Mboga nisizopenda katika maisha yangu

mimi mboga zote nakula mradi isipikwe na vitunguu..aisee vitunguu vina harufu na ladha mbaya vikipikwa
 
Acha mambo ya kiwaki, unaijua mchicha , kisanvu, chainizi kavu kavu geto na ugali wa sembe acha Dona ni noooma!, kaulize moro ndo misosi yetu
 
Mlenda mboga nzuri sana ikiandaliwa katika mazingira safi ( unakula bila kinyaa).

Mchicha+ nyama au samaki na ugali, fresh kabisa.

Chinese cabbage ( sijui sukumawiki) sipendelei
huwa natengeneza picha mbaya sana akilini mwangu likija swala la mvutiko wa mlenda
 
Kuna mtu alisema hizo mboga mmekula tangu udogoni wakati wa ujamaa zimewakuza. Leo majifanya zinawakaba.๐Ÿคฃ Ila Mimi mlenda nimejilazimisha sana ila nimeshindwa
 
Mboga ninayoipenda ni maharage ,dagaaa waliopikwa vizuri.Pia chapati nabondaaa hata mwaka mzima iwe ya maji ,ya kusukuma mi natwanga tu.Tatizo watu naoishi nao hawajui kupika chapati ila mama Shadya kila siku buku langu la chapati anaondoka nalo.Ntavunja magereza yote nchini kuzitafuta chapati
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ