Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 16,419
- 26,594
Katika miaka ya karibuni tumeshuhudia mambo ya ajabu katika ukimbizaji mwenge wa uhuru.
Wakimbizaji mwenge siku hizi wamegeuka kuwa TASK FORCE ya ukaguzi wa miradi.
Sina uhakika kama wakimbiza mwenge ni wahandisi au wataalam wa kukagua miradi na usimamizi wake.
Kama picha hapo juu eti mkaguzi anakagua kwa sululu kupima ugumu wa barabara.
Hili lilofanyika huko Njombe.
Hakuna anayejua vigezo vya ukaguzi huo kitaalam.
Naamini hawa vijana wakimbiza mwenge hawana utaalam wowote, zaidi ya uzalendo mkubwa kwa nchi yao.
Wao si maafisa wa TAKUKURU inayotembea.
Waratibu wa mbio wawape wakimbiza mwenge ujumbe wa kuleta mshikamano, amani ya nchi nakwa ujumla kuleta matumsini kwa wananchi.
Hayo ndiyo yalikuwa majukumu ya kwanza toka enzi za Mwalimu.