Ulivyorahisisha mambo sasa utadhani wewe ndio muumba mwenyewe, katika ukafiri mkubwa ni mtu kupinga jambo la kufufuliwa na huu ni upagani wa wazi, hivi ninyi vichwa vyenu mnavitumia kufanyaje? haufikirii mambo yote yalivyopangwa kwa ustadi wa hali ya juu? hautizami watu wanavyokuja na kuondoka? hauzingatii wengine wanavyodhulumu wenzao?.
Unataraji hayo yatapita burebure? acha kujipa moyo kwenye hamna mkuu, utatumia muda wako na ukifika wakati unaondoka kwenda kulekule walipo wenzako, huko wanaposubiri tukamilike wote kisha siku ya mwisho ifike na hukmu ipite na kila mmoja alipwe kwa kile alichokifanya.
"Wamedai wale waliokufuru ya kwamba hawatofufuliwa, sema: kwanini msifufuliwe!? ninaapa kwa mola wangu! hapana shaka mtafufuliwa na kisha hapana shaka mtaambiwa {yote} mliyoyatenda, na hayo kwa allah ni mepesi".
Qur'an 64:7
Jiandae na kifo chako mkuu, kikifika hicho ndio kiama chako kidogo kisha kufufuliwa ndio kiama chenyewe, na si busara kujipa matumaini kwenye hamna, no where to run.