Mbona hamjahoji kuhusu Panadol, Aspirin na ARVs kuwa wazungu wanaweza "kutufanyizia"?

Mbona hamjahoji kuhusu Panadol, Aspirin na ARVs kuwa wazungu wanaweza "kutufanyizia"?

Retired

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2016
Posts
44,629
Reaction score
83,056
Makelele mengi kuhusu chanjo ya corona, mbona hamjahoji au kukataza dawa/chanjo tunazozitumia hospitalini leo hii?

Aina za chanjo ambazo kila mtoto wa Kitanzania anazipata na zinatoka west/USA

BCG (Bacile Calmette-Guérin)
DTP au DPT (Dondakoo, Pepopunda na Kifaduro)
Surua
Polio

Magonjwa haya ya kila mtu wa hapa Tanzania yanatibiwa na dawa toka wapi?
  • Dondakoo
  • Pepopunda
  • Kifaduro
  • Homa ya Manjano
  • Hepatitis A
  • Hepatitisi B
  • Haemophilus influenzae aina ya b (Hib)
  • Homa ya mafua (mafua)
  • Surua
  • Matumbwitumbwi
  • Kirusi cha rota
  • Surua ya Rubela
  • Pneumococcal
  • Polio
  • Varicela (tetekuwanga)
Yote hayo juu tunatibu kwa dawa zao, humo hawawezi kuweka hicho mnachokihofia kwenye chanjo ya corona?
 
Unaji contradict. Wewe muda unakuhusu nini as long as zinafanya kazi kama ulivyosema, muda is of what concern? Unakuwa na concern na muda kwa vile vaccine tunnel is very long na hii imekuwa very short tunnel, hivyo ukawa na wasiwasi na muda. BUT BY YOUR OWN ADMISSION KUWA ISSUE IS NOT EFFICACY, SAFETY ETC BUT TIME.
unatumia nguvu mzee..swala sio kua hazifanyi kazi...swala ni mda uliotumika kuidhinishwa
 
unatumia nguvu mzee..swala sio kua hazifanyi kazi...swala ni mda uliotumika kuidhinishwa
Nadhani by your post kuwa suala siyo kuwa hazifanyi kazi (meaning they are OK) umehakikisha kuwa haya yote HAPA CHINI yako perfect, sasa issue ya muda inatok wapi?

The vaccine construct must be safe and effective. To achieve this, the newly designed construct/s need to be checked for its antigenicity,
allergenicity,
toxicity,
solubility and stability
The result must show that the construct needs to be a potential antigen, non-allergic, non-toxic, soluble and highly stable. These outcomes make it a suitable vaccine candidate for further analysis.

SASA KAMA HAYO YOYE YAKO SAWA, ZINAFANYA KAZI, THEN WHY WORRY ABOUT MUDA?
 
Gwajima anapaswa atoke hadharani awaombe Radhi watanzania. vinginevyo atawajibika kwa kauli zake za upotoshaji wakati Taifa lipo ktk mapambano ya janga hili la korona.
 
Hili la chanjo ndio maana limeachwa liwe hiari, kila mmoja ana mtazamo wake tofauti na mwingine kwa sababu zake binafsi.
Kwa mfano mimi sichanjwi sio kwamba naamini wazungu wanataka kutuangamiza , la hasha, wana njia na mbinu nyingi sana za kufanya hivyo kama wakitaka kutuangamiza.

Umetolea mfano wa chanjo zilizotangulia na dawa tunazoendelea kutumia, ukaelezea kwamba ikiwa iko salama kwanini tuhoji kuhusu muda? Jibu ni kwamba ili hayo majibu ya usalama na madhara yapatikane, kuna muda umewekwa kujaribia na kujiridhisha kwa hatua kadhaa ili kuhitimisha na kuidhinisha matumizi yake.

Nikuulize, umeshawahi kusaign form ya kutokuiwajibisha serikali au watengenezaji wa chanjo kwa hizo za awali ulizozitaja? Unafikiri ni kwanini imeidhinishwa kwa matumizi ya dharura? Tatizo sio kutuangamiza, inaweza kuwa na madhara ambayo hata wao hawajayaona kwa sasa kutokana na huo udharura. Lakini pia inawezekana kabisa zikawa salama na zisiwe na tatizo lolote. Hapo ndio nnapoomba uhiari uheshimiwe. Kama unataka kuchanja, chanja, kama hauipokei kaa pembeni lakini sioni sababu ya upande mmoja kuwaona wengine wana tatizo au uelewa mdogo, kwenye hili ni kama kamari.

Ikumbukwe aliyechanjwa, anaweza kupata na akaathiriwa vibaya tu na hiyo Covid, japo wanasema anakua na uwezekano mdogo wa kupelekeshwa sana na madhara ya hiyo homa.
 
Back
Top Bottom