Umeeleza vizuri,Suala la kwenda Mbinguni kwa mkristo wala sio la kushangaa,tatizo kuna watu wakisika mtu kaenda mbinguni wanaanza kuwaza kama wao kwamba mtu kavaa mkanda nje na viatu na begi lake anasubiri basi la kumpaisha ndio maana anaona ni kitu kisichowezekana.
Kupelekwa mbinguni,inatoka roho yako ambayo ndio imevalishwa huu mwili,unaacha mwili wako kitandani unauona,au vinginevyo unapewa maono ya namna mbingu ilivyo.
Sasa wasio mjua Mungu wataelewa nini,ogopa sana jambo usilo lijua akaja mtu kutaka kukuaminisha ,kuishi maisha ya neema na kumjua Mungu si watu wote walio jaaliwa.
Ingawa kumekuwa na mafundisho mengi ya kumwelekea Mungu lakini ni wachache mno wanao yajali na hata kuyaelewa na kufuaata yasemavyo.
Enzi za zamani kumjua Mungu ilikuwa ni siri nzito na ilikuwa ni baadhi ya familia tu zinazo mjua na kumtumikia mwenyezi Mungu,wengine wengi walikuwa wakiponda anasa na mambo machafu wakati wote wala hawakutambua uwepo wake ,na wengine wale wenye kutambua kwa kiasi waliishia kupuuzia tu,Maandiko yapo wazi juu ya hili.
Mtu awaye yote asiye kuwa karibu na Mungu na wala asiye jishughurisha naye hawezi kumuelewa mtoa mada,Kuna watu wapo deep sana katika imani.
Mnatakiwa mueelewe kwanza neno imani.
Ili kitu kitendeke lazima kwanza uamini.
Usipo kuwa na imani, wewe utaishia kufanya mambo madogo madogo tu ya kidunia ambayo kila mtu anauwezo wa kufanya ,utaota ndoto za kushiba na kupandishwa vyeo makazin au kuota una kula tunda kimasihara
Dunia ina mambo mengi ,unaweza ukajua baadhi ya mambo na ukazani umeimaliza kumbe hakuna kitu unajua.
Mimi nimekaa na watu walio jikita kwenye imani hadi nikaona kama wanaigiza kumbe ndo maisha yao.Wewe unae ishi kidunia mambo ya imani ni nini kushughurika nayo? na kwa sababu ipi ujue nani alienda wapi na akarudi ? Ya kazi gani sasa ! Hata ukiamini au usipo amini itakusaidia nini,si kujichosha bure huko!
Ya ngoswe muachie ngoswe ,wewe agiza bapa kubwa tupige ,tushushie na yule asiye pendwa na wale watu .
Imani ni siri ,siri hufichwa ,ni sawa na uchawi ,watu huamini upo na wengine kata kata hukataa,ndivyo ilivyo .Kukubali au kukataa jambo haiondoi uhalisia wa uwepo wake au kutokuwepo kwake.
Imani ni mlango unao ingiza nguvu ndani yako na hata kujua au kuona na hata kutenda mambo mageni au yasiyo ya kawaida kwa mwanadamu.
Mimi nina imani na ninaamini katika kile mtu anachoeleza mana nina imani ya kwamba lolote linawezekana.
Kwa mfano katika mambo mengi ya wazi wanayo fanya watu yanayo husu imani ni uchawi,uchawi ni vilahisi zaidi kuuona ama kuushuhudia kazi zake,japo hufichwa ila ni rahisi sana kuziona kazi zake katika mazingira tofauti tofauti.
Ili uchawi ufanye kazi lazima imani itumike na ihusike.Jambo lolote ukitaka ulifahamu vyema basi jitahidi kushiriki pamoja na washirika wake.Ukitaka kuijua imani yoyote kaa na watu wa umani hiyo.
Mfano sisi sote tumesoma ,na hapo mwanzo angali tupo wadogo tulikuwa hatujui chochote kuhusu elimu ,iwe kusoma au kuandika,tulihangaika sana kuumba herufi moja moja tu,yaani hata kuandika herufi 'a' kwetu ilikuwa mtihani.
Ila taratibu tukaja jikuta tunaweza kusomewa imla na tukaandika vyema na kukokotoa hesabu matata vyema kabisa.Leo hii tusingejifunza kuandika na kusoma si tungeona ni mambo yasiyo wezekana aslani .
Basi chochote na lolote linawezekana ingali tukiwa hai hapa tuniani.
Basi tambua jambo lolote usilo lijua ,uambiwapo lipo au hutokea ingawa wewe hujawahi shuhudia ama kuona usiwe mwepesi wa kubisha tu ,maana mengi bado huyajui hata ukiwa na phd yako,wewe bado tu ,unaweza ukayaona na kuyajua yanayo onekana kwa macho ya mwilini tu ila yale yasiyo onekana kwa macho ya mwilini usiyajue.
Basi tuamini kwa kuona au kusikia na hata tusipo ona ama kusikia twaamini mana tunayo imani na ishara zatuijia .