Mbeya: Wananchi wajitokeza kufuatilia kesi ya kupinga kusainiwa kwa mkataba wa bandari

Mbeya: Wananchi wajitokeza kufuatilia kesi ya kupinga kusainiwa kwa mkataba wa bandari

Kamanda Asiyechoka

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2020
Posts
3,315
Reaction score
5,058
Wananchi wamejitokeza katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mbeya kufuatilia kesi ya kupinga kusainiwa kwa mkataba wa bandari iliyofunguliwa na wanasheria Boniface Mwabukusi na mwenzake Philip Mwakilima, wakisema mkataba huo hauna maslahi kwa Taifa na haujashirikisha maoni ya Watanzania ili kuuridhia kati yake na kampuni ya DP World ya Dubai.

Jambo TV

Kesi Bandari.jpg
 
Naamini haki itatendeka, kwa sababu naamini jaji wa hiyo kesi sio mzanzibari, na sheria zilizovunjwa ziko wazi kila mwenye macho anazifahamu, mkataba wa kihuni uliokuja kuvunja sheria za Tanganyika, badala ya kufuata sheria za Tanganyika.
 
Unapoingiza Uzanzibari ndio unapokosea bwashee!
 
Naamini haki itatendeka, kwa sababu naamini jaji wa hiyo kesi sio mzanzibari, na sheria zilizovunjwa ziko wazi kila mwenye macho anazifahamu, mkataba wa kihuni uliokuja kuvunja sheria za Tanganyika, badala ya kufuata sheria za Tanganyika.
Endelea kuota mkuu, ukija kustuka bandarini kuna watu wenye weledi na sio wezi
 
Kama ni Kidume kwenye hili sakata huyo jamaa aliefungua kesi basi ni kidume na nusu.
 
Naamini haki itatendeka, kwa sababu naamini jaji wa hiyo kesi sio mzanzibari, na sheria zilizovunjwa ziko wazi kila mwenye macho anazifahamu, mkataba wa kihuni uliokuja kuvunja sheria za Tanganyika, badala ya kufuata sheria za Tanganyika.
Anaweza asiwe Mzanzibar akawa mtu wa Pwani au Tanga
 
karme hii hakuna MTU kukubali kunyonywa na mabeberu
 
Kumbe yule Mwakilishi wao ambaye ni Spika hawakutuma hayo aliyoyakubali pale Dodoma ?

Basi wasifanye ajizi kumfikishia taarifa Pindi atakaporudi....
 
Endelea kuota mkuu, ukija kustuka bandarini kuna watu wenye weledi na sio wezi
Tutashitukia baglashia na hizblaa zimejaa bandari I ndio furaha yako wala hakuna Cha weledi hapo.Mama amewapa Bure bure
 
Na kalamu Maria Sarungi-Tsehai

Port of Dar - TPA and Benki ya Dunia
Nawarudisha mwaka 2017/18 Benki ya Dunia ilikubali na kuingia mkataba wa mkopo wa maendeleo na serikali wa kuimarisha Bandari ya Dar es Salaam chini ya mradi unaoitwa Dar es Salaam Maritime Gateway Project ambapo dola za kimarekani (USD) milioni 400 ilitolewa kuimarisha miundombunu halisi (phyiscal) na dola milioni 21 kwa ajili ya kuimarisha taasisi na kusaidia kutekeleza mradi Mamlaka ya kutekeleza mradi huu ni TPA - pesa ilienda huko Mradi unaisha 30 June 2024 (mwakani) Kwa kifupi sisi wananchi tutalipa deni hili sehemu kubwa ya milioni 421 iliyotolewa na Benki ya Dunia na kuwekezwa ktk kuimarisha bandari Sasa tuchambue ripoti nini kimefanyika, na kwa nini DP World imetajwa katika ripoti hii?
Katika muhtasari wa Dar es Salaam Maritime Gateway Project report iliyotolewa February 2023 (mwaka huu) inaonyesha kuwa utekelezaji umezidi kuzorota na RISK ya mradi umeongezeka na kuwa SUBSTANTIAL yaani kuna hatari mradi kutotimiza malengo Inaelezwa kuwa mradi huu ulioidhinishwa 2017 na kuanza kutekelezwa 2018 ina mikataba 7 ikiwemo mashirika 5 ya consulting. Utekelezaji bado siyo mzuri na lengo la kuONGEZA UFANISI wa ports and terminals zote zinazoendeshwa na TPA, na kuijengea uwezo kuwa MENEJA na DEVELOPER (mwendelezaji) wa ports zingine huku ikiendelea kutathmini uwekezaji binafsi (tulikuwa bado hatujafikia hiyo hatua)
Katika ripoti ya World Bank ghafla DP World imeibuka Sasa ngoja niwaeleweshe Sehemu ya mkopo na msaada wa $421 milioni kuna pesa ya kujenga mfumo wa IT wa bandari kupitia TPA. Ripoti ya Benki ya Feb 2023 walisema hakuna maendeleo ILA TPA imesema imeingia makubaliano (MoU) na DP World kujenga mfumo huu wa IT ELEWENI: DP World watalipwa kutoka pesa hizi za mkopo wa Benki ya Dunia kusaidia “mifumo isomane” hawawekezi Pili kwa mujibu wa serikali walisema ile MoU ya TPA na DPW ni kuhusu mfumo wa IT (tunaambiwa ilisainiwa Feb 2022) Imekuwaje consultancy ya DPW ya IT imegeuzwa kuwa IGA na tunatoa bandari zetu kwa kusema eti DPW watatusaidia mifumo isomane alafu tunawapa uendeshaji wa bandari ambao UMESHAKAMILIKA kwa uwekezaji mkubwa wa mradi huu? Hii dili ilianza kama CONSULTANCY na kugeuzwa UPORAJI.

Pesa za mkopo wa World Bank zimetumika (na kukamilika) kupanua na kuimarisha Gati 1-7 na kujenga gati mpya Gerezani kupanua mlango wa bandari hadi Gati 11 kuboresha na kuunganisha na reli Kupanua na kuimarisha Gati 8-11 Kuna RORO terminal ilijengwa na kukamilishwa Sasa tuangalie wanachodai DP World kufanya kwa mujibu wa IGA Cha kwanza kikubwa eti kujenga, kuendesha na kusimamia RoRo terminal na Gati 1-4 na gati 5-7 Yaani pesa zote zimewekezwa za walipa kodi kupitia mradi wa sasa wa WB alafu wao wanakuja kuendesha na kusimamia? Wanawekeza nini?? Ndiyo maana mkataba haujawekwa thamani ya uwekezaji wao kumbe wanadandia mradi unaoelekea kukamilika waje wajisifu! Nyieeeeeeeeee! Mnaotetea mkataba huu mnajua kuwa mnatumika kutetea ulaji wa genge ndogo!?
 
Sugu vipi mbona kimyaaaa! Hata kuwaanzishia jamaa harambee kwa maslahi ya taifa hamna? Jamaa huwa ni mbishi kwa Asili
 
Wananchi wamejitokeza katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mbeya kufuatilia kesi ya kupinga kusainiwa kwa mkataba wa bandari iliyofunguliwa na wanasheria Boniface Mwabukusi na mwenzake Philip Mwakilima, wakisema mkataba huo hauna maslahi kwa Taifa na haujashirikisha maoni ya Watanzania ili kuuridhia kati yake na kampuni ya DP World ya Dubai.

Jambo TV

Wanyak hatutaki mkesyoo oh, ni wabishi na masikini jeuri, baba zetu waliwahi mwambia Nyerere kama hamtutaki kusikiliza tutahamia Malawi.
 
Back
Top Bottom