FEEDBACK!!…
NIMESAFIRI KUFIKA LINDI LEO KUJIRIDHISHA NA UTETEZI WA BAADHI YA VIJANA
1.Lindi Bado ni Mkoa ambao upo nyuma sana kuliko mikoa yote niliyowai kuitembelea na yote ambayo nimewai itembelea
Kifupi bagamoyo pameendelea na kuchangamka kuliko Lindi!!
2.Ina idadi ndogo sana ya watu hivo kufanya iwe sehemu iliyopoa zaidi Tanzania
3.Stand yake n ndogo sana kuliko stand ya Usagara Ya Mwanza misungwi, Tabora mjini,
Kifupi haikaribiani hata nusu ya stand hizi kama ya shinyanga,Mtwara,Mbinga Ruvuma,singida ,
Sijui hata budjet yao ya kujenga na kupanua stand walipeleka wap!!
4.Sehemu kubwa ya Lindi ni mapori makubwa sana (Nashangaa hizi vita za wafugaji na wakulima kanda ya ziwa kwann wasiwahamishie huku wafugaji[emoji3]
5.Sehemu za starehe huku msiba!! (hakuna )
6.Hakuna muingiliano mkubwa wa watu huku
7.Vyuo ndo hivo tena nisiseme mengi
8.Ingawa sijafika Kilwa lakini naona kuna dalili hizi hizi za Mkoa mama huu Lindi!! Nadhani kutakua na sifa hiii hii kubwa Mji wa zamani lakini wa mwisho kwa ukuaji
9.Kuna kiwanda cha cement nadhan n cha dangote ukipita barabarani wamejaza mawe
10.Uchimbaji chumvi upo kwa kiasi kikubwa nadhan ni sehemu ya kipato cha wakazi wa huku
Fursa!!
1.Kilimo na ufugaji-Kuna ardhi kubwa sana huku kwa ufugaji na kilimo!!..cha mazao kama minazi,korosho nk(Sijayafanyia utafiti)
2.Kulingana na uwepo wa Gesi maeneo haya basi ni vema serikali isihamishe gesi huku!! Ifue umeme ndiyo iuunganishe na grid ya taifa kwenda mikoa mingine atleast kutafufua uchumi wa eneo hili!!..
3.Kuanzisha huduma ya gesi majumbani ya mfumo wa kuunganishiwa kama maji
Hii project ingeanzia huku ingeboresha maisha ya wakazi wa hapa pia ingefanya sehemu iwe pendwa kwa watanzania wengi hivo kukuza maendeleo
4.Kujenga vyuo Lukuki hasa huu mkoa!!!…
Uhitaji wa Elimu ya juu bado mkubwa kwa tanzania ,,,,Hivo kuongeza miundo mbinu hii ya vyuo vya elimu ya juu hapa kungeleta uchangamfu wa mji na maendeleo kwa ujumla kadiri watu wanavoongezeka!!
Hapa n kwa sekta binafsi na sekta za umma vyuo n vyuo bana
5.Kuna fursa kubwa sana ya utaliii hasa ukizingatia almost nusu ya mkoa umepakana na bahari, utalii wa fukwe,milima nk na wamajengo ya zamani pia
6. Uvuvi
Kutengeneza mazingira ya kuwezesha uvuvi wa kisasa maeneo haya wa kutumia meli za kisasa pamoja na miundo mbinu na viwanda vya kuchakata samaki
7,8,
Vingine mnaweza kuongezea