Chadema kilianzishwa kwa misingi ya kidemokrasia, na lengo kuu ilikuwa kuionesha dunia na nchi kwa ujumla jinsi demokrasia ya kweli inavyotakiwa kufanya kazi, ndio maana chama kikaitwa chama cha "demokrasia na maendeleo". Katika kuthibitisha hilo chama kilianza kwa kutengeneza katiba ya chama ambayo ilikuwa inamruhusu mwenyekiti wa chama hicho taifa kukaa madarakani kwa vipindi viwili vya miaka mitano mitano, na baada ya hapo uongozi wake unakuwa umeisha kikatiba, hivyo anampisha mungine ambae atachaguliwa kupitia uchaguzi mkuu wa chama, kisha yule alieshinda atachukua uongozi wa chama aanzie pale alipoishi mwenzie na kukiendeleza zaidi kwa lengo la kukiimarisha chama ili kije kishike madaraka na kuwaongoza wanachi kupitia mifano halisi ya uongozi wa chama chao. Sasa kitendo cha mwenyekiti wa sasa kwenda kinyume na katiba ya chama au desturi ile waliyoanzisha wenyekiti wenzie waliomtangulia kwa kupokezana uongozi kwa njia ya amani na demokrasia, huku ni kuvunja katiba na sheria za chama. Na viongozi wa aina hii siku wakiingia madarakan watabadilisha katiba ya nchi kama walivyofanya kina M7, ili aweze kututawala milele yeye na familia yake. So kwa sifa zake hizi hapo juu, tayari jamaa ni dikteta wa chama ndo maana watanzania wengi hatuwezi kumruhusu aje awe dikteta wa nchi.