Mbingu ni kweli ipo na huu ni ushuhuda wangu binafsi

Mbingu ni kweli ipo na huu ni ushuhuda wangu binafsi

Hapana bro, Mungu ni muaminifu, wa haki, halazimishi na wala sio mkoloni. Yeye amekupa uhuru wa kuchagua nji uipendayo. Amekuumba mwanadamu ukiwa kiumbe kitimilifu na kukipa mamlaka ya kuchagua wapi pa kwenda. Umilele wako unauandaa wewe mwenyewe kwa kuchagua njia uipendayo. Yeye anasema tazama nimeweka njia mbili kwako njia ya uzima na njia ya mauti. Chagua wewe uzima au mauti. Njia ya uzima ni kumuishia yeye katika kicho na utakatifu ila njia ya mauti ni kuishi katika dhambi. Chagua fungu lako sasa bro.
Kwani hii akili ya uchaguzi wa zuri na baya imewakwa nanani aliyeziwela alijua IPI itakuwanangu kwangu nakama alijua na ilafanya kama alivyojua ninani wakuraumiwa aliyeziweka au mtumiaji?
 
Kwani hii akili ya uchaguzi wa zuri na baya imewakwa nanani aliyeziwela alijua IPI itakuwanangu kwangu nakama alijua na ilafanya kama alivyojua ninani wakuraumiwa aliyeziweka au mtumiaji?
Aiseeee, ebu soma tena hiki ulichoandika dogo.
 
Aiseeee, ebu soma tena hiki ulichoandika dogo.
Asate kwa kunisahihisha. Nilikuwa namanisha hivi. Kwani hii akili ya uchaguzi wa zuri na baya imewekwa nanani aliyeziwela alijua ipi itakuwa nanguvu kwangu nakama alijua na inafanya kama alivyojua ninani wakuraumiwa aliyeziweka au mtumiaji?
 
Hata enzi za Nuhu walisema hivyo kwa kuwa hawakuwahi ona mvua kubwa. Sodoma na Gomora walisema na kutamba hivyo lakini hasi leo miji hiyo imebaki kuwa majivu kama ushuhuda wa vizazi na vizazi. Hukumu ya milele ipo hata, kuzimu ipo, jehanum ya moto ipo. Ni wewe kuchagua sasa umilele wako kuwa utaishi wapi. Acha kujidanganya.
Hahahah! sasa unatoa referrence kutoka kwenye hicho hicho kitabu cha watu unahisi nitakuelewa?
 
Nimeona watu wengi humu JF wakimponda na kumkashfu Mwalimu Mwakasege baada ya kusema Mungu alimfunulia kuhusu mbingu na kwenda Mbinguni.

Binafsi nadeclare interest kuwa ninatumika Kanisa la TAG kama Mzee wa Kanisa huku Nyanda za juu kusini pia ni Mtumishi wa Serikali na huwa nahubiri mara moja moja. Siandiki hivi kwa kufurahisha watu au kujisifu wala kutaka kumsafisha Mwalimu Mwakasege ila naeleza kile nilichoshuhudia na kile ambacho Mungu amenitendea.

Kwa umri na muda niliomtumikia Mungu kama Mkristo nafahamu Mungu anajifunua kwa watu wengi yeye binafsi na pia kuwafunulia kuhusu wengi kuhusu mbingu.

Binafsi, nashuhudia leo na kikiwa na akili timamu na dhamira njema Moyoni mwangu kuwa nimemuona mwenye haki "Yesu Kristo" si chini ya mara 4 toka nikiwa mdogo na amenitokea kwa namna mbalimbali tofauti na watu wanavyokashfu kuwa tutatokewa na Mapepo yaliyovaa sura ya "Bryan Deacon" yule aliyeigiza "Filamu ya Yesu" Pia nashuhudia, Mungu kunifunulia na kuiona mbingu.

Mafunuo haya ya kutokewa na Yesu kwangu mimi hayakuwa kwa jinsi ya kimwili "yaani kunitokea physically" ila ni katika ndoto na Maono ya usiku pia wakati nasali nikajiona tu nimekutana naye.

Leo sitaelezea kuhusu kutokewa na Yesu ila nitaelezea kuhusu ushuhuda wangu wa kuiona Mbingu ila nasisitiza katika hilo, kila maono, ndoto au mafunuo ya Kimungu yanajengwa chini ya Neno la Mungu. Neno: Ayubu 33:14-16 hapa Mungu anasema kuhusu kusema na wanadamu kuhusu ndoto ns mqono ya usiku.

Neno: Yoel 2: 28-29 Anasema kuhusu "Ndoto na Maono".

Kuhusu Mungu kuwafunulia watumishi wake mbingu, tunaona Paulo anasema namna alivyochukuliwa na kuoneshwa kuhusu Mbingu katika 2 Korintho 12: 2-9 pia Stephano naye anafunuliwa katika Matendo ya Mitume 7:56 na pia Mtume Yohana anafunuliwa kuhusu Mbingu wakati anaandika kitabu cha Ufunuo wa Yohana.

Binafsi, Nakumbuka ilikuwa 2016. Mungu alinipa Neno toka Yeremia 33:3 inayosema "Niite nami nitakuitikia na nitakuonesha mambo makubwa, magumu usiyoyajua" pia kwa muda mrefu nilikuwa naimba moyoni mwangu wimbo mmoja wa zamani sijui uliimbwa na kwaya gani ila kuna kipande wanaimba " Nimpeleleza nani raha ya Mbingu×2, Yesu ndiye wa Kumpeleleza"

Nakumbuka Siku hiyo niliamka kama kawaida saa 9 alfajiri na kusali. Ilipofika saa 11:45 nikasema nilale kidogo ili nikiamka saa 1 hivi niende kazini. Nilipolala kama saa 12 alfajiri nikaona Malaika mmoja aliye kama mwanadamu amevaa mavazi meupe yenye kung'ara huku akiwa mwenye sura inayong'ara ananiambia "nimetumwa nikufuate". Akanishika mkono, nikaona natoka kwenye mwili upande wenye moyo.

Nikapita kwenye bati la nyumba bila kizuizi. Safari ya kupanda juu ikaanza kwa speed ya ajabu huku akiwa amenishika Mkono. Nikaangalia chini na kuona mwili wangu, mke na mtoto wangu wamelala kitandani. Unaona nyumba na miti ya duniani. Tukapaa juu kwa spidi nikaangalia chini tena na kuona kadunia kalivyo kadogo then tukafika katika nchi ile ambayo "watu" wanaimba na kumuabudu Mungu. Nikaungana nao tuliimba "Bwana Mungu nashangaa kabisa"

Sijui nielezeje muonekano wake nchi ile ila ni nzuri na ya meta meta. Hali ya hewa na mazingira ni tofauti na huku duniani. Nchi ile ni kweli na mji ule ni kweli. Jitahidi usikose kuingia mji ule.

Baadaye nikaambiwa turudi na kwa speed ya ajabu, najikuta naingia mwilini mwangu upande wa kushoto kwenye moyo, mwili ukawa kama umepigwa "shot" nikashtuka.

Binafsi, nimewasikia na kuwaona watumishi wengi wa Mungu wanaoshuhudia kuhusu Mbingu huku kwetu na sehemu myingine. Ukiacha hao maarufu, japo "Zumaridi hapana kwani inaonekana ana shida ya akili" Ukiacha Mwakasege, hata Marehemu Kulola alishashuhudia siku moja kufunuliwa kuhusu Mbingu.

Nami nimeona nishare uzoefu wangu kuhusu Mafunuo ya Mbingu. Siku nyingine nitaeleza kuhusu kutokewa na Yesu ana tutokeaje, yupoje na tunajuaje kama ni Yesu.

Asanteni.
Hahahahaha dah
 
Inaonekana una amini Mungu kwa sababu umetishiwa moto. Mbali na hayo matisho Mungu ni Hadith ya kufikirika tu. Hayupo hajawai kuwepo na hatokaa awepo
Kama akili yako imesalimika bila kuchafuliwa na fikra za wana falsafa na wapuuzi wengine basi hata wewe mwenyewe ukijitizama ni ishara tosha kuwa yupo aliyekuumba, mambo ya moto ni imani ya juu sana jitizame tu kwenye kioo ni ishara tosha.

Kwahyo huu ulimwengu, mvua kunyesha, upepo, bahari kupwa na kujaa, watu kuwa matajiri wengine maskini, wengine kulia machozi wengine kucheka, wengine kufa wengine kuzaliwa, wengine kuishi maisha marefu wengine kufa mapema, mambo yote haya anayafanya putin sio?.
 
Roho zote kabla ya kuingia ktk tumbo la mwanamke na Kuzaliwa mtoto wa kike au kiume ASILI yake ni MBINGUNI.

Hata bila kwenda Mbinguni, IPO connection ya Roho na Mbinguni.

Mungu husema na Kila mtu Usingizini katika NDOTO, Maono au ktk Ulimwengu wa Roho.

Mungu kusema nawe na usisikie au kuelewa haimaanishi kuwa hasemi na WANADAMU.

Tusiwe wabishi, Tujifunze namna ya kuisikia sauti ya Mungu na kuelewa asemacho maana daily husema nasi na Kila tulalapo Huwa tunaenda Mbingu mbalimbali Kila tulalapo.
 
Nijaaminishwa katika quran au biblia ili kuamini dini za kimapokeo zilizoletwa na wanyonyaji,dhurumati,wezi,nk.

Ni wapi iwe Afrika,Asia,Amerika au Ulaya amewahi kukufuka au kufufuliwa mtu yeyote?

Basi wale wote wanaomfuata yesu au muhamad hasa masheik na wachungaji wangekuwepo waliowahi kufufuka.

Mtu hupaswa kuamini kinachomtokea au kilichowahi kutokea ktk jamii anayoishi siyo VYAKULETEA /KUHADITHIWA.

Yaani mnaoshinda mnasali miskitini na makanisani mmekithiri kwa umaskini hao wanaodai wanapeleka mbunguni ni wanatajirika kwa ujinga wenu.

Ni wapi unapoweza kuwatenganisha au kuwagundua wanaosali na wasiosali kwa kuwaangalia?

Ongezeni na akili zenu
Wapi kwenye Qur'an pameandikwa mtu wa mashariki ya kati atafufuka 2023, mkuu mnalala vizuri kweli usiku?.
 
Sasa mbona umerudi hukuchagua kubaki mbinguni. Au kule hakuna mbususu ukaona weee wasikutanie
Nathamini muda na comment yako asante kwa kucomment ila jitahidi kuficha uchi wa akili yako mbele za watu. Unajidharirisha na kujivua nguo. Ungepita kimya tusingeona uchi wa akili yako.
 
Sikatai mungu yupo ila hayo mengine, mmmmhh!

@kazakhdestoyer na Kinengunengu usikute na nyie mnaamini kuwa yesu ndie mungu muumba
 
Fungua U-tube, tafuta mtu Sonhguru, amesema nini kuhusu Mbinguni!! Maisha ni haya haya, hakuna mengine zaidi ya haya.
 
Asilimia kubwa ya wanaopinga kuhusu Mungu na Mbingu ni WITCHES.

Kuna watu humu wanashuka kuzimu kutafuta Mali, lakini ni WA kwanza kupinga INJILI, uwepo wa Mungu na Uweza wake.

Wanazijua Kona zote za KUZIMU na hawataki watu wamjue Mungu na Mbingu iliko asili ya Roho zote za WANADAMU.
 
ulisema ulikuta mbinguni wanaimba je ilitumika lugha gani huko..?
 
Ili uishi kwa amani, kariri kuwa hizi ni hadithi za sungura. Mbinguni na motoni ni maisha unayoishi hapa duniani. Maisha ya raha ni Mbinguni na maisha ya mateso ni motoni. Ukifa ni jumla.
 
Nimeona watu wengi humu JF wakimponda na kumkashfu Mwalimu Mwakasege baada ya kusema Mungu alimfunulia kuhusu mbingu na kwenda Mbinguni.

Binafsi nadeclare interest kuwa ninatumika Kanisa la TAG kama Mzee wa Kanisa huku Nyanda za juu kusini pia ni Mtumishi wa Serikali na huwa nahubiri mara moja moja. Siandiki hivi kwa kufurahisha watu au kujisifu wala kutaka kumsafisha Mwalimu Mwakasege ila naeleza kile nilichoshuhudia na kile ambacho Mungu amenitendea.

Kwa umri na muda niliomtumikia Mungu kama Mkristo nafahamu Mungu anajifunua kwa watu wengi yeye binafsi na pia kuwafunulia kuhusu wengi kuhusu mbingu.

Binafsi, nashuhudia leo na kikiwa na akili timamu na dhamira njema Moyoni mwangu kuwa nimemuona mwenye haki "Yesu Kristo" si chini ya mara 4 toka nikiwa mdogo na amenitokea kwa namna mbalimbali tofauti na watu wanavyokashfu kuwa tutatokewa na Mapepo yaliyovaa sura ya "Bryan Deacon" yule aliyeigiza "Filamu ya Yesu" Pia nashuhudia, Mungu kunifunulia na kuiona mbingu.

Mafunuo haya ya kutokewa na Yesu kwangu mimi hayakuwa kwa jinsi ya kimwili "yaani kunitokea physically" ila ni katika ndoto na Maono ya usiku pia wakati nasali nikajiona tu nimekutana naye.

Leo sitaelezea kuhusu kutokewa na Yesu ila nitaelezea kuhusu ushuhuda wangu wa kuiona Mbingu ila nasisitiza katika hilo, kila maono, ndoto au mafunuo ya Kimungu yanajengwa chini ya Neno la Mungu. Neno: Ayubu 33:14-16 hapa Mungu anasema kuhusu kusema na wanadamu kuhusu ndoto ns mqono ya usiku.

Neno: Yoel 2: 28-29 Anasema kuhusu "Ndoto na Maono".

Kuhusu Mungu kuwafunulia watumishi wake mbingu, tunaona Paulo anasema namna alivyochukuliwa na kuoneshwa kuhusu Mbingu katika 2 Korintho 12: 2-9 pia Stephano naye anafunuliwa katika Matendo ya Mitume 7:56 na pia Mtume Yohana anafunuliwa kuhusu Mbingu wakati anaandika kitabu cha Ufunuo wa Yohana.

Binafsi, Nakumbuka ilikuwa 2016. Mungu alinipa Neno toka Yeremia 33:3 inayosema "Niite nami nitakuitikia na nitakuonesha mambo makubwa, magumu usiyoyajua" pia kwa muda mrefu nilikuwa naimba moyoni mwangu wimbo mmoja wa zamani sijui uliimbwa na kwaya gani ila kuna kipande wanaimba " Nimpeleleza nani raha ya Mbingu×2, Yesu ndiye wa Kumpeleleza"

Nakumbuka Siku hiyo niliamka kama kawaida saa 9 alfajiri na kusali. Ilipofika saa 11:45 nikasema nilale kidogo ili nikiamka saa 1 hivi niende kazini. Nilipolala kama saa 12 alfajiri nikaona Malaika mmoja aliye kama mwanadamu amevaa mavazi meupe yenye kung'ara huku akiwa mwenye sura inayong'ara ananiambia "nimetumwa nikufuate". Akanishika mkono, nikaona natoka kwenye mwili upande wenye moyo.

Nikapita kwenye bati la nyumba bila kizuizi. Safari ya kupanda juu ikaanza kwa speed ya ajabu huku akiwa amenishika Mkono. Nikaangalia chini na kuona mwili wangu, mke na mtoto wangu wamelala kitandani. Unaona nyumba na miti ya duniani. Tukapaa juu kwa spidi nikaangalia chini tena na kuona kadunia kalivyo kadogo then tukafika katika nchi ile ambayo "watu" wanaimba na kumuabudu Mungu. Nikaungana nao tuliimba "Bwana Mungu nashangaa kabisa"

Sijui nielezeje muonekano wake nchi ile ila ni nzuri na ya meta meta. Hali ya hewa na mazingira ni tofauti na huku duniani. Nchi ile ni kweli na mji ule ni kweli. Jitahidi usikose kuingia mji ule.

Baadaye nikaambiwa turudi na kwa speed ya ajabu, najikuta naingia mwilini mwangu upande wa kushoto kwenye moyo, mwili ukawa kama umepigwa "shot" nikashtuka.

Binafsi, nimewasikia na kuwaona watumishi wengi wa Mungu wanaoshuhudia kuhusu Mbingu huku kwetu na sehemu myingine. Ukiacha hao maarufu, japo "Zumaridi hapana kwani inaonekana ana shida ya akili" Ukiacha Mwakasege, hata Marehemu Kulola alishashuhudia siku moja kufunuliwa kuhusu Mbingu.

Nami nimeona nishare uzoefu wangu kuhusu Mafunuo ya Mbingu. Siku nyingine nitaeleza kuhusu kutokewa na Yesu ana tutokeaje, yupoje na tunajuaje kama ni Yesu.

Asanteni.
Shalom Mtumishi wa Mungu!

Binafsi ni Mkristo, ninayeabudu kwenye Kanisa lolote lile pale Moyo wangu ukijiskia Amani kwalo.

Kama Mkristo ambaye namwabudu Mungu, naamini juu ya Mwanae Yesu Kristo, na kama Mkristo ambaye nasoma Biblia, kufunga na Kuomba, ili kuwa karibu na Mungu, na kwa Mkristo yoyote yule aliye hai ndoto yake baada ya Maisha haya ni kwenda Mbinguni kwa Mungu Baba!

Tunasoma Biblia kwa uchache inagusia kuhusu Maisha ya Mbinguni, tumekua na Nadharia nyingi na watu kutaka kufahamu kuhusu Mwonekano, Mazingira ya huko Mbinguni japo watu kujaribu kupata picha kukoje, ila mara nyingi ni kuwa lazima Maisha yako yaishe kwa Wema hapa Duniani ili upate nafasi kufika huko!

Nina furahi kusikia kwamba Mtoa post umefika huko kupitia Ulimwengu wa roho!

Nina maswali machache nataka kukuuliza!

Nitaanza na Maswali, umesema ulipofika Mbinguni ulikuta Watu wanaimba Wimbo ambao pia naupenda sana " Mungu wangu, nashangaa Kabisa........!"

1. Je! Huo wimbo ulikua unaimbwa kwa Lugha gani!?

2. Wewe na Malaika mlikua mnaongea Lugha gani!?

3. Malaika kwa Mwonekano alikua wa Rangi gani!? (Mwafrika, Mzungu, Mchina).

4. Hao watu uliowakuta huko Mbinguni mkiimba wote, walikua katika Mwonekano wa jamii moja, Rangi moja, ama Races mchanganyiko kama tulivyo Duniani!?

5. Katika hao watu huko Mbinguni kulikua na Wazee, Vijana na Watoto ama wote walikua katika rika moja?

Asante Mtumishi, ni katika tu kujifunza.
 
Back
Top Bottom