Mbinu za kuchukua namba ya Simu katika Mazingira Magumu

Mbinu za kuchukua namba ya Simu katika Mazingira Magumu

Nikudondosha simu chini ya kiti na kujifanya unaitafuta unaomba Mlengwa simu yake mara Moja uibip kama umeibiwa,baada ya sekunde mbili unajisikia chini ya kiti wote Kwa pamoja wanaitikia haaaa kumbe uliangusha....Imeisha hiyo[emoji26][emoji26][emoji26]
[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji1787]
 
Part 2:
Nilikuwa Samaki Samaki pale Mlimani City.

Napiga maji, ghafla nikaona Chuma kikali sijapata kuona aisee ubaya alikuwa na Boyfriend/Mume wake.

Basi nikamlia timing wakati wa kwenda Washroom nimfate huko huko (Mazingira ya pale kwa upande wa Washroom kuna Distance kubwa).

Basi kweli bhana Manzi akajipindua kuelekea Washroom na mimi nikaunga Tela, tulivyokunja kona tu ya kuingia corridor la choooni nikamshtua, akasimama nikamwomba namba akasema yeye ameisahau kama vipi nimpe yangu, basi akanipa simu yake nimuandikie Namba yangu..

Kumbe nyuma Bwana ake anakuja na yeye tyr kashanipa simu yake ndio niandike namba nashangaa Manzi kageuka chap kakimbilia choo cha wanawake. Mie nikawa nimesimama tu sielewi nini kinaendelea ila kwa kuwa nimesoma CUBA sikugeuka ila nikapiga jicho kwenye kioo (Reflection) nikaona mjuba anakuja ila bahati nzuri na yeye alikuwa anatembea huku anachat so hakuona tukio la mbele.

Sasa simu ninayo ya yule Manzi namrudishiaje??.. [emoji1787]

Na jamaa kumbe alikuja kumsubir kule kule kwenye Corridor la Washroom ili arudi naye.

Mie nikajipindua Choo cha kiume kama Kawaida nikazuga zuga pale, Dem akatoka akanipa ishara ya nitulie huko huko.

Basi jamaa akarudi naye Mpaka walipokuwa wamekaa. Mie nikatoka baadae kurudi ktk meza yangu, nikamuita mhudumu mmoja hivi (Best yangu) nikamwambia nenda pale idondoshe hii simu miguuni (Mapajani) kwa yule Dada pale then uje kuna Zawadi yako hapa..

Mhudumu hakusita, alifanya hivyo na yule Dada aliiokota simu yake then.. tukaendelea kuwasiliana pale pale...

Huyu aliniletea shida sana.. mpaka nikawa naishi kama Mwizi.
Hyo story ya kuishi kama mwizi utusimulie ilikuwaje
 
Muendelezo...:
Statics mawardat Rayns

Ilipita kama siku 3 bila mawasiliano yoyote baina yangu na yule Dada, nikawa naendelea na harakati zangu nipo job, nikakutana na Mwamba yule aliyenichomesha. Piga story mbili tatu akanielezea jinsi alivyotafutwa na hao waliojitambulisha kuwa ni Ndugu zangu.

Mie nikamwambia ni namna gani kaniharibia mambo yangu, na mbaya zaidi aliwaambia mpaka kazi yangu ni wapi exactly.

Basi, nikawa naishi kama Dididigi.., kazini full machale, home ndio kabisa nalala jicho moja lipo wazi.

Kuna siku nimetulia home ikaingia namba ngeni, nikapokea ni sauti ya kike, kumskiliza vizuri ni yule yule Manzi, akaniambia ile sio namba yake rasmi ni ya mtu wa ofisin kwake, amechukuliwa simu zake, gari mpk kadi za bank na mumewe.

Na yeye ndie anamfata kazini na kumpeleka, and akaniambia niwe makini maana mumewe si mtu mzuri, sasa nikamuuliza mumewe na mimi kuna connection gani hapo mpaka anitafute? Kwani mm na ww tunamahusiano yoyote? (Kumbuka hapo sijamtongoza wala kuweka ishu za mapenzi), yule Dada akasema analijua hilo ila kuna mtu aliwahi kumuona nae na kuna watu wanapeleka umbea yaan mambo mengi mie hata sikumwelewa. Nikakata simu.

Basi, ikabidi nikae chini nianze kutatua hii shida, nikaweka mikakati ya anonymity yaani ratiba na schedules zangu ni unpredictable, simu nikabadirisha pamoja na line. Ila nilichofanya ni kuiweka ile line yangu ya zamani ktk moderm. Kuna sayansi behind it.

Ni hivi Network protocols za Simu zipo same na za Moderm ndio maana tunapata sms na data. Ila calls huwa ni ngumu mara nyingi zinakuwa rejected au kuweka line busy. Pia traceability ni ndogo kunitafuta nipo wapi exactly itatuma taarifa ya mnara ila haitokupa pinpoint nipo wapi. Tofauti na simu ya kawaida yenyewe inabroadcast exactly upo wapi.

Tuendelee..

Pia nikaamua kuacha kazi kwa hiari. (Situation ilikuwa very worse nikawa sina AMANI), na baadhi ya watu wangu wa karibu hasa wanaonijua vzr niliwaambia nimepoteza simu so wawe makini kuna matepeli na vitu kama hivyo ili pia isije kutokea wakanichomesha zaidi.

Sasa, kuna siku ilikuwa weekend usiku kama saa 3 hivi, niliishiwa umeme na ktk simu hela sina nikaona nisogee mtaani kutafuta namna ya kusolve tatizo.

nilikaa kama nusu saa huko, wakati narudi niliona kama watu wawili, mmoja kavaa suti ya dark blue mwingine kavaa kanzu, huyu aliyevaa kanzu alikuwa anapiga picha pale napokaa na mazingira ya nje pale. Nikawaangalia baada ya kumaliza wakawa wanaongea na simu, sikuwasikia wanaongea nini. Nikajivuta pembeni nione vizuri hata sura.

Basi baada ya kumaliza kuongea na simu waligonga pale nje kama mara mbili tatu baada ya kuona kimya wakaanza kuchungulia madirishani huku wanazunguka zunguka nje.. sasa kuna gari ilikuwa inakuja upande wao nikaona wanatoka pale wanasogea barabarani (Walikuwa wanazuga) gari ikawapiga taa nikaona mmoja sura yake vizuri.

Yule mwingine aliyevaa kanzu sikumuona, gari ikanipita.. na wao hawakukaa sana waliondoka pale kwa kutembea kwa miguu kuelekea main road. Na mimi nikawafata mbele kidogo nikaona wamepanda kwenye pickup zile kama za police, na mule ndani kulikuwa na wengine kama watatu plus dereva jumla walikuwa kama 6.

Mie nikarudi kwa njia nyingine nikakaa nje kama masaa mawili nagombana na Mbu tu.. ndani hapakaliki, nje hapalaliki.

Mida kama ya saa 6 usiku nikaingia home, nikapanga vitu vyangu vya muhimu vizuri, kesho yake nikaita bajaji nikavihamisha kwa wazee, nikarudi kumtafuta Landlord nikaongea nae na kumwambia nina safari ya miezi kama minne sitakuwepo au kama ntakuja sitakaa zaidi ya siku mbili. Kodi imebakije? Akanitajia kodi imebaki miezi miwili. Nikamwambia sawa hamna neno, ila kama sitaonekana akae akijua nimesafiri au mtu yeyote akiniulizia awaambie nimesafiri, wapi? awaambie hajui.

Hivyo, so nilichokuwa nafanya ni kurudi usiku saaana na kuwahi kutoka. Nilikuwa naenda katika chuo kimoja (Sitakitaja Jina) kama part time Technician and tutor, nikitoka naenda kwenye ma bar au clubs mpk mida isogee ndio narudi. Yaan niliishi kwa wiki mbili mfululizo kama mwizi au jambazi anayesakwa.

Muda huo natafutwa na namba tofaut tofauti ikiwemo na yule Manzi pia, sasa nashindwa ku ignore namba ngeni. Kila ikiingia text kuna namna namuuliza aliyetuma jibu atakalonipa najua huyu ni fulani so tunaendelea kuchat maana kwa maongezi ya simu haiwezekani, line ipo kwenye moderm na natumia PC pale napokuwa nimetulia kama huko chuoni au nikijibana kwenye ki pub au Bar.

Itaendelea nikipata muda wa kuandika.. this time ni nani exactly huyo Mumewe, ni nani aliyekuwa anamtafuta. Na mimi ilikuwaje nikasolve hii ishu.
Aisee pole, fanya kumalizia aisee.
 
Story tamu
emoji16.png

Safiii.... umetuwakilisha vyema.
Hivi viumbe wakilia lia we tatua shida zao mara moja.. hutotumia nguvu kamwe.
Kuna mwingine siku nyingine tulikuwa naye kwenye basi ambalo lilianzia tunduma kwenda Dar, mimi nikapandia njiani, yeye kaanzia tunduma. Sasa nikagundua tunavyoshuka kuchimba dawa au kununua msosi yeye hashuki au akishuka hanunui kitu. Nikajiongeza nilivyoshuka kituo kilichofuata nikadouble vitu nilivyonunua (maji, soda, chipsi, nyama choma). Nilivyofika nikamgawia aisee alishukuru. Safari ikachangamka kabisa yaani tukawa kama mtu na mkewe.
Huyu sikumtaka kivile maana hakufiti kwenye vigezo vyangu, so sikuhangaika na kuomba namba. Ila nikajifanya namkubali ili asijisikie vbaya. Tukiwa mlandizi sijui alihisi nini huenda ameona tunaweza kuachana bila mm kuomba namba. Yeye ndo akachukua namba yangu, akanibip nikaisevu. Kesho yake akanitafuta ila sikuhangaika naye. Baada ya wiki akanitafuta tena sikuhangaika tena ikabidi tupotezane hivyo.
 
[emoji23][emoji23][emoji23], mnajitahidi kutoa huduma kwa abiria wenzenu,
 
Hahaha.. basi hapo atatoa ushahidi kwamba kuna wanaume wakarimu.. hawana Tamaa za kimapenzi anaweza kukusaidia bila kuomba papuchi..

Kumbee hajafiti kwenye mfumo na mwamba umeona yanini mie..

🤣
 
Hahaha.. basi hapo atatoa ushahidi kwamba kuna wanaume wakarimu.. hawana Tamaa za kimapenzi anaweza kukusaidia bila kuomba papuchi..

Kumbee hajafiti kwenye mfumo na mwamba umeona yanini mie..

🤣
Nina list ndefu ya wanawake ambao huwa tunaanzisha mawasiliano na urafiki ambao kwa ucheshi wangu (na mwonekano wangu)yeye huchukulia namtaka ila mambo huenda ndivyo sivyo. Mimi mwanamke ambaye nitamtaka hata kama issue ikija kubumburuka hata mke wangu itabidi akubali tu kuwa hapa jamaa hakuwa na namna. Pisi kali inayoeleweka. Nikichat nao kama 10 hivi naweza ambulia wawili tuu au mmoja.
 
Ewaa.. sio unakuwa ZOA ZOA tu .. upo sahihi. Sometimes we need to be very selective.
 
Back
Top Bottom