Mboga nisizopenda katika maisha yangu

Mboga nisizopenda katika maisha yangu

mimi mboga zote nakula mradi isipikwe na vitunguu..aisee vitunguu vina harufu na ladha mbaya vikipikwa
 
1.Mchicha. 2.Mlenda. 3.Kisamvu. 4.Dagaa wa mwanza. 5.Chinese. Hizi mboga sizielewi sijui kwa nini watu wanazipenda
Acha mambo ya kiwaki, unaijua mchicha , kisanvu, chainizi kavu kavu geto na ugali wa sembe acha Dona ni noooma!, kaulize moro ndo misosi yetu
 
Mlenda mboga nzuri sana ikiandaliwa katika mazingira safi ( unakula bila kinyaa).

Mchicha+ nyama au samaki na ugali, fresh kabisa.

Chinese cabbage ( sijui sukumawiki) sipendelei
huwa natengeneza picha mbaya sana akilini mwangu likija swala la mvutiko wa mlenda
 
Kuna mtu alisema hizo mboga mmekula tangu udogoni wakati wa ujamaa zimewakuza. Leo majifanya zinawakaba.🤣 Ila Mimi mlenda nimejilazimisha sana ila nimeshindwa
 
Mboga ninayoipenda ni maharage ,dagaaa waliopikwa vizuri.Pia chapati nabondaaa hata mwaka mzima iwe ya maji ,ya kusukuma mi natwanga tu.Tatizo watu naoishi nao hawajui kupika chapati ila mama Shadya kila siku buku langu la chapati anaondoka nalo.Ntavunja magereza yote nchini kuzitafuta chapati
 
FB_IMG_1730402321088.jpg
 
Back
Top Bottom