Mboga zangu 5 simple nizipendazo kulia chakula (hasa ugali) na Jinsi ninavyoziandaa

Mboga zangu 5 simple nizipendazo kulia chakula (hasa ugali) na Jinsi ninavyoziandaa

nmekwelewa sana mkuu. japo haya mayai ya kisasa yana madawa sana asee mm siyapendi. nkimaliza kusoma hii thread nategemea nitaanza kupenda kupika mana spend kupika asee.!!
pika mkuu kama una vitendea kazi vyote mkuu pika,kama hupiki

nakuhakikishia afya uliyonayo si yako,pika hebu halafu utaona.
 
hv karibun nahis ntaanza kupika mana kila cafe nnayohamia naona wanapika hovyo hovyo mno asee. afu unakuta veges waanakuwekea kakijiko kamoja dadeq
fungua macho unapoenda kula mahali tena fungua macho zaidi unapochota mboga Ipo siku utaona kitu na itakua ndio mwisho wako wakula huko.
 
Vyote hivyo nakorofisha pia hupenda nyama ya kukaanga kwa ugali pembeni kuna kachumbari pia prawns wa kukaanga lakini unaacha sosi kidogo hawa ni kwa wali. Sasa hivi niko kwenye zoezi kali sana la kujifunza kupika pilau. [emoji39][emoji39][emoji39][emoji39] Mie pia sipendi kula nje nafanya hivyo mara moja moja sana.
Hahaha eti zoezi kali,
Nakumbuka nilipika pilau langu la kwanza nikiwa na miaka 13, nilipika pilau la njegere, ilikua kama utani vile nikatoa kitu kila mtu hakuamini, naikumbuka ile ladha hadi leo.
 
Mkuu usiombe ukutane na anayejua kupika maini,yatakuwa your new fav side dish tena km jioni upate na ndizi mzuzu fried au chips na fresh juice.....aah usiku unalala tu
ni muda sana nilikua nayala kila asubuhi kwenye cafe naletewa na chapati mbili daah yalikua mazuri sana ila baada ya kuondoka ule mkoa sikuwahi pata fundi wakujua yapika kama vile,nili jarbu sehemu tofaut ila bado nikawa nakuta yanapkwa hovyooo basi ukawa mwisho na hadi na leo siya miss hata.
 
Hii ya yai nilikuwa sana nikiwa mwanafunzi. Ukikaanga vitunguu, hoho na nyanya acha viive kidogo. Unavunjia mayai mawili au matatu na kuyaacha kwanza. Yakiiva una Ona kabisa cheupe na njano wala havionekani kama uchafu.
nakulaga sana tena kwa maelezo hayo hayo uliyotoa pembeni na glass yangu ya mtindi aaah safi kbsa
 
Mimi ni moja ya wale wajuba wasiopenda kula mitaani iwe hotel,cafe,bar,pub,nk sehemu yeyote wanayotoa huduma ya chakula sio mpenzi wa kula sehemu hizo na hii n kwasababu sipendi pikiwa chakula nisichojua kimeandaliwaje,kimepikwa ktk hali gani,nk nk (sababu ni nyingi).

Mimi ni moja ya watu ambao huchelewa sana kurudi nyumbani kutokana na kazi zangu lakini hii hainifanyi niache kupika kwasababu moja ya vitu nivipendavyo chini ya jua basi kupika ni mojawapo ya vitu hivyo.

Unajua kuna watu humu tunawasiliana sana huwa nikirudi home naweza mwambia ngoja nipike kidogo basi wanaishia kucheka na kuniona muongo sazingine wananikubalia ila hawaniamini kbsa kama napika.

Leo nataja mboga zangu pendwa ninazo penda zipika ninapokua nimerudi home,hizi ni baadhi tu ya zile za chap chap ambazo ndani ya dk.10-20 nishaivisha mzigo upo mezani tyr kuelekea tumboni.

1. Mboga ya nyanya

Hii mboga naiita hivi kutokana nyanya ndio kitu pekee kilichotawala hii mboga.

Mahitaji yangu ni:
  • Nyanya
  • Hoho
  • Kitunguu maji
  • Kitunguu swaum (hiki hakikosekan kwenye friji huwa kipo standby maana hamna mboga napka ikose hii kitu hakuna)
  • Tangawizi (niliyoparua) hiii pia ipo standby kwa friji haikosekani maana naitumia ktk kila kitu ninachopka chini ya jua
  • Karot (nakwangua kdg na nyingine nakata kata)
  • Viungo vya pilau (vilivyosagwa)
  • Pilipili mbichi
Huo mchanganyiko naanza kuupika kama mboga zingine naanza kitunguu maji ilaa sisubri mpk ktunguu kiwe brown nakoroga in 1min natia tangawizi,nakoroga naleta karoti zangu zile zakukata kata + hoho (naweka pamoja) nafunikia kama dk kadhaa nakuja naweka nyanya + karoti zile zakukwangua naweka pamoja nakoroga then nafunika baada ya muda kidogo nakuja namalizia kile kitunguu swaum changu na viungo vya pilau masala+ ile plipli yangu kisha nakoroga mboga naifunikia, in 5min nikifunua nikipga mwko kona mbili tatu linatoka sotojo moja tamu sana. Chumvi mimi huwa nawekaga kule mwanzo kabisa wakati wakukaanga vitunguu.

Hii mboga nakulaga nayo ugali mkubwa hata mtto mdogo anaweza asivuke. (ni tamu sana na ni simple sana)

2. Mboga ya Mayai

Hii mboga ya mayai nadhani n mboga ninayoila sana chini ya jua kuliko mboga zingine nadhani n kwasababu ya utamu wake na addiction yangu na mayai kwakweli hata kama n kitambi nahisi hii mboga ndio chanzo cha kitambi.

Mahitaji

Ni yale yale na vile vile kama hapo juu kwenye mboga ya nyaya ila ninapopika mboga ya mayai huwa siweki masala za pilau so ktk mahtaji ondoa pilau masala ila vingine vyote viache kama vilivyo.

Jinsi yakuipika hiii kuna style zangu mbili ambazo napenda

style 1

Nikishaandaa mboga yangu kama nilivyoandaa mboga ya nyanya pale juuu ikiwa jikoni navunjia mayai yangu idadi ninayojiskia kisha nakoroga mpk yale mayai yaive mchuzi wa nyanya nao ukauke.Mboga tyr.

style 2

Napika mboga yangu kama mboga ya nyanya kule juu ila ikifka muda wa kuweka mayai,nakaanga pembeni mayai yangu yenyewe kama yenyewe yakiwa tyr nayaweka kwenye sahani nayakata vipende vidogo vidogo kisha vile vipande vyote namwagia kwenye ile mboga yangu,inakua kama nakula nyama mzeee kumbe n vipisi vya mayai,daah tamu sana na ugali.

3. Dagaa

Bana mimi ni moja ya wale raia ukiwalisha dagaa kila siku ndani ya wiki/mwezi/mwaka mzma hawachoki wala kukinai kila siku hii mboga n kama mpya kwangu kutokana na mapenzi yangu kwa dagaa nmejikuta jikon dagaa hawakauki ila sasa dagaa wengi walio tyr n wale wa mwanza wale wanaokua tyr wamekaangwa.

Mahitaji

  • Nyanya 1
  • kitunguu maji
  • karoti (zakukata kata + za kukwangua)
  • hoho
  • kitunguu swaum
  • tangawizi
  • pilipili
Wakati wakupka kama kawaida naanza na kitunguu changu maji,sisubr kiwe brown naweka karot + hoho nakoroga then nakuja naweka dagaa zangu + ile karot ya kukwangua kwa pamoja na pili pili yangu nakoroga mpk viungo vyangu karot na hoho nione vinakarbia iva kisha mwsho namalizia na ile nyanya yangu 1,nyanya hii nmeiweka mwsho mana haihelewi kuiva nikipga mwko mizunguko miwili mitatu mzgo unatoka unameremeta kbsa. Mboga tyr kuliwa na chakula cha siku hyo.

4. Kachumbari

Mahitaji
  • Nyanya mbichi 1
  • Kitunguu maji
  • Karoti
  • Hoho 1
  • Tango
  • Parachichi 1
  • Limao
  • Pilipili

maandalizi n simple kama yeyote anavyoweza andaa basi ikikamilika namix safi kabsa kitu tyr kuliwa na chakula cha siku husika.

5. Mtindi

Hiii kwangu husimama kama mboga na mara zingine husimama kama chakula kbsa maana kuna siku nakunywa nalala yani friji ikose kila kitu ila sio pakti ya mtindi.

Hizi ni zile za chap chap ambazo at any time naweza ziandaa mtu akala chakula akahisi kala 5 star hotel kwasababu sio masihara msosi ninaopenda kuula huwa najua upika kwa ustadi ule unaokidhi vigezo vyote kuliwa na raia mwenye njaa yake mjini.
Mkuu wewe ni JINSIA gani kwanza?
 
[QUOTE="Freema Agyeman, post: 36903590, member: 38427"
Dagaa, mtindi na mayai si mboga.

nieleweshe basi ni nini mkuu nielewe
[/QUOTE]

Pitia post #106 hapo juu.

Kutokula mboga za kutosha huathiri macho na kuona.

📌Dagaa, mtindi na mayai si mboga 📌
 
Back
Top Bottom