Mbingu ni kweli ipo na huu ni ushuhuda wangu binafsi

Nilipolala kama saa 12 alfajiri nikaona Malaika mmoja aliye kama mwanadamu amevaa mavazi meupe yenye kung'ara huku akiwa mwenye sura inayong'ara
😁😁😁 Ina maana malaika alivaa nguo gani? Jinsi kali na koti jeupe la Gucci? Chini alivaa yeboyebo nyeupe au buti?
 
😁😁😁 Ina maana malaika alivaa nguo gani? Jinsi kali na koti jeupe la Gucci? Chini alivaa yeboyebo nyeupe au buti?
Wacha weeew, mawakala mnajitahidi kunivunja moyo kwa kuniandikia ujinga na makwazo ila hamtaniweza.
 
Wacha weewwee.
 
Ni level ya juu sana huwezi elewa, kuna utaratibu kwa kila. Jambo, uwepo wa mbingu, haihalalishi Mwakasege kuenda, utaratibu wa maandiko ndo jambo la msingi.

Dubai ipo, ila kwenda ni uataribu.... Wewe ni fala kabisa
Hahaaaaaa, naona unatukana.
 
Unaleta habari za ndoto alafu unaita watu wapumbavu? Mbona wewe ndo unaonekana kiongozi mwandamizi wa wapumbavu!
 
Mimi nawashangaa sana walokole wa Africa. Hivi nyie mnamjua Mungu kuliko wale walioletea hizo habari za huyo Mungu. Mbona wazungu hawana utaaahira wa dini kama nyie na wao ndo wamewaletea. Mbona wao hawaoteshwi ndoto na kufungua Makanisa kama ilivyo huku kwetu kila kona kanisa, kila nyumba nabii

Ogopa sana mtu akiku-Brainwash na kukukamata kupitia imani unakuwa zezeta pro max
 
Asante kwa ushuhuda wako wenye nguvu Mtumishi. Ubarikiwe sana!
 
Walokole mna matatizo sana,,,huko ulipoenda hukuona malaika weusi wanaong'aa na waliovaa nguo nyeusi za kung'aa??
 
Kwa hyo biblia inapoeleza kila jicho ltamwona wewe unapingana nayo, bro hizo ni ndoto tuu habar za kupaa angani huwaga naota sana hta mm,, bt usihusishe na maswala ya kiimani, ni ktokana na mazungumzo na shughuli zako za mchana na shibe pia style ya kulala. Hakuna YESU atakaenokana kwa mtu mmoja na maandko hayohayo yameonya tusimwamini mtu wa hvo kama wewe apo, kasome ;

Ufunuo wa Yohana 1:7
[7]Tazama, yuaja na mawingu; na kila jicho litamwona, na hao waliomchoma; na kabila zote za dunia wataomboleza kwa ajili yake. Naam. Amina.

Marko 13:21-23
[21]Na wakati huo mtu akiwaambia, Tazama, Kristo yupo hapa, au yuko kule, msisadiki;
[22]kwa maana wataondoka Makristo wa uongo, na manabii wa uongo, watatoa ishara na maajabu, wapate kuwadanganya, kama yamkini, hata hao wateule.
[23]Bali ninyi jihadharini; nimekwisha kuwaonya yote mbele.
 
Imani bwana,

Mwenzako zumaridi ana matatizo ya akili ila wew mzima yani unajiona wew upo sahihi sana kusema kwamba ulifika mbinguni ila zumaridi muongo alafu mbinguni ulienda ukaimba na kurudi tu.

Enh tueleze kidogo hao mliokuwa mnaimba pamoja na wametoka duniani au wenyew in Wakazi wa huko.
 
Mkuu fanya evaluation ya afya ya akili seriously. Na huyo mnyama ulimuona huko?
 
Ndoto kama hizo kila mtu ameota, na uzuri hakuna ambaye hajawahi kuwa warrior kwenye hizo ndoto.

Nishaota ndoto nikiwa superman na fly kwenye highest roof na shuka langu, hiyo yote kwasababu ya Marvel movies

Wewe umeota ya kupaa mbinguni kwasababu ya ufunuo wa Yohana

Wakati nipo mdogo nilipoangalia filamu ya Yesu kwa mara ya kwanza nilipata emotions nikalia, usiku nikapata nightmare niko Yerusalem.

Kitu ambacho kina spin kwenye ubongo wako ndio hicho hicho utachoenda kukiota.

Nje na hapo hizo ni Polimilai
 
Mkuu
Hakika ninaamini usemayo.

Kuna mambo fulani yalinitokea maishani ambapo naamini Mungu ni mkuu, yupo na mbingu ipo.

Ulichokiona ninashuhudiwa hapa kuwa ni kweli.

Mengine nisiyaseme sana maana muda na wasaa utakuja nitasema
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…