Sisi wananchi lazima tuchangie maendeleo ya nchi yetu- hivyo tutachoka lini kusimangwa na wazungu na wachina kila wakitupatia misaada. Kutokana na mahela yaliyokusanywa ni wazi kwamba kuna watu wanauwezo wa kulipa hizo tozo . Pesa iliyokusanywa kwa miezi miwili - billioni 60 si mchezo, huku wananchi wakilalamika kuwa hawana uwezo . Kuna pesa nyingi inayo pita kwenye miamala ya simu- kuna biashara kubwa sana mtandaoni, Serikali ilikuwa haipati kitu! Hongera kwa serikali ya Mama kugundua chanzo kipya cha mapato. Awamu ya tano -ilijitahidi kiasi chake - lakini iliacha madeni makubwa kwa wazabuni waliofanya kazi na serikali, wafanya biashara walifunga maduka yao wakilalamikia TRA. Hiki chanzo kipya kitasaidia kujenga nchi hii kikitumika vizuri. Wezi wa wapesa za wananchi wapigwe miaka 30 jela, tuone kama mtu ataziiba.