Mbinu nayotumia kumlea mwanangu anayesoma private awe mjanja, awe na furaha, asigeuke kuwa kuku wa kisasa

Thread closed
 
Mlee mwanao katika njia impasayo nae hataiacha hata atakapokua mzee!!
Kila mtu amlee mwanae kwa uwezo wake na katika njia atakayoona inafaa!! Chonde chonde kwa wale tuliotoka lower & middle class families tujitahd watoto wetu wawe aware na changamoto za maisha zinazoweza kumkumba pale maisha yakibadilika
 
Wewe umeandika false. Mimi naishi uswahilini najua tabia za huku. Nimeamua kujitenga na hii jamii kwani inaharibu hasa watoto.
Mimi najifungia ndani sio mtundu sio mcheshi na ni mpole kupitiliza.
Na nimesoma shule ya watukutu na hakuna aliyejaribu kuleta utani Wala kunionea na wananiogopa sababu najitambua na kujiamini. Wajinga wote wananiogopa na kuniheshimu shule na mtaani.

Watu wa mitaani hawana adabu hawana heshima. Matusi na ngono ndicho wanachofikiria muda wote.
Watoto wa age yangu wana uwezo mdogo sana wa maono na maoni wala hawana uwezo wa kufikiria.
Wao wanawake na ngono ndo mawazo yao.
Hawajui nini kinaendelea nchini wala future plans yaani ni vilaza.
Watoto wadogo wa miaka 5n6 wanafikiria ngono pia na kutukanana matusi ya mama. Na shule nako hivyohivyo. Na wewe sikulaumu sababu ni zao la hao watu.

Wazazi wao na mtaa mzima kutukana ku....Nina ni kawaida. Wivu uchoyo chuki matusi kama unayotukana wewe na majungu ndo maisha yao.
Na wewe sikulaumu sababu ni zao la hiyo jamii. Ndo maana badala ya kujibu hoja unashusha matusi.

Hizo perspective zako baki nazo kufa nazo mwenyewe. Wewe umenizidi umri lakini ni mjinga.
Hao wanaokubaliana na wewe wote ndo zao la hizo jamii mbovu za kiafrica. Ndo hawa wanasoma ili wapate ajira. Hii inachochea umasikini Africa. Huruma.
 
Hongera kuwa mmoja wa wazazi wachache wenye kujua siri hii. Wazazi wengi tumeiga malezi ya ulaya...na kusahau kuwa ubunifu, uvumilivu, mahusiano, na kujitambua havigundishwi darasani na hata vikifundishwa havina tija bila kufanyia mazoezi. Watoto wengi wa english medium..zao ni katooni na kizungu. Anaongea vizuri ila hana ubunifu wala mahusiano mazuri na wenzie. Watoto kama wako..anajifunza mengi anaposhirikiana na vijana wa mtaani kwa bibi..mbali na kupiga sarakasi..ila kuhusiana na wenzie..kuwa mvumilivu pale anapokwazana na wenzio.

Mimi ningekuwa raisi..ningefumua huu mgumo wa maisha..na kulaImisha shule zote za private na public kufanya masomo ya michezo na sayaskimu..angalau watoto wachangamke!
 
Hio elimu ya darasani tunato wengi tu na wengine tumefika vyuo vikuu, ni elimu ambayo inatusaidia kuajiriwa tu, ndio maana kuna wanaofoji vyeti na wanafanya kazi bila kugundulika.

Wengi humu wanadhani simwi mtoto vizuri lakini wanasahau anaeacha asili ni mjinga, Siwezi kumlea mtoto wa kiume kimayai mayai eti nimlipie school bus utafkiri ni kilema ama yeye sio kama wenzake weliojazana shule za kata wanaotembea kwa miguu bila matatizo.

Siwezi kumzuia asicheze nje maana hii dunia ni ya watu, watu hawakwepeki, inabidi ajifunze social skills ku interact na wenzie, kuna vitu kama kukaribisha wenzako unapokula, kugawana na wenzako chakula,n.k kajifunza huko.

pia ujanja ujanja nao ni muhimu, mambo ya kuonewa sina stress nayo tena, mtoto wa kiume ukipigwa rudishia sio kuja kwangu unalia "baba nimepigwa", kuna kesi nillitwa shuleni huko mtoto wa darasa la juu yake walipigana, mimi nikaona ndivyo inavyotakiwa sio kuitwa huko shuleni kwamba anaonewa.

Pia maisha ni connection. hii inabidi mtoto awe na marafiki pande nyingi nyingi huku mimi nikiwa na analyze.
 
sawa endelea kujifungiaga ndani
 
Hao kuku wa kisasa unawaona hapo mitaani wakivuta bangi??....hayo mawazo ya kimasikini tu hakuna chochote cha msingi.....umeona wapi mtoto wa bakhressa anacheza na mitoto mihuni ya kiswahili inayovuta weed?..... umeandika pumbapoint...
 
Pumba hizi unadhani wote wanasoma ili waajiriwe....
Sio kila asili ni ya kugezwa dunia inabadilika kila kitu ni tech wewe bado unakazana na ukuti..
Sitoshangaa ukisema ukeketaji ni lazima...god what's wrong with Africans mind?..... pathetic...
 
mwanae anaruka salakasi za kinyume nyume!

hivi ukiruka salakasi za kinyume nyume ni moja ya social skills??

mwanae sasahiv amepata vikesi viwili vitatu huko shuleni

kumbe kupata vikesi viwili vitatu ni moja ya social skills?!
Mkuu jitahidi kujifunza kucheza na ujumbe uliofichika kwenye maneno.
 
Nimepapenda hapo pa kutania wasichana hili ni jambo la vizazi na vizazi,miaka nenda miaka rudi, hivi kwanini wasichana hawawatanii wavulana,bali wavulana wanawatania wasichana,wasichana huwa hawana Interest na utani au?
 

Uko vizuri.
 
Nakukubali sana Chief

ุจุงุฑูƒ ุงู„ู„ู‡ ููŠูƒ ุฃูŠู†ู…ุง ูƒู†ุช
 
Nzuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ