Hii ni sheria mbaya haifai. Kwanza ni ya kibaguzi kwa sababu kuu TATU:
1. Sheria hii haizungumzi kuhusu wasagaji, kitu ambacho kinaenda kinyume na madhumuni ya kuundwa kwake.
Ni mashoga pekee ndio wahanga wa sheria hii. Huu ni ubaguzi wa kionevu na ni kinyume na katiba.
Kama lengo ni kuzuia mapenzi ya jinsia moja, kwanini usagaji uwe halali halafu ushoga uwe haramu? HILI NALO MKALITIZAME.
2. Sheria hii haishughuliki na HETEROSEXUAL SODOMY. Wale wanaowafira wake zao wako salama na hakuna anayewagasi au kuwabughudhi.
Kama lengo kuu ni kuzuia MATENDO YA KINYUME NA ASILI, kwanini kumfira mwanamke ni halali, wakati kumfira mwanaume ni haramu?
JAPO SHERIA imesema vyote ni haramu lakini utekelezaji wa sheria unadhihirisha wazi kwamba hapa walengwa ni mashoga tu na sio mabasha au wanawake.
3. Sheria hii inatekelezwa kihuni kwa kumkamata kila mwenye mwonekano wa kike na kuanza kummulika na makamera. Na kwenye EXTREME CASES, hata kumpima kwa kumpiga vidole mkunduni. Huku ni KUTWEZA UTU.
Si kila shoga ana mwonekano wa kike. Kwahiyo kuwawinda na kuwa-target watu wenye mionekano ya kike si sawa. After all hakuna sheria inayozuia mtu mume kuwa na mwonekano wa kike kwa minajili ya bayolojia yake au mavazi yake. Huu ni UHUNI.