Mbona malalamiko mengi kwenye nyumba za kuficha Bati (Hidden Roof), Mafundi wanakosea nini hadi zinavuja?

Mbona malalamiko mengi kwenye nyumba za kuficha Bati (Hidden Roof), Mafundi wanakosea nini hadi zinavuja?

Nyumba hizo ni hatari sn. Sitarudia tena. Zimenipa HASARA KUBWA SANA. Nimeamua kuezeka kawaidi. Sasa nafurahia kuwa nyumbani kwangu kwa raha hata kama mvua inanyesha. Zamani inapokuja mvua ROHO JUU! Maana imewahishusha Gypsam board yote chini. Ikavunja vitu vingi ndani pale. Aise sitakaa nisahau.
Mpaka Sasa Watakuja Wakina Tomaso Ama Tuseme "Kusikia Kwa Kenge Mpaka Atoke Damu Puani Na Masikioni "
 
huu uezekaji asili yake ni kutoka uturuki,lakin tofauti yetu na wenyewe n kwenye paa wanamwaga jamvi ila kwa kwetu utakuta fundi anataka pesa hawezi kukushauri vzr juu ya nyumba hizi ila kiukweli kuna sababu nyingi sana zinazopelekea hizi nyumba kuvuja na pia ukiezeka jitahidi ndani ya miaka mitano uchumi wako usiyumbe
 
Yaani hujui tu ubabaishaji wa Tanzania? Mafundi wenye sifa ya ufundi ni wachache sana. Wengi vishoka. Nchi nzima.
Uko sahihi sana mkuu. Fundi aliyenichinjia baharini aliniambia ni fundi maarufu toka DAR. Na amejenga nyumba za namna hiyo nyingi sana, kwamba amejenga mpaka Zanzibar. Akanionyesha na picha.
Kula leki akaniingiza mkenge. Mvua ya kwanza tu maji ndani. Akarekebisha. Mvua iliyofuata gypsam bodi yote chini, puuu! Tanzania hatuna wataalam wa nyumba hizo....tuna force tu.
 
View attachment 2924216
Kumekuwa na malalamiko mengi kuwa nyumba za kuficha Bati maarufu kama Contemporary au Hidden Roof zina shida ya kuvuja sana, sasa wataalamu au mliofanikiwa kujenga hizo nyumba hebu tushauriane hapa mafundi maiko wetu hawa wanakosea wapi?

Maana nataka kubadili paa langu liwe Hidden ila kila nikiona malalamiko ya wadau na picha za baadhi ya nyumba zinavyotia balaa nakosa ujasiri wa kufanya hizo changes.
Ukweli ni kuwa Mafundi wengi awajui jinsi ya kuezeka hizi aina ya paa! Tanzania ya sasa Vijana awataki somea fani yeyote..... wanapenda Short cut. Kuanzia kwenye ufundi magari,simu,Nyumba ndo kabisa unakuta fundi anaweka tiles Chooni maji ayaendi😭. Jirani yangu baada ya kubadilisha mafundi zaidi ya 2 na hasara juu.... nikamwambia juu ya fundi mbobezi wa kuezeka hizi paa(ni graduate wa Civil Eng) Nikampa no yake akamwita...alipopewa Bei akakataa akaendelea tafuta Mafundi Magumashi wa bei rahisi. Mpaka muda huu nnapoandika hapa Nyumba ipo aijapata fundi mzuri na wa bei chee.Waenga walisema BURE AGHALI. Mafundi wabobezi wapo tatizo wengi wetu tunapenda Kitonga
 
View attachment 2924216
Kumekuwa na malalamiko mengi kuwa nyumba za kuficha Bati maarufu kama Contemporary au Hidden Roof zina shida ya kuvuja sana, sasa wataalamu au mliofanikiwa kujenga hizo nyumba hebu tushauriane hapa mafundi maiko wetu hawa wanakosea wapi?

Maana nataka kubadili paa langu liwe Hidden ila kila nikiona malalamiko ya wadau na picha za baadhi ya nyumba zinavyotia balaa nakosa ujasiri wa kufanya hizo changes.
tumia bati bora na imara zingatia ratio ya cement huko juu 🐒
 
Uko sahihi sana mkuu. Fundi aliyenichinjia baharini aliniambia ni fundi maarufu toka DAR. Na amejenga nyumba za namna hiyo nyingi sana, kwamba amejenga mpaka Zanzibar. Akanionyesha na picha.
Kula leki akaniingiza mkenge. Mvua ya kwanza tu maji ndani. Akarekebisha. Mvua iliyofuata gypsam bodi yote chini, puuu! Tanzania hatuna wataalam wa nyumba hizo....tuna force tu.
Kama wachina wakijitosa kwenye ufundi ujenzi wa mtaani watapata masoko sana. Wanajua kunyoosha nyumba na kila detail inakuwa imepatiwa. Bongo kweny kona za kuta kwa mfano hawawezi kunyoosha. Ukija kwenye vigae vya chooni au bafuni ni kichekesho.
 
Client wengi hawataki kutumia Engineers anaona gharama, anachukua fundi mtaani ,cjui designer wa graphic bhas hao wanaanza ujenzi Project ikifeli wanapelekana polisi
 
Nadhani Mafundi wapo.
Na asili ya hizo nyumba ni kumwaga ZEGE JUU .
Kwa hiyo nyumba iweze kuhimili hilo ZEGE
Ukipata fundi wa kufanya hivyo na gharama uwe Tayari kuimudu bila shaka huwezi kupata shida
 
Huwezi shindana na maji, narudia, huwezi shindana na maji, narudia
 
Kutana namimi iwapo nyumba yako Ina vuja Mimi nakushauri vzr nyumba haito vuja NAKAMA Ina vuja ninadhibiti kabisa nyumba yako inakua salama number yng hiyo @lwimikowaterprooftz 0716354056 chimbia bati ndani
Weka mfeleji mkubwa tumia bati ya kawaida yn usitumie mgongo Mpana zingatia slop FUNGA mkanda juu wa zege yenye resho kubwa sana hapo huto hitaji water proof ukibugi hapo lazima unitafte nikuwekee water proof ili nyumba yako iwe salama.
 
Nyumba hizo ni hatari sn. Sitarudia tena. Zimenipa HASARA KUBWA SANA. Nimeamua kuezeka kawaidi. Sasa nafurahia kuwa nyumbani kwangu kwa...
Hukutumia wataalamu mf Engineers
 
walio wengi wanaojiita mafundi wa mapaa si mafundi wa kweli. Tafuta fundi mzuri na utaachana na story za vijiweni!
hahahah

sio ndio wale mafundi maiko wanakwambia Gari zile BMW sio gari kabisa , anakwambia pita garage zote za Mjini namba D kibao za BMW zimepaki …ukimuuliza una ujuzi rasmi wa kutengeneza yale Magari anaishia kukutajia makanja nja wenzie wanaojifanya wajuaji

Tatizo letu ni umaskini na kupenda kuonekana wa kisasa

style mpya bado haijaenea na wewe pesa ya mawazo unakubali nyumba yako kugeuzwa kitengo cha mafunzo kwa vitendo cha VETA
 
Juu wanatakiwa wamwage jamvi/Zege, sio bati, Mbona hizo hotel za watalii zanzibar hazifuji, na mfumo wanaojenga wa mabati ni hidden 🤔
 
huu uezekaji asili yake ni kutoka uturuki,lakin tofauti yetu na wenyewe n kwenye paa wanamwaga jamvi ila kwa kwetu
Asili ya Flat + hidden roof ni uturuki, samahani utupatie chanzo cha hiyo taarifa yako mkuu.
 
View attachment 2924216
Kumekuwa na malalamiko mengi kuwa nyumba za kuficha Bati maarufu kama Contemporary au Hidden Roof zina shida ya kuvuja sana...
Watu wengi hukimbilia hidden roof kukwepa gharama za nyumba za kawaida yani (mgongo wa tembo) matokeo yake hukutana na gharama mara mbili baada ya kutokea kuvuja n.k.

Ukweli ni kwamba Hidden roof hubeba bati chache na mbao pia huwa chache.

Nyumba yoyote ili bora inahitaji budget yakuelewe sio kwamba mafundi wengi hawajui kutengeneza Hidden roof but budget yako ndo inapelekea low quality.

Ili mtu apate nyumba ya Hidden roof isiyo changamoto inabidi awe na ramani ya nyumba, ujue gharama za ramani hiyo andaa mahitaji, tafuta fundi mzuri ujenge.

Jambo la mwisho ni usimamizi wakati wa ujenzi hapo ndo watu huibiwa vifaa (materials) na hutokea low quality.
 
Back
Top Bottom