Pre GE2025 Mbeya: Naibu Waziri Biteko aingilia Maandamano ya CHADEMA

Pre GE2025 Mbeya: Naibu Waziri Biteko aingilia Maandamano ya CHADEMA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Maandamano huwa na ratiba yake, barabara yake na muda maalumu. Huo msafara w Naibu Waziri Mkuu una ratiba na hiyo ruti?!
Aiseee, mbona mbowe hakuheshimu ratiba ya rais kwenye Manyara kwenye mafuriko.?
 
Nina video nyingi Iła nashindwa ku attach. Moderator Nitumie namba nikutumie WhatsApp
 
Kutumia msafara wa Naibu waziri mkuu ku interfere maandamano siyo Jambo lenye afya na linadhalilisha ofisi ya waziri mkuu, msafara wa Waziri mkuu siyo wa ghafla hivyo ni wazi wakuu wa usalama Barabarani walikuwa na taarifa kabla, walichotakiwa kufanya ni kutafuta njia mbadala au kupishanisha muda wa maandamano na msafara.
 
Huo msafara ungesubiri kwani Chadema ilisha ruhusiwa...Viongozi wajifunze kustaraabika

Tunakuwa kama primitivu
Kila mmoja anawajibika kutimiza haki yake bila ya kuingilia haki za wenzake, Chadema na wafuasi wake wanayo haki ya kuandamana inalindwa kikatibu na wamepewa haki hiyo kwa utaratibu ambao hautaathiri haki za wengine za kutumia barabara na kuendelea na shughuli zao nyengine.
 
Kutumia msafara wa Naibu waziri mkuu ku interfere maandamano siyo Jambo lenye afya na linadhalilisha ofisi ya waziri mkuu, msafara wa Waziri mkuu siyo wa ghafla hivyo ni wazi wakuu wa usalama Barabarani walikuwa na taarifa kabla, walichotakiwa kufanya ni kutafuta njia mbadala au kupishanisha muda wa maandamano na msafara.
Watu ndo tunaokuza mambo, Chadema waandamane kwa amani huku wakiheshimu haki za wengine za kutumia Barabara, na Polisi wanaongoza kuhakikisha kila kundi linatekeleza haki yake na wajibu wake
 
Wakati mwingine wananchi tuwe wakali. Shusha hao wajinga, piga gari kiberiti. Siku zote kunapokuwa na maandamano, magari inabidi yasubiri.
Tutakua taifa la Aina gani? Leo CCM, ACT, Wakristo, Waislamu watake kuandamana kuwasilisha ujumbe wao Barabara zifungwe kwaajili yao? Sio kweli
 
Hapo biteko na watu wake ndio wakorofi, maandamano halali yamepangwa siku nyingi tu alafu na mtu anakuja na msafara wake siku hiyohiyo
 
Hv kwann hao wengine wajiepushe na hayo maeneo wakati mlishasema ni maandamano ya amani, kwahy watu wasiendelee na majukumu yao kisa maandamano yao.?
Swali zuri sana, Yaani sababu wao wanaandamana wanatamani shughuli zote zisimame, kuna muda unaweza kuwaunga mkono watawala kuweka zuio za mambo kama haya
 
Kwann wanachadema wanazomea na kutoruhusu naibu Waziri mkuu kutokupita, c walisema yatakuwa ni maandamano ya amani.?

Naibu Waziri ni mtu mmoja, maandamano ni ya maelfu ya watu. Kwa nini Naibu Waziri asiheshimu wananchi walio wengi? Polisi wana taarifa na details zote za barabara gani watatumia waandamanaji, na muda gani, kwa nini wasimtafutie alternative road kuliko kuwasumbua waandamanaji na kuharibu mpangilio.
 
Polisi wanalazimisha naibu waziri mkuu apite. Wananchi wamegoma.

Ni maandamano ya kutoka Uyole.

Naibu waziri mkuu anazomewa

Wamepitisha magari pembeni baadhi ya watu wanarusha chupa. Msafara wa Naibu Waziri Mkuu una magari kama 50.

Mbeya sio mchezo.

Naibu waziri mkuu kapitishwa pembeni baada ya wananchi kugoma.

Lissu awaambie waandamanaji kwa muda huu barabara hii ni ya waandamaji.
Nadhan kumpitisha Biteko hapo ni setup ya mfumo kutest hamasa za waandamanaji na Biteko ametolewa kama chambo bila yeye kujiua.
 
Amani imerudi baada ya msafara wa naibu wa waziri mkuu kupita.

Tundu kahutubia na sasa msafara unaendelea kawaida.

Nafikiri kuna kitu wamejifunza kwamba watu wako serious. Waligoma kabisa kumpiga Biteko.
Nilikuwepo aisee nao wa msafara wamezingua sana
 
Tutakua taifa la Aina gani? Leo CCM, ACT, Wakristo, Waislamu watake kuandamana kuwasilisha ujumbe wao Barabara zifungwe kwaajili yao? Sio kweli
Maandamano popote pale duniani kikawaida barabara hufungwa kama waandamanaji ni wengi.
Pia polisi wanaweza kuongoza kama waandamanaji wachache ili kutoa nafasi kwa wengine pia kutumia barua.. Lakini kwa maandamano makubwa kama haya Huwezi kuruhusu tena wapinzani wao watumie barabara hiyo hiyo kwa wakati huo huo. Ni hatari mno.
 
RPC mkoa wa Mbeya anamsalimia Lissu na Mwabukusi na kuwaambia wapo kuwalinda na maandamano yaendelee.

Polisi wame behave vizuri. Walivyoona wananchi hawataki kuachia barabara hawakutumia nguvu badala yake wakatafuta njia mbadala kumpitisha Biteko.
 
Naibu Waziri ni mtu mmoja, maandamano ni ya maelfu ya watu. Kwa nini Naibu Waziri asiheshimu wananchi walio wengi? Polisi wana taarifa na details zote za barabara gani watatumia waandamanaji, na muda gani, kwa nini wasimtafutie alternative road kuliko kuwasumbua waandamanaji na kuharibu mpangilio.
Taarifa za Polisi za kukubali haya maandamano hazikuonyesha barabara zilizopangwa zitakuwa za maandamano pekee kwa siku na muda husika, taarifa zinaonyesha barabara itatumiwa upande mmoja na mwengine utatumiwa na watu wengine
 
Back
Top Bottom