Mbinu za kumfukuza kwako kijana aliyefikia umri wa kujitegemea

Hapana simfukuzi mwanangu kwangu namtafutia kazi aajiriwe na siku za weekend namwekea mambo yakufanya kama siumeajiriwa unapata mshahara hapa unachangia kidogo tu nenda sehemu nzuri nzuri ukaenjoy bwana upate mke kama ni. Mwanaume na katafute bwana bana kama nimwanamke aku.
Eti mwanangu ni mkimbize ninfukuzie mbali mtoa mada unajua uchungu wa mwana kenge wewe.

Ataolea kwangu . Atakuja muda wowote nitafuta shamba nimjenge nanikiwa nauwezo na mnunulia gari .

Unachekesha sana
 
Kwa maisha yetu ya kiafrika mtoto wa kiume unakaane nyumban muda wote ukingoja chakula mezan? Ivi najiuliza hapo baadaye hao ndo wanakua wazee wa kutoa ushaur Kwa watoto wao na ndugu mmmh 🤔
Nina kaka angu ana miaka 40net yupo home mpaka mda huu yupo pale kula kulala
 
Ndo kwa baba yake hapo aende wapi baba ndo anatakiwa kuondoka naye aende kwa baba yake 😂 😂
 
Hizo mbinu zako unafanya zote kwa mkupuo au unachagua mojawapo? Duh

Nimekumbuka msela mmoja alikuaga anagombana na baba yake, mzee akienda kazini au msikitini anafungiwa geti alafu sela linafoka ndani "nenda kwenu kijijini apa ni kwetu mimi ata kama umejenga nenda kwa wazee wako.. mshua hadi anakua mpole anajishusha bas fungua mwanangu, fungua babaa.
 
1. Namba Moja weka na kuku
2. Mwajiri house girl kutoka kwa wambulu au wahehe kwa gharama yoyote. Hili ni pigo la mwisho akigoma kusepa hapa unalenga aanze majukumu na demu atamlazimisha wasepe wakajitegemee. Na wakati mwingine kijana atakimbia kukimbia mimba yake
 
Ukimtimua Gen z hivyo anaondoka na harudi tena nyumbani maisha ya sasa sio kama zamani now days njian nyepesi ya kumfukuza kijana ni kumsaidia Kwa kumuwezesha kiuchumi mpe mtaji ,nenda nae ofisini kwako kama kuna kuhusu mfano kama ni fundi,dereva wa daladala,mfanya biashara nenda nae kwenye shughuli zako mlipe viposho ye mwenyewe ataona aibu kuendelea kukaa nyumbani coz ana pa kuanzia sasa ww unataka mtu aondoke Tu wakati kama mzazi hujamtengenezea hayo mazingira
 
Huyo mtoto unaemfanyia hayo yote ni huyuhuyu uliemzaa au wa kuokotwa??
Usithubutu kumfanyia hivyo kijana wako maana utajenga chuki Moja kali sana( hasa kwa wababa) huyo mtoto unaemfanyia hivyo akija kutoboa atamjali mama yake tu.

Kwani ukikaa nae ukamweleza kwamba kwa umri wako unatakiwa kuanza kujitegemea kitapelea Nini???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…