Mbeya: Msanii wa Nyimbo za Injili, Sifa Bujune ashikiliwa kwa tuhuma za kuimba wimbo wenye maudhui ya uchochezi

Mbeya: Msanii wa Nyimbo za Injili, Sifa Bujune ashikiliwa kwa tuhuma za kuimba wimbo wenye maudhui ya uchochezi

Alaaa!!

Unabii unasema hivi, huu ni muda wa .....kuingia na kitabu Kanisani, baada ya hapo, aliyeingia na kitabu Kanisani, anarudi tena mara ya pili kukabidhi Kwa Kanisa.

Wenye macho wameona Yehu akijenga madhabahu ya Mungu mkuu na kuangusha miungu ya mabaali.

Na HAKI itasimama juu ya nchi Ili mtoto Amani azaliwe.

Endelea na mapambio kuwambia wamevaa wakati nanii ziko nje!!!
Wacha blah blah, hakuna unabii wa namna hiyo. Hizo mbwembwe tu. Kuna nabii gani kwenye Biblia alitabiri kama unayosema wewe. Acha uongo na upotoshaji dogo. Sijui kwanini kila kitu sasa mnakiweka kwenye mlengo wa kisiasa. Yaani mtu akikataa kuamini unachoamini na kutaka unalazimisha siasa.
 
usimshambulie huyu mtu bure. hata wewe pesa huna. hata mbarikiwa pesa hana, labda anazowadanganya ninyi mnampa halafu hawahubirii neno anaishia kutukana watu.

kitu kingine, kama upo karibu na mbarikiwa, mwambie kwamba yeye hajaitiwa kuhubiri, ameitiwa kuimba na anajua sana kuimba, kama angeimba yule angeshakuwa bilionea Tanzania hii na nyimbo zake zilikuwa zinasaidia sana watu kiroho. hiyo ndio talanta Mungu alimpa. mshauri hivyo tu, aache kuhubiri hawezi na Mungu hayupo naye kwenye fungu la kuhubiri alilolichagua. hata leo akiamua kuachana na hicho kikundi cha wahuni, akaanza kuimba nyimbo, atapata pesa nyingi sana hata za kusapoti injili na kusaidia masikini na wahitaji wengine, badala ya kushinda kutwa anapambana na serikali badala ya kupambana na shetani.
Rabbon Ione hii
 
Wasengenyaji mnoo, halafu waoga.
Hawa ni wachungaji wangu nawajua nje ndani.

Elimu ya kuunga unga haiwapi ujasiri kukosoa, wengi ni weupe sana kichwani.

Pili wamejaa umaskini, wanakimbizana na sadaka na mafungu ya kumi tu.

Kama ana bisha aseme kanisa lake hapa
Sio wote kaka🤭nI baadhi tu
Wengine wako vzr
 
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia mwimbaji wa nyimbo za injili SIFA BONIVENTURE BUJUNE [25] Mkazi wa Isyesye Jijini Mbeya kwa tuhuma za kuimba wimbo wenye maudhui ya uchochezi na kuurusha kwenye mitandao ya kijamii.

Kamanda wa Polisi Mbeya, Benjami Kuzaga amesema Mtuhumiwa alikamatwa Septemba 13, 2023 huko Isyesye Jijini Mbeya baada ya kuimba wimbo wenye maudhui ya uchochezi dhidi ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuusambaza kupitia mitandao ya kijamii pamoja na mtandao wa kurusha maudhui wa Youtube.

Mtuhumiwa anaendelea kuhojiwa kwa hatua zaidi za kisheria.
Uchochezi haukubaliki
 
usimshambulie huyu mtu bure. hata wewe pesa huna. hata mbarikiwa pesa hana, labda anazowadanganya ninyi mnampa halafu hawahubirii neno anaishia kutukana watu.

kitu kingine, kama upo karibu na mbarikiwa, mwambie kwamba yeye hajaitiwa kuhubiri, ameitiwa kuimba na anajua sana kuimba, kama angeimba yule angeshakuwa bilionea Tanzania hii na nyimbo zake zilikuwa zinasaidia sana watu kiroho. hiyo ndio talanta Mungu alimpa. mshauri hivyo tu, aache kuhubiri hawezi na Mungu hayupo naye kwenye fungu la kuhubiri alilolichagua. hata leo akiamua kuachana na hicho kikundi cha wahuni, akaanza kuimba nyimbo, atapata pesa nyingi sana hata za kusapoti injili na kusaidia masikini na wahitaji wengine, badala ya kushinda kutwa anapambana na serikali badala ya kupambana na shetani.
Napenda akiimba tenzi!
Hivi ni kweli Hana kipawa Cha kuhubiri?
Au anacho ila Kuna Mahali adui kamuwahi tu katoka kwenye reli?

Niliona mikutano yake kadhaa Iko poa!
Lkn pia mbarikiwa sio masikini bwana Hana njaa ya kusema ategemee sadaka 😅
 
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia mwimbaji wa nyimbo za injili SIFA BONIVENTURE BUJUNE [25] Mkazi wa Isyesye Jijini Mbeya kwa tuhuma za kuimba wimbo wenye maudhui ya uchochezi na kuurusha kwenye mitandao ya kijamii.

Kamanda wa Polisi Mbeya, Benjami Kuzaga amesema Mtuhumiwa alikamatwa Septemba 13, 2023 huko Isyesye Jijini Mbeya baada ya kuimba wimbo wenye maudhui ya uchochezi dhidi ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuusambaza kupitia mitandao ya kijamii pamoja na mtandao wa kurusha maudhui wa Youtube.

Mtuhumiwa anaendelea kuhojiwa kwa hatua zaidi za kisheria.
Wanataka Dogo apate viewers wengi, weka link faster
 
Mimi ni kiongozi wa Kanisa na ni miongoni mwa wajumbe CPCT Taifa, kama wapentecoste tulishauri na kutoa maoni yetu kwa Mamlaka kuhusu Bandari kwani nasi tunaaminiwa na watu hatuwezi mshutumu mfalme mbele za watu.
Wewe na wenzako ni ama machawa au mmepewa bahasha. Mfalme kama umempa ushauri wako halafu akaupuuza inapaswa kumpinga hadharani.

Maaskofu wa katoliki kule Zaire (DRC) walimpinga rais Joseph Kabila waziwazi na hadharani tena kwa maandamano alipotaka kuwania muhula wa tatu kinyume na matakwa ya katiba ya nchi hiyo.

Ninyi viongozi wa dini za matumbo yenu ambao miujiza yenu ya uponyaji inaamshwa na fedha na mkipewa fedha na watawala mnasema ni chaguo la Mungu hamfai hata kidogo.

Kiuhalisia wewe na wenzako siyo viongozi wa dini bali matapeli manaotumia dini kufanya utapeli wenu.
 
Napenda akiimba tenzi!
Hivi ni kweli Hana kipawa Cha kuhubiri?
Au anacho ila Kuna Mahali adui kamuwahi tu katoka kwenye relief?
Kiburi na kutokushaurika ndio chanzo cha anguko. Binafsi ni mpenzi wake na nina nyimbo zake nyingi sana za tenzi. Wengi wale walioanza naye wameachwa naye baada ya kuona alivyo. Sasa kuokoteza vijana anawapelekesha atakavyo. Kuna kijana mmoja anaitwa Ulimwengu Milenga alikuwa naye kikosi akaamua kujitoa kikosi, akaanza mtukana na kumlaani. Anguko lake lilishaonelana toka alipoanza tokana watu kwenye kipindi cha korona. Kama kanisa tulidhatuma watu wamshauri na kumrejesha kwa upendo tulichoambulia ni matusi. Fuatilia watoro wake akina Onesmo Mwakajila, Isaya n.k. fuatilia namna pia walivyomshambulia Kuhani Lawi alipomshauri tena hadi kutengeneza voice note fake ya kumchafua.
 
Wewe na wenzako ni ama machawa au mmepewa bahasha. Mfalme kama umempa ushauri wako halafu akaupuuza inapaswa kumpinga hadharani.

Maaskofu wa katoliki kule Zaire (DRC) walimpinga rais Joseph Kabila waziwazi na hadharani tena kwa maandamano alipotaka kuwania muhula wa tatu kinyume na matakwa ya katiba ya nchi hiyo.

Ninyi viongozi wa dini za matumbo yenu ambao miujiza yenu ya uponyaji inaamshwa na fedha na mkipewa fedha na watawala mnasema ni chaguo la Mungu hamfai hata kidogo.

Kiuhalisia wewe na wenzako siyo viongozi wa dini bali matapeli manaotumia dini kufanya utapeli wenu.
Wacha weeeeeee.
 
Hao ni vijana wa Mbarikiwa Mwakipesile na huwa tunamshauri sana aache kushindana na dola na kama anainba kuisema serikali aimbe na kusema yeye kama yeye na asihusishe kanisa na Ukristo kwenye mambo yake. Yule ana shida kidogo kwa. Suala lake binafsi liniiuma sana kwani nilikuwa nampenda na kupenda zile tenzi wanazoimba.

Sasa amejiingiza kushambulia serikali bila sababu akisema wamemuulia mwanaye tena Mkurugenzi wa usalama wa Taifa ndio kafanya hivyo. Jamaa hashauriki, vijana wake hao waliokamatwa hawashauriki wao wanatokana na kujiona wajuaji kama genta alivyo. Kiburi, kutojinyenyekesha, ujuaji mara nyingi huenda kwenye anguko.

Sasa kumezuka wimbi kubwa la watumishi wanaosimama na kuoneshana umwamba na serikali. Hakuna duniani mtumishi wa Mungu aliwahi ishinde dola nasi wajibu wetu ni kushauri na kuiombea mamlaka na siyo kushindana nayo.

Mimi ni kiongozi wa Kanisa na ni miongoni mwa wajumbe CPCT Taifa, kama wapentecoste tulishauri na kutoa maoni yetu kwa Mamlaka kuhusu Bandari kwani nasi tunaaminiwa na watu hatuwezi mshutumu mfalme mbele za watu.

Tulikumbushia kwa Spika wakati wa mkutano wetu mkuu pale CBC Miuji Dodoma kuhusu maoni yetu na msimamo wetu ki sio kushindana wala kupinga hadharani.
Sio kila mtu ni muoga wa aina yako. We weka maoni yako kwa kificho, acha wenye uthubutu wahoji hadharani.
 
Back
Top Bottom