Ni muhimu sana kwani kila nikiangalia naona Mkoa wa Mbeya na wenyeji wa Mkoa huo pamoja na Kanda ya Ziwa wanapaswa kuwa kama Zanzibar ndani ya Tanzania, naamini kabisa Mbeya kama vile Kanda ya Ziwa watapata maendeleo makubwa sana kama wakiachwa wajitawale wenyewe kama vile Zanzibar.
Watu wa Mbeya na Kanda ya Ziwa wana potential kubwa sana ambayo haitumiki na Mikoa yao hasa Mbeya ni kama imesahaulika, ni lini Raisi wa Tanzania aliwahi kufika Mbeya mara ya mwisho ?
Muandishi kwanza unatakiwa kutofautishs kanda ya ziwa na Mbeya.
Mkoa wa Mwanza pekee ni mkubwa kwa hadhi kuliko Mbeya ila haujaomba 'kujitawala' kama Zenji.
Kanda ya Ziwa ina Mwanza, Geita, Simiyu, Mara, Shinyanga na Kagera (hii ni mikoa 5) unapojenga hoja kufanya mkoa mmoja uwe na hadhi kama mikoa 5, bila shaka inathibitisha namna gani huijui vya kutosha kanda ya Ziwa.
Ikitokea Mbeya imetembelewa mara kwa mara na Mkulu, nini kitaongezeka?
Ikitokea Mbeya imejitenga kwa kuwa na hadhi ya Rais wa Mbeya kama Zenji, itapata nini cha kuifanya ikue?
Mkoa unaweza kukua kwa kutegemea ridhaa ya Rais wa nchi au shughuli za wananchi kuzalisha kwa tija na ufanisi wa hali juu ili kukuza uchumi wa eneo?
Pengine ntakubaliana nawe kama RC alieopo sio mzuri kwa lobbying na anategemea mamlaka ya uteuzi ifanye kila kitu, basi Mbeya kama ilivyo mikoa mingine itasubiri sana.
Kuna shida kubwa toka enzi ya Mwl. JKN, ukuu wa mkoa na sekretariet ya mkoa inakuwa na watendaji wasio wazawa na ina faida ya kutokukuza ukanda, na ina hasara kwa kuwa na watu ambao wanafanya business as usual na wanaweza wasiwe creative na innovative kukuza uchumi wa eneo husika kwa msingi wa kutowajibika kwa wananchi moja kwa moja.
Wengi hujuiona wajubu wao ni kumpendezesha mkulu wa Magogoni/Chamwino.
Kwa kuwa hoja ya Mbeya kupewa hadhi kama ya Zenji ni kama haiwezekani kutokea, fikiria mbadala ya nini kifanyike ili uchumi wa Mbeya ukue, mzunguko wa fedha uwepo kwa watu kufanya biashara na kuwa na fedha za kumudu mahitaji yao.
Purchasing power matters bila kujali mtu yuko Mbeya au penginepo.
Nini kifanyike ili watu wengi wa Mbeya wakuze uchumi wao na hata imvutie Mkulu mara kwa mara awe anatia mguu kuzindua miradi ya uwekezaji Mbeya, hilo kaweza kufanyika haraka pasi kutaka kuipa Mbeya hadhi ya Zenjibar.
Jpili njema.
FAM