Nikinukuu mada ya mdau Synthesizer (Quote):
"Kuna account humu JF zimefunguliwa na watawala kwa ajili ya kutumiwa na group la watu wanaolipwa kwa ajili ya kujibu kukosoa kukejeli nk... Mwanshambwa sijui Tlaatlaah nk sio mtu mmoja. Ni watu kadhaa wanaolipwa na wameambiwa watumie
Kama unataka kulinda hadhi ya jukwaa letu na unataka tubaki na mijadala yenye afya kuhusu nchi yetu, fanya maamuzi haya leo. Kila ukiona akaunti yenye sifa hizi, usipoteze sekunde yako kuwajibu—bofya Ignore, kisha pita hivi!
Wakikosa watu wa kuwabishia na kuwapa kiki, mradi wao utakufa wenyewe na mabosi wao wataona hawana faida tena. Sisi ndio wenye jukwaa hili, tulilinde!