Mbona hamjahoji kuhusu Panadol, Aspirin na ARVs kuwa wazungu wanaweza "kutufanyizia"?

Mbona hamjahoji kuhusu Panadol, Aspirin na ARVs kuwa wazungu wanaweza "kutufanyizia"?

Damage control? Kasema kila Doctor atakaye administer chanjo ATAKUFAA!! Na kwamba hizo chanjo zimeletwa kutufanya mazezeta and sijui tumepokea kwa sababu tumepewa hela!!

Chanjo zimefanyiwa upembuzi na TMDA/NEMC etc ssa anaposema chanjo zimetolewa bila wataalam wa ndani kuzichunguza huoni ni mis information??

Angepinga chanjo kwa hoja zake ila sio kuanza kupotosha. Ni huyu huyu Aliapa corona itaishia Kenya ila TZ haitofika.... Ni huyu huyu alitabiri JPM kufika 2025 kwa kishindo ina maana nabii hakujua kuwa JPM hawezi maliza second term??

He's fake acheni kumtetea
Hao TMDA/NEMC kazi yao si ku certify tu kwani kuna ambalo lenye maslahi wanalipingaga? Hata wakigundua shida usitegemee watasema ila wao na familia zao wata abscond tu!
 
mi sina tatizo na chanjo kwakua nna wazee kwe familia(sikai nao) kinachonichanganya ni nguvu inayotumika...hii ni multi-million dollar empire..mind you wenzetu hawana madini..imagine chanjo zao wanazipush sana..ila za china na india wanazikataa,,wakati hata hizo sijui aspirini na chroloquine tunanunua india...wanataka tuchome za marekani tu wakati hata wao wenyewe wanazikataa.so hii ni biashara kama biashara nyengine....hata muuza majeneza anavutia kwake ukienda

Africa’s needs​

The World Bank estimates that Africa alone would need about $12bn for COVID-19 vaccines to attain sufficient levels of inoculations to interrupt virus transmission, according to a new paper by the lender and the IMF.
Sikatai kuwa na agenda ya siri ya biashara, ipo kabisa hiyo, you are perfectly right for that argument, but ni justifiable biashara.. nadhani unanielewa. Ninachokataa ni mastory kama ya Gwajima and the like. Issue ya biashara lazima iwepo ndiyo maana Benz ni bora kuliko Toyota..... Rolls Roys ni bora kuliko Toyota cresida... 😀 😀 😀 😀 😀
 
Take note please: Usije ukasoma clip za mitandaoni ukaziamini, sidhani kama una uthibitisho usiokuwa na mashaka na hicho nilichoki quote hapo
kwanini wao USA waikatae JOHNSON & JOHNSON
 
Nimesisitiza tokea awali, haki na hiari ya kuchanjwa kila mmoja anayo, ni ajabu na kushangaa ikiwa upande mmoja utajitapa na kuwaona wengine hawako sahihi. Na sijawahi beza wanaochanjwa hata mara moja na sitokaa nifanye hivyo kwa vile naheshimu uhuru wa wengine.

Hayo mambo ya treni na miduara sijui yanatokea wapi.

Miye pia nimesisitiza tangu mwanzo chanjo ni hiari. Basi wote letu moja.
 
Kwani kosa lake ni lipi?

Amesema dhahiri tumuunge mkono raisi wetu katika mapambano dhidi ya Corona ila pia kwakuwa chanjo zimekuja ila anaona ingefanywa hiari ili anayetaka achanjwe na asiyetaka asichanjwe!

Ila kwa ushauri wake yeye binafsi asingeshauri watu kuchanjwa kwa sababu anahisi medical procedures za ku arrive kwenye chanjo hazijafanyika kwa utaratibu sahihi ili chanjo hizo zisije zikatuletea madhara.

Thats by the observation of the Video Clip yake!
Anatuaminisha kuwa chanjo hizi sio salama, as if Serikali yetu imekurupuka!

Wakati Mhe Rais amejiridhisha kwa kuunda Jopo la wataalamu wabobezi ktk masuala ya afya na majanga na kuthibitisha chanjo hiyo kuwa ni salama kabisa, halafu pia bado ni hiari kuchanja.

Asitubabaishe, Askofu sio msemaji wa mambo ya afya aache kiherehere cha kuingilia utaratibu wa serikali.

Serikali ipo tena ipo makani kuliko anavyo waza.
 
Hao TMDA/NEMC kazi yao si ku certify tu kwani kuna ambalo lenye maslahi wanalipingaga? Hata wakigundua shida usitegemee watasema ila wao na familia zao wata abscond tu!
Kwahiyo hamziamini tena TMDA/NEMC..... Then kwanini mnatumia dawa au maabara ambazo ziko certified na taasisi za serikali if at all hamuwaamini? Hamuoni mnafanya double standard
 
Ameandika Malisa GJ.

Kumekuwa na mjadala mkubwa sana kuhusu chanjo ya Corona katika nchi nyingi za Afrika. Baadhi ya viongozi wa dini wamedai chanjo hiyo inalenga kupunguza idadi ya watu weusi kwa kuwazuia kuzaliana, na wengine wameihusisha na chapa ya 666 inayodaiwa kuwa ya Mpinga Kristo.

Kufuatia madai hayo mwanaharakati Tracy Zille wa Afrika Kusini ameandika maoni yafuatayo (nimefanya tafsiri isiyo rasmi);
_________
Waafrika wanapaswa kuwa watu wa mwisho kulalamika kuhusu chanjo ya Corona. Kama kweli wazungu wangetaka kuwaua wangeshafanya hivyo miaka mingi iliyopita. Vinywaji vingi vinatoka Ulaya, hadi maziwa ya watoto. Wangetaka kuwaua wasingekua na haja ya kusubiri chanjo ya Corona.

Kitu kikubwa waafrika wanachoweza kutengeneza ni watoto wasio na mpangilio baada ya kufanya ngono kienyeji. Tulieni, hakuna mtu mwenye mpango wa kuwaua. Nyie sio muhimu sana wala sio tishio kwa dunia kiasi cha kutaka kuwaua.

Kama hamtaki chanjo yetu basi tengenezeni yenu. Lakini kama hamuwezi kutengeneza kondomu wala miswaki, mtaweza kweli kutengeneza chanjo ya corona? Hadi vichokoa meno (toothpick) mnaagiza China halafu mko busy kutukana wazungu eti wanataka kuwaua?

Jifunzeni angalau kutengeneza condom kwanza kabla hamjapiga kelele zisizo na msingi kuhusu chanjo ya Corona. Dawa nyingi mnazotumia katika hospitali zenu ni kutoka Ulaya, lakini leo mnajazana ujinga eti wazungu wanataka kuwaua kupitia chanjo ya Corona.

Hata chupi mnazovaa zimetoka nje ya Afrika. Kama sio kutoka China basi ni mitumba kutoka Ulaya na Marekani. Hamuwezi kutengeneza hata chupi za kusitiri maungo yenu lakini mko "busy" kutukana wazungu wanaoumiza vichwa vyao kutengeneza chanjo ya corona.

Hamuwezi hata kutengeneza dawa rahisi ya kutuliza maumivu ya kichwa kama Panadol, lakini mnajazana ujinga eti wazungu wanataka kuwaua. Sasa uamuzi ni wenu. Kuikubali chanjo ya corona mpone, au muikatae mfe kwa ujinga wenu.

Kama sio wazungu midomo yenu ingekua inanuka kama maiti ya panya kwa sababu hamuwezi kutengeneza hata dawa ya meno. Colgate inatengenezwa Marekani, Aquafresh Uingereza, Mentadent Canada, Sensodyne Japan. Tungetaka kuwaua si tungeshawamaliza siku nyingi? Kwanini tusubiri kuja kuwaua kupitia chanjo ya corona?

Tunatengeneza wanasayansi wa kuisaidia dunia, nyie mko busy kutengeneza Mitume na Manabii matajiri. Tunatengeneza chanjo ya corona nyie mnatengeneza mafuta ya upako. Halafu mnasema tunataka kuwaua. Wajinga nyie.

Hata dawa za kupunguza makali ya virusi vya UKWIMWI (ARVs) zinatoka Ulaya na Marekani. Sasa kama kweli wazungu wanataka kuwaua waafrika si wangeshawamaliza kupitia ARVs? Unakuta mwafrika amekondeana kwa UKIMWI lakini akishameza ARVs za wazungu akapata afya anasema eti wazungu wamebuni chanjo ya Corona ili kuua waafrika. Upumbavu gani huu?

Msinitukane kwa kuwaeleza ukweli. Tumetumia pesa zetu kuwajengea vyuo vikuu (Chuo kikuu UDSM kilijengwa mwaka 1961 na JF Kennedy, Chuo kikuu cha Zambia kilijengwa na Harold Wilson mwaka 1996, Chuo kikuu Nairobi kilijengwa na Anthony Eden mwaka 1956 kikiitwa Royal Technical College).

Hiyo ni mifano tu lakini tumetumia pesa zetu kuwajengea vyuo vingi na vituo vingi vya utafiti. Nyie mnatumia pesa zenu kujenga makanisa makubwa na kuwanunulia Mitume na Manabii magari ya kifahari.

Vituo vyetu vya utafiti vimebuni chanjo za magonjwa makubwa kama surua, polio, tetekuwanga, ndui, homa ya ini etc. Vituo vyenu vya mitume na manabii vimebuni mafuta ya upako. Mnanunua mafuta ya upako kwa gharama kubwa bila kupiga kelele, lakini chanjo ya corona mnayopewa bure mnapanua midomo kuitukana. Mna mdudu kichwani, si bure.

Halafu hii sio chanjo ya kwanza kuwaletea huko Afrika. Tumeleta chanjo nyingi na mmezitumia bila kelele. Chanjo za polio, surua, homa ya ini, tetekuwanga etc. Tungetaka kuwaua si tungetumia chanjo hizo? Kwanini tusubirie ya corona?

Baadhi ya nchi za Afrika mmeanza kuharibu miundombinu ya teknolojia ya 5G kwa kuihusisha na Corona. Hili si jambo la kushangaza kwa sababu mnaua hadi mama zenu wa kuwazaa kwa kuwahusisha na uchawi. Kwa sababu tu ya ngozi zao kusinyaa kwa uzee na macho yao kuwa mekundu kwa kutumia nishati ya kuni, kwenu huo ni ushahidi wa uchawi. Mnawaua bila huruma.

Muda si mrefu mtaanza kuwaua wagonjwa wa Corona kwa kuhisi wamelogwa au wametupiwa mkosi. Haya ndio mawazo ya watu wapumbavu, wasioelimika na washamba kama nyie. Watu ambao mnaamini eti kila nyumba ya tajiri ina chumba maalumu cha kufuga majoka yanayomletea hela.

Sikikizeni nyie wapumbavu. Kama chanjo ya Corona ingegunduliwa Afrika, viongozi wenu wasingeitumia. Wangesafiri kwenda India au nchi za Ulaya kutafuta chanjo nyingine.

Viongozi wa Afrika hawaamini katika huduma za afya za nchi zao. Hawaamini hospitali zao, hawaamini madaktari wao, hawaamini hata dawa zao. Ndio maana wakiugua hata malaria tu wanapanda ndege kwenda kutibiwa nje ya nchi.

Kwahiyo wakati mkiwaza eti wazungu wanataka kuwaua kwa chanjo ya corona, viongozi wenu nao wanawaza mnataka kuwaua kwa huduma mbovu za afya. Ndio maana wanajenga hospitali lakini hawatibiwi humo, wanasomesha madaktari lakini hawawaamini. Wanakimbilia kutibiwa nje. Wanajenga shule lakini watoto wao hawasomi humo.

Chanjo ya Corona ni kengele ya kuwakumbusha waafrika kuchagua viongozi wenye maono na uwezo wa kupambana na matatizo yao. Afrika ingekuwa na uongozi thabiti ingekua bara tajiri zaidi duniani. Lakini kwa sababu ya ujinga wenu wa kuchagua viongozi wasio na maono, wameuza rasilimali zenu kwa wazungu na Wachina, kwa faida yao na familia zao, huku wananchi mkiteseka kwa umaskini.

Badilikeni. Kabla hamjalaumu wazungu,

Nini maoni yako?
 
Kufuatia madai hayo mwanaharakati Tracy Zille wa Afrika Kusini
Malissa ana quote fake account?? Tracy zille ni account ya EFF kuchochea racist wars!! wala hakuna mwanaharakati wa jina hilo huko Sauzi.
 
Sawa tu
Screenshot_20210725-204901_Chrome.jpeg
 
Makelele mengi kuhusu chanjo ya corona, mbona hamjahoji au kukataza dawa/chanjo tunazozitumia hospitalini leo hii?

Aina za chanjo ambazo kila mtoto wa Kitanzania anazipata na zinatoka west/USA

BCG (Bacile Calmette-Guérin)
DTP au DPT (Dondakoo, Pepopunda na Kifaduro)
Surua
Polio

Magonjwa haya ya kila mtu wa hapa Tanzania yanatibiwa na dawa toka wapi?
  • Dondakoo
  • Pepopunda
  • Kifaduro
  • Homa ya Manjano
  • Hepatitis A
  • Hepatitisi B
  • Haemophilus influenzae aina ya b (Hib)
  • Homa ya mafua (mafua)
  • Surua
  • Matumbwitumbwi
  • Kirusi cha rota
  • Surua ya Rubela
  • Pneumococcal
  • Polio
  • Varicela (tetekuwanga)
Yote hayo juu tunatibu kwa dawa zao, humo hawawezi kuweka hicho mnachokihofia kwenye chanjo ya corona?
Kwa kuwa ASKOFU Gwajima hawezi kupata UKIMWI NA KUTUMIA ARV.....yeye ni mtu wa mbinguni.....

Kwa kuwa ASKOFU GWAJIMA hana ndugu awezaye kupata UKIMWI na kutumia ARV....ndugu zake nao ni wa mbinguni na si dunia hii......

Kwa kuwa ASKOFU Gwajima haumwi na kichwa....na akiumwa Kichwa hatumii PANADOL na ASPIRIN....watu wa mbinguni huwa wanafanya tu MAOMBI na kujibiwa HAPOHAPO.....

#KaziIendelee
#TukitokezeTukachanjwe
#NchiKwanza
 
Makelele mengi kuhusu chanjo ya corona, mbona hamjahoji au kukataza dawa/chanjo tunazozitumia hospitalini leo hii?

Aina za chanjo ambazo kila mtoto wa Kitanzania anazipata na zinatoka west/USA

BCG (Bacile Calmette-Guérin)
DTP au DPT (Dondakoo, Pepopunda na Kifaduro)
Surua
Polio

Magonjwa haya ya kila mtu wa hapa Tanzania yanatibiwa na dawa toka wapi?
  • Dondakoo
  • Pepopunda
  • Kifaduro
  • Homa ya Manjano
  • Hepatitis A
  • Hepatitisi B
  • Haemophilus influenzae aina ya b (Hib)
  • Homa ya mafua (mafua)
  • Surua
  • Matumbwitumbwi
  • Kirusi cha rota
  • Surua ya Rubela
  • Pneumococcal
  • Polio
  • Varicela (tetekuwanga)
Yote hayo juu tunatibu kwa dawa zao, humo hawawezi kuweka hicho mnachokihofia kwenye chanjo ya corona?
Kwamba unadhani tunakataa chanjo kwa sababu tunapenda kufa?

Tunaangalia mambo mengi tu, huko ilikotoka kwenyewe waliwahi kuikataa hii chanjo ya J&J, inatia mashaka sana hizi chanjo, hatupendi kufa ila tunasikia mengi ndio maana watu tunaogopa, huko Ulaya wamechanja na lockdown inaendelea, kuvaa barakoa kunaendelea kwanini??

Suala la Corona liko kipekee sana usifananishe na surua na magonjwa mengine
 
Sikatai kuwa na agenda ya siri ya biashara, ipo kabisa hiyo, you are perfectly right for that argument, but ni justifiable biashara.. nadhani unanielewa. Ninachokataa ni mastory kama ya Gwajima and the like. Issue ya biashara lazima iwepo ndiyo maana Benz ni bora kuliko Toyota..... Rolls Roys ni bora kuliko Toyota cresida... 😀 😀 😀 😀 😀
We mstaarabu ndugu yangu...ila hali ikiwa sio hali kuchoma kitu gani......tutachomwa tu aisee
 
Back
Top Bottom