Mbona mwanamke ukimkataa anakuchukia sana?

Mr_S

Senior Member
Joined
Apr 2, 2022
Posts
108
Reaction score
89
Ndugu zangu mimi kuna jambo huwa silielewi kabisa kuhusu wanawake/ mwanamke: "ukiwakataa huwa wanakuwa na chuki kali sana dhidi yako haijalishi mpo katika mazingira (hata kazini/biashara) gani."

Kwanini hawa wenzetu huwa suala la kukataliwa wanalibeba kwa uzito sana. Mbona wao wanatukataa kila siku sisi huwa tunasema "sawa tu".

Unaweza ukasema si vizuri kumkataa mwanamke lakini vipi kama ni mke wa mtu ? Tena unaweza kumwonyesha wazi kwamba huwezi kuwa na mahusiano naye kwa sababu yeye ni mke wa mtu lakini bado hilo suala halitokuepusha na chuki yake dhidi yako.

Mbaya zaidi ujikute katika mazingira ambayo unahitaji kuonana naye kwa masuala ya kazi labda mfanyakazi mwenzako au mtu ambaye huwezi kuepuka kuonana naye basi atakuonyesha wazi wazi kwamba anakuchukia na hataki kuongea na wewe.

Natamani nipewe ufafanuzi kuhusu jambo hili, na jinsi gani naweza kukabiliana nalo hasa ninapokuwa na sababu nzuri ya kumkataa mwanamke.
 
Tabia chafu sana hiyo na usirudie....
Hasa kwa siku muhimu kama ya leo Nyerere day.
Unamkataaje mtoto wa watu?
Inamaana kakataliwa na nyerere pia.
Kuna mke wa mtu ananitega sana. Sasa nampotezea basi sasa hivi hanipendi kabisa, hata tukizungumza ananipa majibu mabaya tu
 
Sio kumkataa tu yaani hta mkiachana anataka uharibikiwe akiona umepata mwangaza kidogo tu anajirudisha ukimpotezea anaanza kulalamika
Anataka kujua mwanamke uliyempata baada ya kuachana naye yukoje: mzuri au mbaya!
 
Kuna kidemu fulani cha chuga kama kidume😂😂😂nilikitema maana sinaga mazoea ya ovyo basi kimeanza chuki za kunipakazia eti mara natembea na fulani mara ivi!! Wakati sina time nacho wala hao anawataja sina hata mazoea nao
 
Ilishanikuta mazingira ya kazi nikaamua liwalo na liwe,ila alinichukia sana,usiombe mwanamke awe na kinyongo na wewe.
N.B:Chanzo kikuu ni ubinafsi.
Ndugu yangu wewe, mimi yananikuta yaani majibu ninayopewa hayaendani kabisa na muktadha wa mazungumzo. Halafu hata usoni hanitazami.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…