Mbeya: Watu wanne (4) mbaroni kwa kufurahia kifo cha Rais Magufuli kwa kupika supu na kununua lita 20 za Ulanzi

Mbeya: Watu wanne (4) mbaroni kwa kufurahia kifo cha Rais Magufuli kwa kupika supu na kununua lita 20 za Ulanzi

Unaweza ukaona kama utani ila kuna jamaa aliniambia maeneo ya kwao walikunywa pombe hiyo tar 18 balaa,kuna jamaa akanipigia simu anashangilia ila kwa ile tone inaonekana alikuwa bwiiii.
Tupo zaid milion 50 wanaonekana road hawazid ata million moja wengine wako wap sijui😂
 
Tupo zaid milion 50 wanaonekana road hawazid ata million moja wengine wako wap sijui😂
Propaganda za MATAGA tu,ukitaka kujua ni wanafiki ngoja siku 21 ziishe utaona tu maana itabidi waanze kumpigia pambio Mh Rais Samia na kumsahau MEKO.
 
Polisi waache hofu labda hao jamaa walikuwa WAJUKUU wa JPM kiumri hivo kimila na kidesturi uwa ni sherehe kabisa
Ninaposema sherehe na maanisha ni sherehe
 
Hii Serikali mbona inafanya mambo ya aibu?
Toka lini msiba ukawa ni wa lazima kwa kila mtu kusikitika au kuhuzunika??

Rais SSH usipokemea huu wendawazimu wa Serikali yako, mwisho wa siku na wewe utaonekana ni mmoja wao. This madness has to be condemned strongly!

Hapa kidogo tunakosea kumhusisha SSH na mambo yanayoendelea sasa hivi. Hii bado ni serikali ya JPM. SSH bado hajaunda serikali yake.
 
Nadhani hao maofisa wanashindwa kuelewa kuwa wenyeji wa mikoa kama Mbeya, Kagera, Iringa na Kilimanjaro kuombeleza kwa kunywa ni sehemu ya mila na desturi tena hasa akifariki mtu mzima wa rika la Magu
 
Hapa kidogo tunakosea kumhusisha SSH na mambo yanayoendelea sasa hivi. Hii bado ni serikali ya JPM. SSH bado hajaunda serikali yake.
Lakini tayari ameshakula kiapo cha kuwa Rais. Sasa hivi Serikali yote iko chini ya mamlaka yake, iwe aliwateua au hakuwateua, they report to her.
 
Kitendo cha kutaja tu hapo Mbele ya makamela kwamba, wamewashika watu wakijipongeza Kwa kifo cha kipenzi cha Watanzania wengi, ni kuongezea udhalilishaji pia,

Kwa nini wasingewakamata kimyakimya??
Na kwanini wawakamate kimya kimya, wacha waanike akili zao ulimwengu ushangae yanayofanywa na waliopewa dhamana ya kulinda raia na mali zao.
 
Kuna kesi za mauaji hazina watu kwanini wasiunganishiwe hawa ngedere
 
hao ndio Bina bin damu a.k.a Binadamu na wakiwa wengi kama hao waliojitia ganzi za ubongo wanaitwa Wana halafu damu.
Mungu aturehemu tu. Kweli mtu ikiwa mwezi kiasi cha kushangilia kifo hadharani!..khaaa...
 
Duuuuu Jamaa mmoja hapo katika hao ninamfahamu Asifiwe Mwasaga ni dereva wa magari ya mizigo yanayopaki Mwanjelwa karibu na sheli ya Chipukizi.
Madereva wa Magari ya mizigo waliathiriwa sana na utawala Huu baada ya Wadau wengi kuhamishia mitaji yao nchini Msumbiji Bandari ya Beira
 
Kinachowauma polisi ni supu ya mbuzi iliyoandaliwa na watuhumiwa wakati wenyewe wametoka kula kande
 
Kupika supu na kunywa pombe ni kusheherekea kifo cha mtu kwani??
 
Tulimpoteza Mwalimu Nyerere, Baba wa Taifa letu. Tulihuzunika sana. Sikuwahi kusikia au kuona kwenye mtandao wowote, mtu yeyote akifurahia.

Tukampoteza Aboud Jumbe, sikushuhudia yeyote akifurahia.

Tulimpoteza Simba wa Vita, Rashid Mfaume Kawawa. Hakika sikushuhudia mtu yeyote akifurahia.

Akafariki mzee wetu Mkapa, tulipatwa na butwaa, tukahuzunika. Sikumsikia wa kufurahia.

Lakini ni nini hiki? Maana si mtu mmoja, bali ni watu wengi, iwe ni mitaani, kwenye mitandao, mpaka kwenye ofisi za umma!! Watu wengi, siyo watu 10 au 100, bali ni wengi, wanaonekana kufurahia, na kuwa na matumaini mapya.

Sauti ya wengi ni sauti ya Mungu. Vilio vya wengi dhidi yako, ni hukumu yako siku ya mwisho. Daima umwombe Mungu akupe hekima ya kuyatambua yaliyo mema, ili uwatendee heri wanadamu wenzako.
 
Back
Top Bottom