Extrovert
JF-Expert Member
- Feb 29, 2016
- 70,785
- 186,690
Bora mkuu maana angemaliza chuo bila utashi wa kujichanganya ujue angekuwa mwanao hapo home mpaka unafikisha miaka 70 unae tu, maanake angekuwa muoga sana kuanza maisha ya kujitegemea ile fighting spirit ambayo watoto wa mbwa wengi huwa wanakuwa nayo mapema tu on their late teens angekuwa hana.Nilistuka mapema sana juu ya madhara ya kusomesha watoto hizi private, unakuta mtoto anatoka saa 10 jioni, akitoka hapo ni tuition, akitoka hapo ni homework na wengi hawatoki nje ni geti kali ni ndani tu hii inahirbu sana maisha ya mtoto.
Pia Malezi ya siku hizi pia yamechangia mno kuwafanya watoto wawe mazube maana watoto ni kuwafuga kama kuku ndani ya mageti (geti kali) huku wazazi wengi wakijidanganya kwamba wanapata furaha kamili kwa katuni na kunanunulia games.
Nakumbuka zamani tukitoka shule tulikua hatukai ndani ucheza games au kuangalia katuni, Tulikua na vikundi vya watoto mitaani tunacheza mpira, kuogelea na hata kujifunza kuto onewa hovyo hovyo, dada zetu walicheza rede, kupika, n.k Hii michezo na maisha haya yalifanya tujue kuishi na jamii tofauti na siku hizi unakuta litoto linachojua na games, katuni na what is water. ukimpeleka huyu mtoto nje kuna uwezekano mkubwa wa yeye kuonewa na hata kuwa mpweke asiwe na marafiki maana hajui ku interact na watu (Hili tatizo ni kubwa ulaya).
Binafsi mtoto wangu wa kiume namsomesha english medium hizi, mara ya kwanza shule niliyompeleka walikua darasani 18 tu na wanatoka saa kumi, kwa huu uchache nakumbuka alikuwa ana rafiki moja tu na muda mwingi ulikuwa ni kusoma hadi saa kumi.
nikaona huu upuuzi sasa, shule ndio ni muhimu ila sio kila kitu kwa mtoto wangu kuna maisha mengi mno anayopaswa kujifunza, Nikamwamishia shule ambayo wapo 48 darasani na wanatoka saa saba na nusu ila tu darasa la saba tu ndio wanatoka saa tisa. Yeye yupo darasa la tatu shuleni huwa yumo kumi bora na hii inatosha kwangu siamini sana mambo ya kuwa wa kwanza.
akitoka shuleni anakula, anafua nguo zake, Zamani nilikuwa nimempiga geti kali ila baada ya hapo nikaanzisha utaratibu anapelekwa nje kidogo ya mjini kwa bibi yake ambako hucheza na wenzake, kulima, kuogelea mtoni, kuwinda, n.k anaenda huko kwa sababu hapa mjini watoto wengi ni mageti kali wapo ndani.
Siku hizi kawa muongeaji mno nlivyomwanzishia huu utaratibu, Kawa mjanja, Shuleni kwao kageuka kuwa aina ile ya mwanafuzni darasani ambae kila mwanafunzi anataka kuwa rafiki yake na nadhani hii ni kwasababu huwa anawapa stori ama kuwafundisha wenzake vitu alivyofundishwa au alivyofanya huko kwa bibi yake,
Shule aliyopo ni yeye peke yake anaweza kuruka zile sarakasi za nyuma basi wenzake wanamkubali sana,
Nimeiwa shuleni kwa kesi za utundu utundu huu wa wavulana kama kupiga kelele na kutania wenzake (kesi 1 mwenzake kesi 2 wasichana) Binafsi ndivyo navyotaka awe mchangamfu na nikiri tu nilifurahi hizi kesi japo nilimkjanya kwa shingo upande, Sitaki mtoto azubae zubae
Sijamlipia school bus kwa maksudi kabisa japo nina uwezo, nilishangaa aliponiambia wenzake pia shuleni wanapenda sana wawe wanatembea kama yeye pamoja na wenzake wawili ambao hawajalipiwa school bus 🙂🙂
Ni hayo tu, Nawaonea huruma wazazi ambao huipa shule kipaumbele mno na kuwafungia watoto wao nyumbani, Matokeo yake mtoto anakuwa hana social skills, anakua anaonewa kirahisi, hafanyi mazoezi hata ya kuimarisha miguu kwasababu ya school bus, anakuwa yupo yupo tu kichwani anajua games na katuni tu.
Binafsi hio kitu imenitesa sana maana mi nimelelewa maisha ya geti kali from Standard 1 to O'level hapo form 2 naishi maisha ya Imla tu na kutii utawala wa wazazi. Nikahamishiwa boarding uboyzini form 3-4 walau nikawa exposed japo nilikuwa bonge la boya. Nimemaliza form 4 sina confidence hata ya kumsimamisha demu na kumpa madini japo nilikuwa nawatamani sana. Simu ya kuongea na demu simalizi dk 2 ashakatisha maana sina story kabisa was too fucking boring.
Ila sasa baada ya kutoka kifungoni toka nimeingia life la chuo nikamix na la mtaa ilikuwa hatari sana. Nikateswa na mapenzi nikapona sahii mi ni mdeadly! Neno moja naweza sema ni "Cuff yo chick!"🤣🤣🤣