Mbingu ni kweli ipo na huu ni ushuhuda wangu binafsi

ulisema ulikuta mbinguni wanaimba je ilitumika lugha gani huko..?
Mtu awapo katika Ulimwengu wa Roho hakuna limit juu ya uelewa wa lugha.

Limits zipo uwapo katika Mwili. Mtu aliyejazwa Roho mtakatifu anaweza kuongea Kwa kijerumani, kichina, kiarabunj bila kuzisomea darasani. Au akaongea lugha za Malaika na za Mbinguni bila kufundishwa sababu Roho ya mtu asili yake ni MBINGUNI.

Mtu aliyepagawa na Pepo anaweza kuongea kiarabu au kiswahili bila kusomea, na Kila siku tunashuhudia wakiongea. Lakini ukimwambia kuwa mtu aweza enda Mbinguni na kuongea lugha za Mbinguni au akajazwa Roho mtakatifu na kusema lugha za Malaika watabisha.

Ni ngumu mtu wa mwilini chini na mtu wa Rohoni Kutoka JUU kuelewana.
 
1. Lugha ya Wimbo. Kiswahili Bwana Mungu nashangaa kabisa. Ulimwengu wa Roho hauna limitation ya Lugha na ndio maana mitume walisikika wakiongea Lugha mbalimbali kwenye kitabu cha Matendo ya Mitume ile sura ya Pili.

2. Aliniongelesha kiswahili kama nikivyoeleza hapo juu. Aliniambia, nimetumwa kukuchukua.

3. Malaika alikuwa na sura ya muonekano wa kibinadamu huku sura yake ikingaa sana kama mwanga wa jua.

4. Walikuwa wanangaa kwa nuru kwenye nyuso zao na huwezi tofautisha race zao huku wamevaa mavazi meupe na yanayong'ara. Wote walikuwa ni wa rika moja vijana wasio wanene wala wembamba na wanaonekana kama vijana wenye umri kati ya 20-30.

Nawasilisha.
 
Amina ubarikiwe Mjoli wa Bwana.
 
Na hayo uliyo orodhesha hapo ndio Yana dhibitisha hakuna Mungu muweza wa vyote. Angelikuepo hayo yasinge tokea
 
Na hayo uliyo orodhesha hapo ndio Yana dhibitisha hakuna Mungu muweza wa vyote. Angelikuepo hayo yasinge tokea
Kwamba ili awepo ni mpaka aendane na akili yako, kwani ulipokuwa unazaliwa uliambiwa hapa ni peponi mkuu? lazima usote na mara nyingine uneemeke.
 
Kwamba ili awepo ni mpaka aendane na akili yako, kwani ulipokuwa unazaliwa uliambiwa hapa ni peponi mkuu? lazima usote na mara nyingine uneemeke.
Mungu hayupo ndio maana Kuna mateso chuki njaa Vita na mengine mengi Ange kuepo hivyo visinge wezekana. Au labda alishakufa ndio maana Mambo yanaenda randamli
 
Mungu hayupo ndio maana Kuna mateso chuki njaa Vita na mengine mengi Ange kuepo hivyo visinge wezekana. Au labda alishakufa ndio maana Mambo yanaenda randamli
"Hapana shaka tutakujaribuni kwa kitu katika khofu, na njaa, na upungufu wa mali na watu na matunda, na wape bishara njema wanaofanya subra."

Qur'an 2:155
 
"Hapana shaka tutakujaribuni kwa kitu katika khofu, na njaa, na upungufu wa mali na watu na matunda, na wape bishara njema wanaofanya subra."

Qur'an 2:155
Ili kua mfuasi wa hizi Imani inabidi uwe mjinga sana. Sasa mnasema Mungu Ni mjuzi wa yote, Ina maana matokeo ya jaribu teyari anayo. Sasa anakujaribu ili agundue nini? Maana kwa uwezo wake tayari ameshajua matokeo kabla ya mtihani
 
Mbinguni ni wazo lipo kichwani tu, hakuna uhalisia. Ukipata raha ni mbinguni na ukipata shida upo motoni. Ni maisha tu ya hapa duniani, ukifa ndio kupotea tu kama inzi.
 
Utukufu kwa BWANA!
 
"Kigogo" mmoja (simkumbuki jina) aliazimia kuziteketeza Biblia zote, kipindi hicho kabla teknolojia ya uchapaji haijagunduliwa. Lakini alikufa akaziacha Biblia zikiwa "hai", na baadaye nyumba yake iligeuzwa kuwa kiwanda cha kuchapia Biblia.
 
Amen kuubwa mimi naamini haya hata kama nitabaki peke yangu nitaamini tu. Japo mi ni mwenye dhambi BWANA UNIREHEMU BWANA UNIREHEMU kuna dhambi moja inanitesa sn ninashindwa kuiacha kbs bt sku nikfanikiwa takuwa mwenye nguvu sn ulimwengu wa roho.
 
Bro tuna mambo genuine ya kufikiria. Peleka mazingaombwe yako shule ya maingi huko. Tuache tuishi uhalisia
Mungu wa mbinguni yupo na ataendelea kuwepo na kujifunua kwa watu wake kwa namna na jinsi impendezavyo. Pia kuamini au kutoamini kwangu juu ya uwepo wake hakumfanyi Mungu kutokuwepo maana yeye haitaji uthibitisho wa mwanadamu ili ajulikane yupo. Yeye ni wa milele na ataendelea kuwepo. Mwana kondoo ameshinda tumfuate.
 
Hii ilikutokea ndugu mwenye hii Id au ume copy maelezo ya mtu ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…