Manndasori
JF-Expert Member
- Feb 19, 2021
- 286
- 259
Watu wa kilimanjaro wamejiletea maendeleo bila kuitegemea serikali, nenda kila kona ya nchi hii unawakuta kina mangi wanafanya biashara na wanapush maendeleo ya nyumbani kwao hasa upande wa elimu ndio maana leo hii kilimanjaro ndio mkoa wenye shule nyingiUkutaka kujua wilaya yenye mapato makubwa ushahidi wa kwanza itakuwa na halmashauri zaidi ya moja. kwa hyo kanda yenu nu Kahama, Tarime na Bunda tu. Tena 2 ziko Mara ambao hawana sifa za kishamba km wasukuma. Hata wilaya za mkoa Kilimanjaro bado zina mapato madogo hakuna hata wilaya moja ina halamashauri 2 lakini ukija kwenye sifa za kijinga watakuambia Kilimanjaro tumeendelea sana. Nchi hii sasa hivi kuna makabila mawili kwenye mitandao sijui wamelogwa na nani. Ni sifa za uwongo na za kijinga.
Wakati serikali inaanza kampeni ya kua na shule ya sekondari kila kata wao walikua na zaidi ya shule mbili kila kata na kila mwaka wanaongeza shule kwa nguvu zao hawaitegemei serikali
Hospitali ya mawenzi haikujengwa na serikali ilijengwa na wakulima wa kahawa
Hospitali ya KCMC waliijenga kupitia KKKT
Hawa watu ni kweli hawana raslimali ya maana mkoani kwao ila wana uwezo mkubwa wa kujiongeza, angalia sehemu yoyote yenye fursa wanawahi chapu
Tujifunze kutoka kwao hao jamaa wana tabia za kiisraeli
Mbeya hoyeee sema nako wamejazana balaa hawa kina mangi