Mapenzi mapenzi yanahitaji akili na uvumilivu kweli.
Nakumbuka siku namaliza mtihani wa kidato cha 6 nilirudi ghetto huku na furaha tele. Nafika tu mtaa niliopanga ghetto langu namtafuta manzi wangu tupige picha ya ukumbusho akataa kabisa hali inabadilika natokwa na jasho na mwili unalowa.
Nilikua nampenda saana yeye aliishia kidato cha 4. Kesho yake namfata kwao kujua kulikoni namfumania na njemba, akili ziliniruka kama mweu nilitembeza kipigoo hatari nilikua nasikia tu majirani wanasema nitauaa. Kila nikiwaza tukio lile ningeishia polisi na kuniharibia future zangu shukrani zimuendee dada wa bint ambaye alizuia wasiende polisi.
Nikiwa chuo tena yakanipata nilikua na mahusiano na bint mwanachuo nikajikuta nampa ujauzito kumbe nyumbani alikua na mahusiano na jamaa mimi nilidanganywa. Yule jamaa alipogundua alikua mbogo aswaa pona yangu ni umbali maana matusi, vitisho tele.fikiri kama tungekua karibu. Wakafanya mchakato wakautoa ule ujauzito najua jamaa aliumia sana.
Nilimaliza salama na bahati nikapata ajira, nafurahia maisha ya single. Wao hadi leo hawajaolewa.
Pumzika kwa Amani kamanda!!