Shalom Mtumishi wa Mungu!
Binafsi ni Mkristo, ninayeabudu kwenye Kanisa lolote lile pale Moyo wangu ukijiskia Amani kwalo.
Kama Mkristo ambaye namwabudu Mungu, naamini juu ya Mwanae Yesu Kristo, na kama Mkristo ambaye nasoma Biblia, kufunga na Kuomba, ili kuwa karibu na Mungu, na kwa Mkristo yoyote yule aliye hai ndoto yake baada ya Maisha haya ni kwenda Mbinguni kwa Mungu Baba!
Tunasoma Biblia kwa uchache inagusia kuhusu Maisha ya Mbinguni, tumekua na Nadharia nyingi na watu kutaka kufahamu kuhusu Mwonekano, Mazingira ya huko Mbinguni japo watu kujaribu kupata picha kukoje, ila mara nyingi ni kuwa lazima Maisha yako yaishe kwa Wema hapa Duniani ili upate nafasi kufika huko!
Nina furahi kusikia kwamba Mtoa post umefika huko kupitia Ulimwengu wa roho!
Nina maswali machache nataka kukuuliza!
Nitaanza na Maswali, umesema ulipofika Mbinguni ulikuta Watu wanaimba Wimbo ambao pia naupenda sana " Mungu wangu, nashangaa Kabisa........!"
1. Je! Huo wimbo ulikua unaimbwa kwa Lugha gani!?
2. Wewe na Malaika mlikua mnaongea Lugha gani!?
3. Malaika kwa Mwonekano alikua wa Rangi gani!? (Mwafrika, Mzungu, Mchina).
4. Hao watu uliowakuta huko Mbinguni mkiimba wote, walikua katika Mwonekano wa jamii moja, Rangi moja, ama Races mchanganyiko kama tulivyo Duniani!?
5. Katika hao watu huko Mbinguni kulikua na Wazee, Vijana na Watoto ama wote walikua katika rika moja?
Asante Mtumishi, ni katika tu kujifunza.