Sawa, lakini tayari serikali imeshahama sasa. Haileti mantiki kurudi maana kufanya hivyo hakupunguzi gharama bali kuziongeza zaidi. Wizara zote ziko Dodoma. Na inaeleweka hivyo. Shida inakuwa wapi?
Kwani ilipotungwa sheria kuwa makao makuu ya nchi yatakuwa Dodoma kulikuwa na makosa katika hilo?
Gharama zipo na zitaendelea kuwepo lakini haina maana kuwa sasa viongozi wa juu waanze kurudi kufanya matukio ya kitaifa Dar es Salaam. Kama maamuzi ya kuijenga Dodoma yalipitishwa basi utekelezaji wake uendelee. Serikali ilianza kuhamishiwa Dodoma kuanzia Rais wa tatu, wa nne na wa tano (aliyefanya kazi kubwa zaidi). Sasa “kazi iendelee” iwe na uhalisia maeneo yote muhimu yenye maslahi kitaifa.
..hata mimi nakubaliana na wewe kwamba kwa Dodoma " kazi iendelee " wasirudi Dsm.
..ila tukubali kwamba ulikuwa sio uamuzi wa busara, hivyo tukubali kubeba mzigo wa HASARA iliyosababishwa na uamuzi huo.
..fedha zilizotumika kujenga Ikulu ya kifahari, maofisi ya serikali, nyumba za viongozi, kwa maoni yangu zingeweza kuelekezwa kwenye miradi inayogusa wananchi wengi zaidi huko VIJIJINI.
..viongozi wa WANYONGE walikuwa na chaguo la kujenga ikulu ya kifahari, au kujenga miradi ya kilimo cha umwagiliaji, wao wakachagua ikulu ya kifahari.
..nashauri serikali ihamie Dodoma moja kwa moja pamoja na kwamba zoezi hilo limesababisha hasara kubwa.