Mbinu watumiazo Mafundi Ujenzi kuibia mabosi zao

Wanatia hasara sana unaweza ua mtu, kuna jirani ghorofa lake walimchakachua vibaya mno ile wanajiandaa kumwaga jamvi la kwanza mvua moja tu nalo likapiga chini.......mbona aliwachomolea bastola walipoteana
 
Kuna jamaa alikuwa anafatua tofari,ila kabla ya kwenda kazini alikuwa anachanganya mchanga na sement yote harafu ndio anawaachia mafundi akijua amewakomesha,kumbe wale walikuwa wanachukua mchanga uleule wanapeleka sehemu nyingine
 
Lakini pia mafundi nao wanadhulumiwa kwa namna moja ama nyingine kupitia malipo duni wapewapo kazi na wateja wao! NAni atawatetea labda.
 
Hivi mnawachukuliaje mafendi eti?
Kwa nini msijenge wenyewe ikiwa mafundi si kitu kwenu?
Pole kwa kukwazika mkuu, tena niwie radhi sana isee.

Mjadala uliopo hapa ni kupeana mbinu na uzoefu kwa ajili ya kuzuia wizi ufanywao na mafundi na si kudhalilisha fani ya ufundi hapana.
Kwa hiyo katika maelezo yangu naomba usinitafsiri vibaya.
Hivi mnawachukuliaje mafendi eti?
Kwa nini msijenge wenyewe ikiwa mafundi si kitu kwenu?
 
Njia nyepesi ya kumpata boss mjuaji. Mfano ww ni mpaka rangi, usiwe na haraka. Hakikisha unajenga uteja dukani. Mpange muuzaji kwanza kuhusu huo mchongo.
Mfano zinahitajika ndoo 6 za weather gurd. Andaa ndoo moja tupu safi, ijaze maji then ipeleke pale shop km bosheni. Siku ya kwenda kununua nenda nae boss wako na usiwe na haraka.
Pakia ndoo hizo peleka site, shusha mzigo then rudi shop uchukue chako. Easy like that.
 
usije mwaga ubongo wa mtu tukusome magazetini mbinu ni kusimamia tu kikamilifu, ukubali kupigwa kidogo

Hivi hakuna kampuni zilizosajiliwa rasmi kusimamia shughuli za ujenzi? Hii ni fursa nzuri sana basi tukutoaminiana
Kupigwa ni lazima. Hizi mbinu nyingi wanatumia haswa kwa wanaofanya ujenzi kwa mara ya kwanza. Usikubali kufanya manunuzi maduka anayoshauri fundi. Lakini umakini mkubwa unahitajika kwenye manunuzi ya vifaa vya umeme. Hapa ndiyo unapigwa vibaya. Mimi nililetewa Main Switch ya laki 3 wakati dukani nimelipia Main Switch ya laki 8. Hii nilikuja kugundua baadaye sana baada y kucheki bei ya Main Switc niliyoletewa.
 
Kwenye hii thread tutakuwa tuna share Mbinu za wizi za mafundi ujenzi ili kusaidia wale wanaotaka kujenga "wasipigwe ".

Wengi tumepigwa sana hadi kuzijua hizi mbinu.

Karibuni.
Ngoja niweke Kambi hapa.
 
Hakuna baraka, ndiyo maana asilimia kubwa hubaki kwenye level hiyohiyo ya maisha miaka nenda rudi.
 
 
Cement ya elfu 14-15 umeipata wapi mkuu? Inaweza kuwa magendo hiyo. Bei aliyokutajia fundi wako ni sahihi kwa hali ya soko ya sasa.

Kuna umuhimu pia wa kujenga uhusiano mzuri na fundi ambao ndio utakuwa msingi wa uaminifu.
 
Hii ndiyo shida ya kutoaminiana!

Uzi Mzima hakuna anayeongelea Contract na BoQ wote tunataka mteremko!
Fundi anayejielewa atakwambia muanze na contract ili iwabane wote, Yeye na Wewe! Just a simple contract kwa hawa mafundi wa uswahilini.
Secondly fundi aliyefocus kwenye kazi hata deal na Materials na Management yake hiyo atamwachia Client maana mwisho wa siku anaweza kugeuka Mlinzi wa vifaa na si Fundi tena!
Katika Suala la Ujenzi vitu vya Msingi ni Vitatu, TIME, QUALITY na COST na hivi huwezi kuvifikia mwenyewe pasipo kushirikiana na Fundi!
Finally, kama huna ABCs za mambo ya Ujenzi tafuta mjuzi atakayekushauri na kukupa mwongozo tuachane na hii tabia ya kudhani tunajua kila kitu.
Huku kwenye mitandao mafundi wa kweli ni wachache kuliko matapeli. Reference ya Fundi ni MUHIMU SANA
 
Umesema sahihi Mkuu

Nadhani ni Wenye nyumba wachache wanaofunga mikataba na Mafundi wao

Mara zote, Mafundi wameonekana sio waaminifu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…