Mbeya: Mwekezaji ajinyonga baada ya ng'ombe wake 50 kukamatwa na Maliasili, RC Chalamila acharuka asihusishwe

Mbeya: Mwekezaji ajinyonga baada ya ng'ombe wake 50 kukamatwa na Maliasili, RC Chalamila acharuka asihusishwe

Sasa kama RC kakosea nini? Ulisikia kakamata ng'ombe kapeleka kwake au maeneo walioyatenga? Tena kawa straight kwamba sheria uchukue mkondo wake

Nilimsikia anasema kama kawaida ya wafugaji walianza kupiga simu wahonge pesa
Ni mwizi tu kama wengine
 
Nchi zilizona mawazo ya kumuendeleza mwananchi humpatia msaada wa kila aina mwananchi wake ili ajikimu kwa nahitaji mepesi mepesi.
Sasa hapa Tz viongozi wengi wanawaambia wananchi fanyeni kazi kwa nguvu zenu,wengine wanawahimiza wananchi wajiajiri wenyewe.

Sasa kuna vilaza waliodandia basi la Magufuli Express hawana wanalolijua wao ni amri kwa kwenda mbele,badala ya kujenga wanavuruga.

Serikali inadai mapaka kodi ya ng'ombe ,huku ndio kujitawala ? Mbona tunarudi kulekule tunakotaka kuondoka kwenye utumwa.

Kuna haja hii kodi iwe na kikomo na mipaka ,kuna mmoja kule mikoa ya kusini kama sikosei ametaka kila mtu awe na shamba kama anapanda mihogo au magugu maji lakini awe na shamba,huyu tunaweza kumpa hongera kwani wananchi wakiitikia wito wake basi amewasaidia ila hawa wenye husuda si viongozi ni mizigo ni watu wenye husuda sana mafisadi amezuia ng'ombe apewe chochote ili aafu ndio awawachie ,sasa yamemkuta achukuwe hao ng'ombe awachunge yeye kama kuchunga ni kazi rahisi kihivyo,

Yaani hapo Mheshimiwa Magufuli raisi wa wanyonge amtake alie wazuia ng'ombe hao awachunge yeye na kuisimamia familia ya kijana aliyepoteza maisha.
 
Chalamila pamoja na genge lako kutoka Tanapa mtavuna mlichopanda
Muwekezaji kwenye hifadhi? Alipata wapi permit ya kufanya ufugaji ndani ya hifadhi? Hii sio mara ya kwanza kufanyika oparesheni huko Ihefu seems watu hawajifunzi
 
Kwa hiyo serikali imeshindwa kabisa kuwaelimisha hawa wafugaji wa kuhama hama kubadili hii aina ya ufugaji?

Miaka nenda sasa jamii ya Wamasai, Wabarbaig, Wasukuma, nk. Wamekuwa wakihama hama hovyo na idadi kubwa ya mifugo wakitafuta maeneo ya malisho, huku wakifanya uharibifu mkubwa wa mazingira!

Ni kwa nini wasitafutiwe maeneo maalum ambayo watatulia na mifugo michache, huku wakiifuga kisasa badala ya kiholela kama ilivyo desturi yao ya vizazi na vizazi!!!

Hofu ya serikali wakifanya km ulivyoshauri nyama itapanda bei maradufu kitu ambacho hawawezi kukubali
 
God save us
Nadhani kuna haja ya kukaa na wawekezaji hao kujua Nini tatizo au changamoto wanayokutana nayo ili kupata suluhisho la kudumu.Siku Chache zilipita nilimwona mh waziri na karibu wake mkuu wa wizara wakijaribu kusikiliza kero za wawekezaji hao ambapo mzee mmoja alitoa taarifa za uongo uliotaka kumsababishia kuswekwa ndani.Kwa namna nilivyofuatilia ziara ile nikagundua kuwa kuna mambo hayaendi sawa pale mbalali hivyo ni lazima intervention ifanyike ili wawekezaji wasifilisike na kusababisha vifo.
 
Chalamila pamoja na genge lako kutoka Tanapa mtavuna mlichopanda
Askari wa tanapa nadhani hawana makosa kwenye hili. Wao wamekata ng'ombe wameingia hifadhini. Na sheria inawataka hivyo. Hawajavunja sheria yoyote.
 
Ila ku deal na wafugaji kazi sana
Hilo ndiyo tatizo la kuwa na ngombe wengi kuwalisha kwako mtihani

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
 
Askari wa tanapa nadhani hawana makosa kwenye hili. Wao wamekata ng'ombe wameingia hifadhini. Na sheria inawataka hivyo. Hawajavunja sheria yoyote.
Utakamataje ng'ombe wote badala ya mtu,
Ingekuwa vyema akamatwe mmiliki na uchukuliwe ushahidi wa picha na gps kwamba ng'ombe walikuwa eneo la hifadhi
Kwenye hili na mengine yanayohusiana na hili inabidi utashi wa binadamu uongezeke zaidi
 
Utakamataje ng'ombe wote badala ya mtu,
Ingekuwa vyema akamatwe mmiliki na uchukuliwe ushahidi wa picha na gps kwamba ng'ombe walikuwa eneo la hifadhi
Kwenye hili na mengine yanayohusiana na hili inabidi utashi wa binadamu uongezeke zaidi
Unakamataje mtu uache ng'ombe ambao ndio kidhibiti? Halafu fine atalipa nani?
Ni sawasawa ukamate jangili halaf aache nyama aliyopiga huko porini. Mtaenda kumshtaki na nn?

Askari wa tanapa huw wanatembea na gps ku mark maeneo ambapo pamefanyika uhalifu.
Picha huwa zinachukuliwa..
Mpaka maelezo ya mtuhumiwa huchukuliwa.

Huwezi mark mifugo kwa gps ni ngumu kuja kwafuatilia. Wale ndio ushahidi.. ukiwaachia ni rais sana mtuhumiwa kuwakataa.. kudanganya idadi ya mifugo..

Sheria inasema mwenye mali atalipa fine. Asipolipa fine ndani ya muda uliowekwa. wanapigwa mnada.. sheria ziko wazi and its simple like that.

Or kama wanaona wanaonewa..wasiingize mifugo ndani ya mapori.
 
TATIZO LINAKUJA KWA WAFUGAJI WENGI WA TANZANIA UNAKUTA MTU ANA NGOMBE WENGI KUWALISHAA NI MTIHANI,SASA KWANINI ASIWAINGIZE KWENYE MAENEO mf-MASHAMBA YA WATU KUWALISHA NGOMBE WAKE,NA HIYO MWISHOWE INALETA VURUGU MPK KUSABABISHA MAUAJI KATI YA WAKULIMA NA WAFUGAJI

ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
 
Tuna tatizo kubwa sana kwenye mfumo....kuanzia ngazi za chini mpaka za juu
 
Back
Top Bottom