Wasalaam wana JF
Hivi katika hali ya kijamii au kiimani mbona hiki kibali cha kuoa wake zaidi ya mmoja sioni mantiki zaidi ya starehe ya ngono, kama nguvu kazi ya kiuchumi mfano kilimo so unaweza kukodi vibarua, je, mwanamke ni chombo cha starehe kwa mwanaume? Kwanini yeye mwanamke pia asiwe na kibali ha Kuoa waume zaidi ya mmoja.
Kuna haja wanawake wajikomboe kwenye hili vinginevyo haijakaa vizuri.
Nimewaza radha ya mbususu na mnyanduano nimestaajabu akili kubwa za wazee wa kale.
Wadau wa jukwaa tusaidieni dhana ya kuoa wake wengi kama msingi wake sio starehe ya ngono kwa wanaume ni nini?
Sex=energy
Energy=food
Food = money
Wadiz
Kila mtu na mapenzi yake na kila mtu ana malengo yake, ila suala la wanaume kuwa na wanawake wengi ni jambo la kawaida lakini lipo juu ya maamuzi ya mtu binafsi.
.
Twende nyuma kwanza, utajiri wa zamani ilikua ni nguvu ya familia. Kwahiyo kadri mnavyokua wengi thamani yenu na nguvu yenu inaongezeka na mnaweza kujilinda, kuzalisha mazao mengi vilevile mnaweza kuvamia wanyonge na mkashinda kirahisi. Kibaiolojia tunafahamu kuwa mwanamke ana ukomo wa uzao na mwanaume ana nafasi kubwa ya kuendelea kuzaa hata kama mke wake mmoja akiwa amefikia ukomo, hivyo basi ili kulinda nguvu na utajiri wa familia inabidi mwanaume aongeze mwanamke amzalie watoto wengine.
.
Turudi sasa, kilichobadilika sasa ni kwamba hakuna haja ya kuwa na familia kubwa ili uweze kuilinda familia, polisi wapo. Lakini kibaiolojia hakuna kilichobadilika. Bado kama wanaume tunataka kuwa na urithi mkubwa, bado tunataka majina yetu yawe makubwa, bado tuna ile hamu ya kuwa na wanawake wengi.
.
Hivyo mwanamke sio chombo cha ngono, bali ni kiungo cha kuongeza jamii, endapo kama hutotaka jamii iongezeke kwa kasi basi ndo apo inabidi mwanaume ajizuie ila kama kama jamii mnataka kuongezeka na mwanaume hana ukomo hivyo inabidi awe na wanawake wengi jamii iongezeke, na ili jamii yoyote iendelee ni LAZIMA iongezeke kwanza.
.
Wanawake ni wengi kuliko wanaume.
.
Mwanamke mmoja ana mudi tofauti kwenye mwezi hivyo wanaume wengi hawawezi kuyahimili mabadiliko hayo, hivyo suluhisho ni kwenda kwa mwanamke mwingine hadi mwanamke wa kwanza awe mtulivu na wapili nae atakua ana mudi tofauti, hivyo atarudi kwa wakwanza, na mzunguko upo hivyo.
.
Sababu nyingine ni kuwa mwanamke ndiye anayechagua kuwa na mwanaume au la, hivyo ni wanawake wenyewe ndio wapo tayari kuwa na mwanaume mwenye wanawake wengi sababu ndie mwanaume mshindi kuliko wanaume wengine, wanawake wanapenda kuwa na wanaume washindi.
.
Mwisho, huo ni mtazamo wako kwamba wanawake ni chombo cha starehe, mwanamke ni kiungo muhimu kwenye jamii, hivyo ukibadili mtazamo utaona tofauti.