Mbona Rais Samia akienda msikitini TV hazimuoneshi?

Aiseee, umewaza sanaaa, ila sio mbaya ntamuambia jamaa mmoja ivi akutumie picha zake 😊
 
Hasa TBC
 
Jinsia yake na hata dini kwa sababu kuna sheria ki dini ambazo kwa mwanamke haopendezi kuonyeshwa basi inatosha tu kuonekana akishiriki katika maombi ya hadhara nayopia ni ibada.
 
Kuna kujionesha "ucha Mungu" na kuna kutaka sifa za kijinga!! Ah kwanini TV ziwafuate viongozi katika nyumba za ibada ikiwa serikali haina dini?
 
Siyo kila udwanzi aliokuwa akifanya mwendazake mama aige,anaenda church kuwasimanga wananchi utadhan watoto wake vile,lawama kila siku,sasa alikuwa anaenda for prayers au kudanga
Wewe nimvuta bangi?
 
Jinsia yake na hata dini kwa sababu kuna sheria ki dini ambazo kwa mwanamke haopendezi kuonyeshwa basi inatosha tu kuonekana akishiriki katika maombi ya hadhara nayopia ni ibada.
Well said.
 
Haitakiwi kiongozi yeyote kwenda kuhutubia Taifa akiwa kwenye nyumba yake ya ibada..

Ibada ni suala lake binafsi..

Kutoa amri na kufukuza watu wakati unahutubia kanisani sio sahihi
Aaaah nakumbuka hayati alimtumbua aliyekuwa Mkurugenzi wa TANESCO....Felichesm Mramba...akiwa kanisan huko Bukoba
 
Ukumbuke kwa imani ya kiislamu wanawake wanakaa nyuma, na silazima akaswalie msikitini wengi huswali nyumbani
 
Ibada sio matangazo. Ni mazungumzo/maombi ya Mja na Mola wake. Hizo kiki za Matv nk ni mambo ya maonesho na Mungu hapendi. Huenda mama pia si mpenzi wa hizo mambo ndio maana hata TBC siku hizi wanaonesha zao tu Ubongo Kids. Hakuna tena habari za Kishindo Awamu ya ngapi sijui na vipindi kwa mapambio kwa mwabadamu.
 
Kwa imani ya kiislam mwanamke akiswali nyumban anamalipo makubw Zaid kuliko kuswalia msikitini so mam itakuw Ana swali San ikulu c msikitini
 
Alionyeshwa mara moja tu kule Unguja siku ya kumbukumbu ya miaka 49 kifo cha Karume, akiwa amekaa na mke wa Hussein Mwinyi.

Kwa waislam wanawake mara nyingi huwa hawaonyeshwi na kamera za runinga, hata ukiangalia zile ibada za siku ya ijumaa kwenye runinga ni mara chache sana kuwaona wanawake.

Hawezi kwenye hadhara ya kidini akasimama na kuongea. Tofauti na sisi wakristo, mara nyingi tu kinadada na kinamama wanasoma masomo pale mimbarini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…