Pre GE2025 Mbeya: RC Homera aagiza kukamatwa kwa kijana aliyemkashifu Rais Samia na kuichoma picha yake

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
kwa hiyo wewe unataka ma idiot yanayotukana wakubwa ndiyo yasikilizwe ?unaweza kuta huyo kijana hata kushika jembe akalime viazi ( maana ni dili sana kule MBEYA) HAJUI anabaki anamtukana mkuu wa nchi.

Franz Kafka > Quotes > Quotable Quote​

(?)
Franz Kafka

“One idiot is one idiot. Two idiots are two idiots. Ten thousand idiots are a political party.” they can even vote one idiot as president to represent them​

― Franz Kafka
tags: idiot, political, political-party
Matusi ninayoona mimi ni mijizi serikalini kuendelea kuiba huku rais anayaangalia tu. Hayo ndiyo matusi kwetu sisi wananchi....subri mtoto wako awe shoga kweye wimbi hili liloingia laba utatoa pongezi...
 
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya ametoa masaa 24 kutiwa mbaroni Kwa Kijana mmja huko Wilayani Rungwe ambae inadaiwa amemkashifu Rais Samia na Kuichoma Picha yake.

My Take
Naunga mkono hoja, upumbavu wa tabia za kihuni za kuiga ukomeshwe na usiruhusiwe hapa Tanzania.

Mnaweza kupinga Kila kitu kadiri inavyowezekana lakini kwa namna ya kuwaheshimu hao msiokubaliana.

Tanzania haiwezimkiwa Taifa lawahuni.

====

Mkuu wa mkoa wa mbeya cde: Juma Z. Homera amemuagiza Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Mbeya SACP Benjamini kuzaga kumsaka na kumkamata kijana anayepatikana Ntokela Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya kwa kosa la kumkashifu Rais Samia kwa maneno makali na kisha kuichoma moto picha inayomuonyesha Rais.

RC Homera amelaani vikali kitendo hicho kuwa si cha maadili wala uungwana na kiko tofauti na utamaduni halisi wa wananchi mkoani Mbeya.

Hata hivyo ametoa masaa 24 kwa Kamanda Kuzaga kumkamata kijana huyo ili alisaidie Jeshi la Polisi juu ya tuhuma hizo na mashambulizi hayo ambayo kayaelekeza moja kwa moja kwa Rais Samia.

Mwisho RC Homera amewasihi wananchi mkoani Mbeya kutojiingiza kwenye vitendo viovu kwa kukashifu viongozi makusudi badala yake wajikite katika utafutaji na uchapa kazi kwa manufaa ya familia zao na Tanzania kwa ujumla.

View attachment 3031314
Video ya Kijana akichoma moto picha ya Rais Samia.
Haya ni matumizi mabaya ya jeshi la polisi, rasimali za taifa na muda. Sijaona popote pale huyo kijana akivunja sheria. Kaonyesha hisia zake, kachoma picha ambayo ni mali yake. Sasa kama huo sio uungwana na sio utamaduni wetu, hayo hayamhusu mhusika na hayana nguvu za kisheria kumshtaki.
 
Je kuna Jinai kuchoma Picha?! Mimi mbona nimechambia sana Picha za Magufuli na sijakamatwa?!

Acheni zenu banaa...
Mimi sisapoti huo ujinga, ila watu wamechoka, matozo ni mengi mno. Mama awe makini sana na wanyuma yake
 
Mnaweza kupinga Kila kitu kadiri inavyowezekana lakini kwa namna ya kuwaheshimu hao msiokubaliana.
Kwani "heshima" ni kitu gan; inatokana na nini na ni nani anaye heshimika?

Utamheshimu mtu unayeona anakiuka unayo yaamini wewe

Sijasema naunga mkono yanayodaiwa kufanywa, kama ni kweli yalifanyika.
 
Ni bahati mbaya sana kama taifa MTU mara apatapo uongozi hugeuzwa/hujigeuza kuwa mungu.
 
😂 😂 😂
Ingechomwa Picha ya Lissu, Mbowe au Zitto lingetoka tamko na amri kama hii?
Halafu Picha inahusiana nini na hadhi na madaraka ya Rais?
 
Mbona mkuu wa mkoa kakazana kusema chalii katoa kauli chafu sijui matusi ni kama kamtukana mama mzazi na blah blah kibao wakati kwenye video dogo hajatukana tusi hata moja.!!
Au RC hata video hajaiona ila kaamhiwa tu kemea na utoe maamuzi ..
 
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya ametoa masaa 24 kutiwa mbaroni Kwa Kijana mmja huko Wilayani Rungwe ambae inadaiwa amemkashifu Rais Samia na Kuichoma Picha yake.

My Take
Naunga mkono hoja, upumbavu wa tabia za kihuni za kuiga ukomeshwe na usiruhusiwe hapa Tanzania.

Mnaweza kupinga Kila kitu kadiri inavyowezekana lakini kwa namna ya kuwaheshimu hao msiokubaliana.

Tanzania haiwezimkiwa Taifa lawahuni.

====

Mkuu wa mkoa wa mbeya cde: Juma Z. Homera amemuagiza Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Mbeya SACP Benjamini kuzaga kumsaka na kumkamata kijana anayepatikana Ntokela Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya kwa kosa la kumkashifu Rais Samia kwa maneno makali na kisha kuichoma moto picha inayomuonyesha Rais.

RC Homera amelaani vikali kitendo hicho kuwa si cha maadili wala uungwana na kiko tofauti na utamaduni halisi wa wananchi mkoani Mbeya.

Hata hivyo ametoa masaa 24 kwa Kamanda Kuzaga kumkamata kijana huyo ili alisaidie Jeshi la Polisi juu ya tuhuma hizo na mashambulizi hayo ambayo kayaelekeza moja kwa moja kwa Rais Samia.

Mwisho RC Homera amewasihi wananchi mkoani Mbeya kutojiingiza kwenye vitendo viovu kwa kukashifu viongozi makusudi badala yake wajikite katika utafutaji na uchapa kazi kwa manufaa ya familia zao na Tanzania kwa ujumla.

View attachment 3031314
Video ya Kijana akichoma moto picha ya Rais Samia.
Safi sana Polisi Kwa kumtia ngivuni yule mhuni 👇👇

View: https://www.instagram.com/p/C87FFmKqZ_m/?igsh=MWl3c2FrZzAwMm55YQ==
 
Mbona mkuu wa mkoa kakazana kusema chalii katoa kauli chafu sijui matusi ni kama kamtukana mama mzazi na blah blah kibao wakati kwenye video dogo hajatukana tusi hata moja.!!
Au RC hata video hajaiona ila kaamhiwa tu kemea na utoe maamuzi ..
Hili ni la kupuuza tu yaani sijui inakuwaje hawa Viongozi Vijana wamekuwa Washamba na Kujipendekeza kumekuwa kwingii na hii yote ni dalili ya kutokujiamini aisee
 
Back
Top Bottom