Ukweli mchungu.
Watu wengi wanatamani Sana kuwa matajiri lakini hawajui mbinu gani zinatumika.
Sisemi matajiri wote walikuwa mabahiri, la hasha Ila kikwetukwetu hii mbinu ya ubahili ndio njia nzuri ya kuelekea kuwa tajiri.
Ubahili nachukulia Kama kitendo Cha kutotumia pesa kwenye matumizi yasiyo ya lazima.
Hii njia nimeitumia miaka 10 Sasa na faida yake nimeiona. Kuwa mbahili sana, alafu utanishukuru baadae.
Pesa nilikuwa napata nzuri tu kwenye mishe zangu za gen supplies na kwenye construction Ila nilikuwa naishi maisha ya kawaida Sana, chumba na sebule kwa elfu 60 kimara huko ndani ndani. Ila kwa mwezi nilikuwa nakusanya faida mil 4, huu ni wastani.
Kuna mwezi napata kazi nyingi faida hadi m 8, 10 na Kuna mwezi napata mil 2 na Kuna mwezi hakuna kazi kabisa hivyo nafidia huo mwezi kwa mwezi niliopata zaidi
Ubahili unalipaje?
Baada tu ya kununua plots kadhaa jijini hapa, kila mwezi nikaanza ku-save mil 1.8 kwa ajili ya kujenga na mil 1.8 nyingine kwa ajili ya biashara ya hardware. Hivyo mwezi mzima nauendesha kwa laki 4 tu, inatoa 60 ya kupanga.
Hapo kulikuwa hakuna Cha kwenda kula bata wala kuhonga Wala kulakula ovyo(wengi mnaita eti kula vizuri). Na hakuna cha kununua gari Wala nini, nilikuwa na pikipiki boxer kwa ajili ya kuwahi mishe. Ila hata Sasa natumia ka-IST tu, hayo ma-prado baadae Sana huko.
Ndani ya miaka minne tu nikajikuta karibu ya mil 80(of course nilitumia mil 78) kwenye kujenga na zaidi ya mil 80 kwenye kuanzisha hardware.
Hivi Sasa hardware ndio inaendesha kila kitu changu na inalipa sana tena Sana. Hivyo nipate tender nisipate mambo ni byeeee.
Story itakuwa ndefu Sana, Ila ACHENI UJUAJI UBAHILI UNALIPA SANA.
ACHENI KULA BATA BILA KUWA NA MIPANGO
Next project ni hii dream house(namba mbili), location itakuwa Tegeta - wazo.
Hii natembea nayo kila mahali hadi kitandani ninayo, soon inazikwa kwa ground.
Architect ni mtaalam vantano, yupo sana kule IG, haikuwa yangu Ila niliipenda sana. Soon, soon.....
View attachment 1771255