Hao ni vijana wa Mbarikiwa Mwakipesile na huwa tunamshauri sana aache kushindana na dola na kama anainba kuisema serikali aimbe na kusema yeye kama yeye na asihusishe kanisa na Ukristo kwenye mambo yake. Yule ana shida kidogo kwa. Suala lake binafsi liniiuma sana kwani nilikuwa nampenda na kupenda zile tenzi wanazoimba.
Sasa amejiingiza kushambulia serikali bila sababu akisema wamemuulia mwanaye tena Mkurugenzi wa usalama wa Taifa ndio kafanya hivyo. Jamaa hashauriki, vijana wake hao waliokamatwa hawashauriki wao wanatokana na kujiona wajuaji kama genta alivyo. Kiburi, kutojinyenyekesha, ujuaji mara nyingi huenda kwenye anguko.
Sasa kumezuka wimbi kubwa la watumishi wanaosimama na kuoneshana umwamba na serikali. Hakuna duniani mtumishi wa Mungu aliwahi ishinde dola nasi wajibu wetu ni kushauri na kuiombea mamlaka na siyo kushindana nayo.
Mimi ni kiongozi wa Kanisa na ni miongoni mwa wajumbe CPCT Taifa, kama wapentecoste tulishauri na kutoa maoni yetu kwa Mamlaka kuhusu Bandari kwani nasi tunaaminiwa na watu hatuwezi mshutumu mfalme mbele za watu.
Tulikumbushia kwa Spika wakati wa mkutano wetu mkuu pale CBC Miuji Dodoma kuhusu maoni yetu na msimamo wetu ki sio kushindana wala kupinga hadharani.