Mbinu za kuchukua namba ya Simu katika Mazingira Magumu

Na sisi tunapita nao tu jumla jumla..
 
...endelea bc mkuu stor ya part 2 episode 3 baada ya jamaa ako kuwaelekeza unapoishi
 
Ilikuwaje..
Huyo demu ana private company anamiliki, surprisingly that very day tulikuwa tunakunywa same drink na yeye tofauti na wengine, japo mimi nilimpenda dogodogo meza hio hio kumbe dogo dogo ni demu wa mmoja wa masela wale, lugha ya macho na uvaaji wangu kibonge akapenda nikamchana kwa ushangiliaji wa Gabriel Jesus wa Arsenal mapema sana demu kaja mezani. Akanambia uko nice and you gotta guts nikamjibu my emotional capture is always my strength biologically. Namkula mpaka leo
 
Hahahaha kwamba.. "My emotional capture is always my strength biologically"
 
Muendelezo...:
Statics mawardat Rayns

Ilipita kama siku 3 bila mawasiliano yoyote baina yangu na yule Dada, nikawa naendelea na harakati zangu nipo job, nikakutana na Mwamba yule aliyenichomesha. Piga story mbili tatu akanielezea jinsi alivyotafutwa na hao waliojitambulisha kuwa ni Ndugu zangu.

Mie nikamwambia ni namna gani kaniharibia mambo yangu, na mbaya zaidi aliwaambia mpaka kazi yangu ni wapi exactly.

Basi, nikawa naishi kama Dididigi.., kazini full machale, home ndio kabisa nalala jicho moja lipo wazi.

Kuna siku nimetulia home ikaingia namba ngeni, nikapokea ni sauti ya kike, kumskiliza vizuri ni yule yule Manzi, akaniambia ile sio namba yake rasmi ni ya mtu wa ofisin kwake, amechukuliwa simu zake, gari mpk kadi za bank na mumewe.

Na yeye ndie anamfata kazini na kumpeleka, and akaniambia niwe makini maana mumewe si mtu mzuri, sasa nikamuuliza mumewe na mimi kuna connection gani hapo mpaka anitafute? Kwani mm na ww tunamahusiano yoyote? (Kumbuka hapo sijamtongoza wala kuweka ishu za mapenzi), yule Dada akasema analijua hilo ila kuna mtu aliwahi kumuona nae na kuna watu wanapeleka umbea yaan mambo mengi mie hata sikumwelewa. Nikakata simu.

Basi, ikabidi nikae chini nianze kutatua hii shida, nikaweka mikakati ya anonymity yaani ratiba na schedules zangu ni unpredictable, simu nikabadirisha pamoja na line. Ila nilichofanya ni kuiweka ile line yangu ya zamani ktk moderm. Kuna sayansi behind it.

Ni hivi Network protocols za Simu zipo same na za Moderm ndio maana tunapata sms na data. Ila calls huwa ni ngumu mara nyingi zinakuwa rejected au kuweka line busy. Pia traceability ni ndogo kunitafuta nipo wapi exactly itatuma taarifa ya mnara ila haitokupa pinpoint nipo wapi. Tofauti na simu ya kawaida yenyewe inabroadcast exactly upo wapi.

Tuendelee..

Pia nikaamua kuacha kazi kwa hiari. (Situation ilikuwa very worse nikawa sina AMANI), na baadhi ya watu wangu wa karibu hasa wanaonijua vzr niliwaambia nimepoteza simu so wawe makini kuna matepeli na vitu kama hivyo ili pia isije kutokea wakanichomesha zaidi.

Sasa, kuna siku ilikuwa weekend usiku kama saa 3 hivi, niliishiwa umeme na ktk simu hela sina nikaona nisogee mtaani kutafuta namna ya kusolve tatizo.

nilikaa kama nusu saa huko, wakati narudi niliona kama watu wawili, mmoja kavaa suti ya dark blue mwingine kavaa kanzu, huyu aliyevaa kanzu alikuwa anapiga picha pale napokaa na mazingira ya nje pale. Nikawaangalia baada ya kumaliza wakawa wanaongea na simu, sikuwasikia wanaongea nini. Nikajivuta pembeni nione vizuri hata sura.

Basi baada ya kumaliza kuongea na simu waligonga pale nje kama mara mbili tatu baada ya kuona kimya wakaanza kuchungulia madirishani huku wanazunguka zunguka nje.. sasa kuna gari ilikuwa inakuja upande wao nikaona wanatoka pale wanasogea barabarani (Walikuwa wanazuga) gari ikawapiga taa nikaona mmoja sura yake vizuri.

Yule mwingine aliyevaa kanzu sikumuona, gari ikanipita.. na wao hawakukaa sana waliondoka pale kwa kutembea kwa miguu kuelekea main road. Na mimi nikawafata mbele kidogo nikaona wamepanda kwenye pickup zile kama za police, na mule ndani kulikuwa na wengine kama watatu plus dereva jumla walikuwa kama 6.

Mie nikarudi kwa njia nyingine nikakaa nje kama masaa mawili nagombana na Mbu tu.. ndani hapakaliki, nje hapalaliki.

Mida kama ya saa 6 usiku nikaingia home, nikapanga vitu vyangu vya muhimu vizuri, kesho yake nikaita bajaji nikavihamisha kwa wazee, nikarudi kumtafuta Landlord nikaongea nae na kumwambia nina safari ya miezi kama minne sitakuwepo au kama ntakuja sitakaa zaidi ya siku mbili. Kodi imebakije? Akanitajia kodi imebaki miezi miwili. Nikamwambia sawa hamna neno, ila kama sitaonekana akae akijua nimesafiri au mtu yeyote akiniulizia awaambie nimesafiri, wapi? awaambie hajui.

Hivyo, so nilichokuwa nafanya ni kurudi usiku saaana na kuwahi kutoka. Nilikuwa naenda katika chuo kimoja (Sitakitaja Jina) kama part time Technician and tutor, nikitoka naenda kwenye ma bar au clubs mpk mida isogee ndio narudi. Yaan niliishi kwa wiki mbili mfululizo kama mwizi au jambazi anayesakwa.

Muda huo natafutwa na namba tofaut tofauti ikiwemo na yule Manzi pia, sasa nashindwa ku ignore namba ngeni. Kila ikiingia text kuna namna namuuliza aliyetuma jibu atakalonipa najua huyu ni fulani so tunaendelea kuchat maana kwa maongezi ya simu haiwezekani, line ipo kwenye moderm na natumia PC pale napokuwa nimetulia kama huko chuoni au nikijibana kwenye ki pub au Bar.

Itaendelea nikipata muda wa kuandika.. this time ni nani exactly huyo Mumewe, ni nani aliyekuwa anamtafuta. Na mimi ilikuwaje nikasolve hii ishu.
 
Dah karibu leo kwa neema sinza kwa ujumbe huu umefanikiwa rasmi kuingia kundi la mabaharia.
 
Umesakwa kama umegusa nyara za serikali vile
 
Hii Stori nzuri ya kuishi kama mwizi, irefushe kidogo mkuu [emoji3]
 

Dah kama movie vile .... tumalizie leo leo mkuu , usiache kiporo
 
Mwendlezo ety🙄
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…