Mr_S
Senior Member
- Apr 2, 2022
- 108
- 89
Ndugu zangu mimi kuna jambo huwa silielewi kabisa kuhusu wanawake/ mwanamke: "ukiwakataa huwa wanakuwa na chuki kali sana dhidi yako haijalishi mpo katika mazingira (hata kazini/biashara) gani."
Kwanini hawa wenzetu huwa suala la kukataliwa wanalibeba kwa uzito sana. Mbona wao wanatukataa kila siku sisi huwa tunasema "sawa tu".
Unaweza ukasema si vizuri kumkataa mwanamke lakini vipi kama ni mke wa mtu ? Tena unaweza kumwonyesha wazi kwamba huwezi kuwa na mahusiano naye kwa sababu yeye ni mke wa mtu lakini bado hilo suala halitokuepusha na chuki yake dhidi yako.
Mbaya zaidi ujikute katika mazingira ambayo unahitaji kuonana naye kwa masuala ya kazi labda mfanyakazi mwenzako au mtu ambaye huwezi kuepuka kuonana naye basi atakuonyesha wazi wazi kwamba anakuchukia na hataki kuongea na wewe.
Natamani nipewe ufafanuzi kuhusu jambo hili, na jinsi gani naweza kukabiliana nalo hasa ninapokuwa na sababu nzuri ya kumkataa mwanamke.