Mbeya: Mwimbaji wa Wimbo wa "Mnatuona Nyani" afikishwa Mahakamani, tuhuma za Uchochezi zayeyuka yawa kesi ya kusambaza Uongo

Imebaki muda kidogo sana kuanzia sasa serikali itajutia uasi inaoutengeneza kwa mikono yake yenyewe maana hiki kinachotokea Mbeya kitaenea na kutekelezwa kwa nguvu maeneo mengine ya nchi ili viongozi waelewe kwamba wanawanyanyasa wananchii na kuwanyima haki zao. Mwimbaji wa nyimbo za injili katika wimbo waliouimba maudhui yake yana madhara gani na kwa nani?

Mkuu wa mkoa, mkuu wa wilaya, RPC, RCO, OC CID na RSO wa Mbeya waepuke kutumia vibaya madaraka ya kupewa mnapanda chuki zisizo na mithili mioyoni mwa Watanzania. Kuna muda watasema ni bora kifo kuliko kukandamizwa na binadamu tena anayetumia dhuluma hizo kwa kodi zao.

Ni aibu sana kufanya kazi pasipo kuzingatia misingi ya sheria; kwanini waharifu wanaohatarisha uhai na maendeleo ya nchi hawakamatwi kama waficha mafuta, wahujumu nishati ya umeme, wapandisha bei za vyakula badala yake mnapeleka hasira zenu za kujipendekeza kwa watawala dhidi ya wananchi wasio na hatia waotoa maoni yao kutokana na changamoto wanazo sababishiwa na wa baadhi ya viongozi??

Enough is enough and a will shall be granted soon.
 
U Unapendekeza ??
Sawa mzee
 
Div IV ya point 32 hiyo
 
Tunakuja Kanda ya Nyasa wiki ijayo
Anziaeni Ruvuma, shukeni kuja Mtwara, njooni Lindi, na mwambao wa Pwani ya Kilwa,, Mafia, Rufiji-Utete, Kibiti Na Mkuranga mtanishukuru.

Changamoto za kusini
1. Mkataba wa gesi kwa waliouziwa ni kwamba ni kuhakikisha Mtwara na Lindi umeme haukatiki, lakini kinyume chake tangu awamu hii imeanza kuna malalamiko mengi ya kukatika umeme na majibu ya shombo
2. Kuna madalali wa mashamba na mazao ya mikorosho kutoka kwa wanasiasa wenye mlengo kandamizi na ufisadi, wananchi wakipunjwa na kucheleweshewa malipo baada ya kukabidhi mazao yao na kupewa stakabadhi ghalani
3. Dangote kapewa eneo kubwa sana la uwekezaji wa kiwanda cha simenti ambapo ukubwa wake unaweza kufikia baadhi ya maeneo ya wilaya nzima ambapo anachimba mawe na kuwauzia Twiga simenti. Bei ya sementi yao iko juu kinyume na ahadi ya kushusha soko kwa kuzalisha kwa wingi
4. Miundo mbinu mibovu na miradi hewa mingi kama pembejeo ni mateso matupu mapori mengi yanahodhiwa na viongozi wa kisiasa au wafanyabiashara huku wananchi wakihamishwa kwa madai maeneo yalipimwa zamani isiyojulikana wakati wameishi hapo vizazi kadhaa
Nk
 
Hata kama polisi ni jumuiya ya CCM muda mwingine pamoja na akili za kuambiwa wawe wanachanganya na akili zao, wakiegemea upande mmoja tu wa kutaka kumfurahisha Bwana wao watakuwa wababaishaji Siku zote.
 
Mkuu Hakuna kijiji kitakachobakizwa , Isipokuwa ratiba iliyotolewa na Kamati Kuu inaelekeza kituo kinachofuata kwa oparesheni 255 ni Kanda ya Nyasa , huko ulikotaja kwa sehemu kubwa ni Kanda ya kusini
 
Mkuu Hakuna kijiji kitakachobakizwa , Isipokuwa ratiba iliyotolewa na Kamati Kuu inaelekeza kituo kinachofuata kwa oparesheni 255 ni Kanda ya Nyasa , huko ulikotaja kwa sehemu kubwa ni Kanda ya kusini
Kwa hiyo kanda ya Nyasa ni Njombe na Ruvuma?

Pamoja na hayo pangeni uwanda niliouelekeza mkibomoa ngome hizo basi hiyo kusini yote itajirudi kufuata mkondo mpya
 
Inaelekea kufutwa kabisa. Vyombo vya dola vifuate sheria siyo kufanya kazi chini ya shindikizo maana siku ya mwisho lawama zitakuwa siyo kwa aliyetoa shindikizo bali ninyi watenda kazi vituoni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…