Mbona malalamiko mengi kwenye nyumba za kuficha Bati (Hidden Roof), Mafundi wanakosea nini hadi zinavuja?

Hapo ndo watu hukosea mfano ramani unatakiwa hata gata ujue ina kama wapi gata za pembeni mwa ukuta ni hatari sana maana watu hutumia ukuta na matifali kama sehemu ya gata kwa maana hiyo lazima tu tofali litavyonza maji na kuvuja .gata inabidi usukwe na nondo na zege la kokotote na isiwe ni sehem ya ukutwa yaan iwe kama linta na ukimwambia mtu gharama za hapo anakuwa mkali sana. Matokeo yake wanasakafia ukuta sdijui na kuwwka tails
 
Mimi mwenyewe hapa nina msala wa kubadili paa la nyumba. Mafundi wengi hawawezi upauaji huu. Fundi wangu kanitia hasara sana
Ukishaakosea gati ni shughulia mtu ameunganisha gati na ukuta sehemu ya ukuta haiwezi kuwa kutengeneza water proof ya maana maana ni lazima,zitavyonza maji tu .gati lazima uisuke na nondo na zenge la maana
 
Kuwekeza kawauda ni nzuri kuliko hidden roof, kwanza shep zake ni mbaya
 
Tatizo siyo mafundi ila ni sisi ambao tunakurupukia vitu bila kuangalia mazingira. Hizo nyumba za aina hiyo hazifahi kwenye maeneo yenye mvua nyingi kama mikoa ya Dar, na mingine ambayo inapata mvua kubwa kwa mwaka.

Hizo nyumba zinapaswa kujengwa kwenye mikoa yenye mvua kidogo kama baadhi ya maeneo ya Singida, Dodoma ambako wananchi wake wamejenga nyumba za tembe.

Ukiona mtu anaishi Mwanza, Kagera, Dar, na baadhi ya maeneo ya Morogoro anajenga nyumba ya aina hiyo huyo ni wa kumuonea huruma. Mtawalaumu mafundi vishoka bure kwa sababu na wao hawajui misingi ya ufundi.
 
Sad truth....
 
Mkuu usije kujaribu kujenga hizi nyumba otherwise muandikishane kwenye vyombo vya sheria.Tatizo mafundi wengi wanafosi kuzijenga ila uwezo wao mdogo
 
Kuvuja ni tabia ya mafundi Wetu kukosa umakini, uelewa, exposure, precission,

Mfano Fundi anapoteza 1mm Kila 1m
Je kwa 10m atamuwa akapoteza mm ngapi??

Ukimwambia anajibu rahisi " hiyo Haina shida"

Hawa mafundi waende shule kwanza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…