Mbingu ni kweli ipo na huu ni ushuhuda wangu binafsi

Imani na mambo yake huwa hayaeleweki kwa ufahamu wa kawaida...
 
Hongera kwa comment, comment yako ni muhimu sana humu JF.
 
Mambo ya Imani ni magumu sana.

Sisi wa afrika tunahitaji uponyaji wa Fikra zetu.

Babu wa kizungu tuliambiwa ni Mtakatifu akikutokea ni sawa.

Lakini babu yangu mwafrika akifa anakuwa mzimu.

Waafrika tuamke turudi kwenye asili yetu.
Hakuna sehemu niliposema kuwa Babu wa kizungu amenitokea na nikamuita Mtakatifu. Hayo ni yako mkuu. Kuhusu Babu yako muafrika kufa na kuitwa Mzimu ni wao wenyewe wanajiita hivyo. Mara nyingi mapepo yakipanda huwa wanasema wao ni mizimu na hata waganha wa kienyeji huwa wanayaita mamizimu ya Babu yako au mababu yao kuyauliza so hakuna sehemu toka nianze kusoma Biblia imeandikwa mababu wa waafrika ni mizimu.

Pole kwa hilo mkuu.
 
Sorry naomba kuuliza unasema ulipofika mbinguni ukakutana na wengine mkaimba wimbo wa β€œbwana Mungu nashangaa kabisa”

Je huko ni lugha ya kiswahili pekee unatumika? Au sehemu ulipelekwa ni mbingu wako wanaojua kiswahili pekee!?

Asante
Mungu ni Mungu wa Lugha na Makabila. Biblia inasema yeye ndiye muanzilishi wa lugha kwani ndiye aliyemuumba Adam na akawa anaonhea naye na pia ndiye aliyewapa usemi Mpya akona Nimrod pale Babeli kwa hiyo ili umuelewe kile anachosema nawe, ataongea nawe kwa lugha mama yako.

Asingeongea nami kiarabu au Kimasai wakati sikijui. Ufunuo kuhusu huo wimbo wa Tenzi ulifunuliwa kwangu kwa Kiswahili na inawezekana Mzungu naye angefunuliwa kwa kiingereza na sio Kigogo ila lugha yake mama mkuu wangu.
 
Amina, Mungu akutie nguvu na akutane na haja ya Moyo wako. Watu wanashindwa kujua kuwa hatumuabudu Mungu mfu ila tunamuabudu Mungu aliye hai na anayesema nasi kila iitwapo leo. Yeye ni muaminifu na kama tutamtafuta kwa nia na mioyo yetu yote, atatufunulia siri za Mbinguni na kutujaza na baraka zake.
 
In sha Allah ngoja na muislamu aje hapa atueleze habari za kimataifa kuhusu mbingu
Hao hawana Mbingu ila wana Pepo. Pepo yao hata wewe umeshawahi kuiona, kwa maana pepo yao kulingana na Quran ipo............
 
Nimecheka sana 😊😊😊
 
Hongera kwa comment yako, tumeithamini sana hii mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…