Mbona kwarezma watu wanafunga na wala hawawakatazi wengine kula?

Binti wa kigalatia mbona ueleweki!

Unaanza na sambusa unamalizia na bunduki.

Habari za kuilaumu serikali inatoka wapi tena?
 
UP3NDO NI MUHIMU KULIKO DINI
Na hapa ndipo mamluki na wasiojua dini zao zinataka nini wanapopotezwa!

UPENDO!

Mtu ana chuki, husda, mfitini, msengenyaji, mchoyo, mlozi Ila sasa anahudhuria Ibada zote na kuaamini yeye mbinguni next door tu hapo!
 
"UDINI" ni ruhusa kutoka kwa nani mpaka mtu asile kwaajili ya dini isyo mhusu?
 
Mtoa mada anataka kujua sababu ya kupiga bakora wengine kwa sababu hawajafunga ilhali mfungo wa kwarsma hakuna kushurutishana,
 
Pole pole ndugu yangu. Hoja yako Ina nguvu Ila mbona haraka haraka Sana? Ona sasa makosa ya kiuandishi yalivyojaa!!. Any way, hizi zote ni changamoto za muungano na za kikatiba. Zanzibar ni Kama nchi za ng'ambo ambazo Katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania haihusiki katika kuongoza na kusimamia kanuni za kiutawala na kisheria. Zanzibar inajiamulia na kufanya inachotaka. Uhuru wa wananchi ziro kabisa. Na serikali ipo lakini haisemi chochote. Leo kaombe kiwanja Zanzibar Cha kujenga kanisa uone!. Wao wakija bara Kila kitu Hakisawa Kama wamezaliwa Mbeya. Katiba mpya ndiyo jibu tu. Ila wanasemaga yajayo ni neema tupu au yanafurahisha nafikiri walitabiri juu ya Katiba mpya. Nisameheni bure jamani, nisiposema Mimi atasema Nani?.
 
Kipindi cha mfungo wa Ramadhani biashara ya kitimoto huwa inashuka sana hasa mikoa ya Dar es salaam ,Pwani 'Tanga,Lindi ,mtwara na ujiji kigoma na Zanzibar kwenye waislamu wengi

Mauzo pia ya Pombe kwenye hayo maeneo Hushuka sana kipindi cha Ramadhani

Mauzo hupanda juu wakifungua
 
Tena sio kuzuia kula tu...wakristo hata hawalalamiki kupanda kwa gharama yoyote ile wao na maumivu yao...njoo sasa upande wa pili....kila kitu wanaonewa utadhani wamepandishiwa wao wengine bei iko chini.

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Acha mipasho lete hoja na mifano hai, nani kakatazwa kula na wapi?
 
Ni raia wanayo haki ya kulalamika bei kama sio rafiki
 
Mkuu vinajaaa hawanaaa marindaa tenaaa????inamaana kuna wanaumee wanawakidhiaa hajaa wanaume wenzaooo???
 
Kuna watu wanakua KAMA WACHAWI
 
Mtoa mada anataka kujua sababu ya kupiga bakora wengine kwa sababu hawajafunga ilhali mfungo wa kwarsma hakuna kushurutishana,
Kama kweli kuna watu wanafanya hivi ni ulimbukeni tu unawasumbua, hao ndio wale hata kumeza mate hawataki (kutuchafulia tu mji) eti watafungua, Uislam haukuifanya funga ya Ramadhani kuwa ngumu kiasi hiki...hao wafanyayo hayo ya kupiga watu kuwalazimisha kufunga hawajui dini...ni ama wamekariri tu...muwasamehe buree!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…