. Wengi wale walioanza naye wameachwa naye baada ya kuona alivyo. Sasa kuokoteza vijana anawapelekesha atakavyo. Kuna kijana mmoja anaitwa Ulimwengu Milenga alikuwa naye kikosi akaamua kujitoa kikosi, akaanza mtukana na kumlaani. Anguko lake lilishaonelana toka alipoanza tokana watu kwenye kipindi cha korona. Kama kanisa tulidhatuma watu wamshauri na kumrejesha kwa upendo tulichoambulia ni matusi. Fuatilia watoro wake akina Onesmo Mwakajila, Isaya n.k. fuatilia namna pia walivyomshambulia Kuhani Lawi alipomshauri tena hadi kutengeneza voice note fake ya kumchafua.
 
Wacha weeeeeee.
 
Sio kila mtu ni muoga wa aina yako. We weka maoni yako kwa kificho, acha wenye uthubutu wahoji hadharani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…