Kama kweli umeanza biashara kwa mtaji wa 350k na sasahivi mtaji umekua hadi 4.5M kwa muda wa miezi 3 basi hiyo biashara ni nzuri. Swali ni je kwanini unafikiria kubadilisha/kuanzisha biashara nyingine? Kuanza biashara mpya means unaweka mtaji wako kwenye risk mpya ambayo hauifahamu. Ushauri wangu ni endelea kufanya hiyo biashara maana mtaji umekua na ni biashara ambayo umeshapata uzoefu nao (small risk) kwahiyo tumia hiyo 4.5M kuexpand biashara yako. Ila kama nia yako ni kubadilisha biashara au kuongeza biashara mpya then nakushauri usiweke mtaji mwingi kwenye biashara mpya. Investment kubwa iwe kwenye existing business wakati unaisoma hiyo biashara mpya.
Kuhusu biashara ya kufanya kwa mtaji wa 4.5M basi angalia biashara zinazotarget wanachuo coz nyingi hazihitaji mtaji mkubwa lakini pia umesema unasoma chuo so I believe you can get customers easy kidogo. Mfano wa biashara ni kama kuuza nguo za mitumba mostly kwa wadada (ni wateja wazuri) and you can easily use social media kuwapata. Biashara nyingine ni salon ya kucha kwa wadada wa chuo (hii sina uhakika kuhusu investment yake so itabidi uifanyie research) ila ukipata wapaka rangi wazuri I believe unaweza kutengeneza hela nzuri wateja wakishakuzoea. Kumbuka! Usikimbilie biashara ambazo zinaanza kukupa faida chap! Nyingi huwa zina risk kubwa sana mfano boda na bajaji, ni biashara nzuri ila ni highrisk. Pia kumbuka kwenye biashara yoyote inakubidi uwe directly involved na hiyo biashara na sio kumuachia mtu, Itakupunguzia risk ya kupoteza mtaji wako.
PS: Mungu aendelee kukusimamia, siku ukifikisha mtaji wa at least Mil 15 nitafute nikupe biashara nzuri zaidi.